Category

News

Category

Mamba aliyenusurika kufa Vita Kuu ya Pili mjini Berlin na ambaye kulikua na tetesi- zisizo za kweli- kwamba alikua ni wa kiongozi wa Nazl Adolf Hitler amekufa katika hifadhi ya wanyama iliyoko mjini Moscow. “Jana asubuhi, mamba huyo aliyefahamika kama Mississippi Saturn alikufa kutokana na uzee. Alikuwa na umri wa miaka takriban 84 – umri wa kuheshimiwa sana ,” ilisema hifadhi ya wanyama. Saturn alitolewa kama zawadi kwa hifadhi ya wanyama ya Berlin mwaka 1936 muda mfupi baada ya kuzaliwa nchini Marekani. Alitoroka hifadhi ya wanyama baada ya kupigwa mabomu mwaka 1943. Wanajeshi wa Uingereza walimpata miaka mitatu baadae na kumtoa kwa Muungano wa Usovieti. Jinsi alivyoishi miaka yote hiyo limesalia kuwa ni jambo la muujiza, lakini tangu Julai, 1946 mamba huyo amekuwa akitembelewa sana na wageni mjini Moscow. . . . . “Hifadhi ya wanyama ya Moscow imekuwa na heshima kubwa ya kumtunza Saturn kwa miaka 74 ,” imesema…