Author

admin

Browsing

Mapenzi nimoja ya kitu kinacho watesa  watu wengi ulimwenguni ,lakini pia mapenzi ni moja ya kitu kinacho  wapa watu wengi   furaha katika maisha yao.Na kama unavyo juwa mapenzi ya siku hizi  yamekuwa na maigizo mengi uhalisia ni mchache ,na wahenga walisema penzi kitovu cha uzembe na ukipenda unazembeka kwelikweli Katika maisha ya mapenzi kumekuwa kuna kupenda ukatendwa ,na kuna kupendwa ukatenda ,na kuna kupendwa  ukapenda,lakini pia kuna kutendana yani nyote wawili mkavurugana yote haya husababishwa na maisha ya watu wawili walioamua kuwa na mahusiano hapa na maanisha mahusiano kati ya mwanaume na mwanamke . Kuna mgawanyiko mkubwa sana katika maisha ya kimahusiano wapo wanao ishi karibu karibu na wapo wanao ishi mbali mbali  ,umbali huo huwenda kutokana na kazi au masomo  nakusababisha wapendanao kuishi  mbali  na kuonana mara chache . Leo hii nakuletea kisa cha wapendanao wawili walio kuwa wakiishi karibu  kwa mapenzi makubwa na yenye uaminifu lakini baada ya…

Mamba aliyenusurika kufa Vita Kuu ya Pili mjini Berlin na ambaye kulikua na tetesi- zisizo za kweli- kwamba alikua ni wa kiongozi wa Nazl Adolf Hitler amekufa katika hifadhi ya wanyama iliyoko mjini Moscow. “Jana asubuhi, mamba huyo aliyefahamika kama Mississippi Saturn alikufa kutokana na uzee. Alikuwa na umri wa miaka takriban 84 – umri wa kuheshimiwa sana ,” ilisema hifadhi ya wanyama. Saturn alitolewa kama zawadi kwa hifadhi ya wanyama ya Berlin mwaka 1936 muda mfupi baada ya kuzaliwa nchini Marekani. Alitoroka hifadhi ya wanyama baada ya kupigwa mabomu mwaka 1943. Wanajeshi wa Uingereza walimpata miaka mitatu baadae na kumtoa kwa Muungano wa Usovieti. Jinsi alivyoishi miaka yote hiyo limesalia kuwa ni jambo la muujiza, lakini tangu Julai, 1946 mamba huyo amekuwa akitembelewa sana na wageni mjini Moscow. . . . . “Hifadhi ya wanyama ya Moscow imekuwa na heshima kubwa ya kumtunza Saturn kwa miaka 74 ,” imesema…

Benki ya NMB yatangaza Hatua za Kuwapunguzia Mzigo Wateja wake Kutokana na Janga la Covid-19  Hatua kuchukuliwa kulingana na mahitaji ya Wateja wa Biashara Ndogondogo na za Kati  Suluhisho pia kutolewa kwa Wateja Wakubwa Dar es Salaam, Mei 21, 2020: Benki ya NMB Plc leo imetangaza unafuu wa ulipaji mikopo kwa Wateja wa Biashara ndogo na za kati (SME/MSME) na wakubwa ili kuwasaidia kukabiliana na madhara yaliyotokana na janga la COVID – 19 kwenye biashara zao. Hii ni jitihada ya benki katika kutoa ahueni kwa wateja wake hususani sekta zilizoathiriwa zaidi na janga la COVID-19. Takribani wateja 412 biashara ndogo na za kati wameshapata ahueni hii kwa kupitia likizo ya marejesho ya mikopo yao na wengine wakiongezewa muda wa kulipa mikopo hiyo ili kuwasaidia kukabiliana na madhara yaliyoletwa na COVID – 19 katika biashara zao. Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NMB , Ruth Zaipuna alisema athari ambazo zimetokana na…

Zaidi ya watoto 100 wenye afya wamezaliwa kutoka kwa wanawake wenye maambukizi ya virusi vya corona katika mji wa magharibi mwa India wa Mumbai. Watatu kati ya watoto 115 walizaliwa kwa akinamama wenye virusi katika hospitali kuu ya Manispaa ya Lokmanya Tilak  – katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita ,awali walipatikana na Covid-19, lakini vipimo vya madaktari vilionyesha kuwa hawakua na virusi, wamesema madaktari. Wanawake wengine wawili wajawazito walifariki dunia hospitalini, mkiwemo mmoja ambaye alikufa kabla ya mtoto wake kuzaliwa. Huku ukiwa na watu takriban 24,000 walioripotiwa kuambukizwa corona na zaidi ya vifo 840 hadi sasa, mji mkuu wa biashara na burudani wa Mumbai umekua ni kitovu cha Covid-19. Zaidi ya nusu ya watoto walizaliwa kwa wanawake walioathiriwa hospitalini -pia katika hospitali ya Sion – walizaliwa kwa njia ya upasuaji, huku waliosalia wakizaliwa kwa njia ya kawaida, walisema maafisa. Hamsini na sita kati yao walikua ni wa kiume, huku 59…

Rais wa Marekani Donald Trump ametoa amri jana ya bendera kushushwa nusu mlingoti kwa siku tatu mfululizo, kuomboleza vifo vya Wamarekani waliokufa kutokana na virusi vya corona. Trump ameamrisha hatua hiyo, baada ya idadi ya vifo vinavyotokana na ugonjwa wa COVID-19 kukaribia 100,000 nchini humo. Aidha Trump amesema bendera zitabakia nusu mlingoti Jumatatu ijayo ambayo ni Siku ya Mashujaa nchini humo, kuwakumbuka wale ambao wamepoteza maisha wakilitumikia jeshi la Marekani. Ingawa idadi ya vifo vya kila siku nchini humo haikuongezeka, watu bado wanaendelea kupoteza maisha, na hesabu kamili inapindukia vifo 94,500 – likitajwa kuwa ni taifa lenye vifo vingi ulimwenguni. Wiki hii Marekani imerikodi vifo 1,300 kwa siku, vinavyotokana na virusi vya corona.

Virusi vya corona vimewaathiri wahudumu wa afya wapatao 10,000 nchini Iran, kulingana na taarifa za vyombo vya habari vya jana Alhamisi zilizomnukuu Naibu Waziri wa Afya Qassem Janbabaei, ambaye hakufafanua zaidi. Ripoti za mapema wiki hii, zimesema idadi ya wafanyakazi wa huduma ya afya walioambukizwa virusi hivyo ni 800 tu. Iran imesema zaidi ya watu 100 miongoni mwa wa wafanyakazi hao wamefariki. Iran ni taifa la Mashariki ya Kati linalokabiliwa na mripuko mbaya zaidi wa virusi vya corona, ambapo takriban watu 7,249 wamepoteza maisha kati ya watu 129,000 waliothibitishwa kuambukizwa virusi hivyo. Takwimu hizo ni pamoja na vifo zaidi ya 66 vilivyotangazwa jana Alhamisi na msemaji wa Wizara ya Afya Kianoush Jahanpour.