Uncategorized

ITAKULIZA! JIFUNZE KUTOMUUMIZA UNAYEMUHITAJI BADO/KISA CHA RAJAB NA PENDO

Mapenzi nimoja ya kitu kinacho watesa  watu wengi ulimwenguni ,lakini pia mapenzi ni moja ya kitu kinacho  wapa watu wengi   furaha katika maisha yao.Na kama unavyo juwa mapenzi ya siku hizi  yamekuwa na maigizo mengi uhalisia ni mchache ,na wahenga walisema penzi kitovu cha uzembe na ukipenda unazembeka kwelikweli

Katika maisha ya mapenzi kumekuwa kuna kupenda ukatendwa ,na kuna kupendwa ukatenda ,na kuna kupendwa  ukapenda,lakini pia kuna kutendana yani nyote wawili mkavurugana yote haya husababishwa na maisha ya watu wawili walioamua kuwa na mahusiano hapa na maanisha mahusiano kati ya mwanaume na mwanamke .

Kuna mgawanyiko mkubwa sana katika maisha ya kimahusiano wapo wanao ishi karibu karibu na wapo wanao ishi mbali mbali  ,umbali huo huwenda kutokana na kazi au masomo  nakusababisha wapendanao kuishi  mbali  na kuonana mara chache .

Leo hii nakuletea kisa cha wapendanao wawili walio kuwa wakiishi karibu  kwa mapenzi makubwa na yenye uaminifu lakini baada ya muda wakatengana kutokana na shughuli za kikazi.

Hapa namzungumzia Miss Pendo pamoja na mpenzi wake Bwana Rajabu ,wawili hawa  waliishi kwa upendo mkubwa sana na uwaminifu mpaka kupelekea kutambulishana kwa wazazi  ,ndugu jamaa na marafiki wanao wazunguka  kwajili ya kuweka wazi mahusiano yao.

Upendo wao ulipelekea  Rajabu kuamua kumtafutia nafasi ya kazi mpenzi wake Pendo katika kampuni aliyokua  akifanyia kazi ili kujipatia pesa za kujikimu kimaisha  ,Rajabu alifanikiwa kupata nafasi hiyo ila  ilipatikana katika moja ya shina ya kampuni hilo ambalo linapatikana mkoani Dodoma .

Hivyo Pendo alilazimika kwenda kuishi Dodoma  kwajili ya kazi na kumuacha mpenzi wake mkoani Morogoro na yeye akiwa anaendelea na kazi,Hapa ndipo penzi  la wapendanao hawa lilipo ingia dowa ,dowa ambalo limepelekea  wawili hawa kila moja kuwa na maumivu makubwa kutokana na vitendo walivyo jikuta wakitendeana .

Pendo alipo fika mkoani Dodoma alianza kazi huku akiwa anajuwa kabisa nipo katika mahusiano na Rajabu ,nae Rajabu aliendelea nakazi huku akijuwa ninae mpenzi wangu pendo .Ila punde tu mambo yalibadilika mara baada ya Pendo kunogewa na Jiji la Dodoma na kuzijuwa kona zake .

Pendo akiwa Dodoma anaendelea na kazi akaingiwa na jini mkata kamba na kujikuta anaingia na tamaa nakujikuta ana anzisha mahusiano na mwanaume mwingine kumsahau mpenzi wake kabisa ,Ndipo hapo penzi lao lilipo anza kuwa shubiri Pendo aka  nogewa na penzi jipya  na kumsahau  mpenzi wake kabisa ,penzi la mwanaume mpya kwa Pendo lili noga hadi kupelekea Rajabu kujawa na kuwa   fumania wakiwa ndani.

Rajabu;Pendo  ni nini hiki unafanya ina maana umesahau kwamba upo katika mahusiano ?

Pendo;kimya

Rajabu ;aya sawa endelea na maisha yako

Rajabu aliondoka zake ana kumuacha Pendo akiwa na mpenzi wake mpya,alipata wakati mgumu sana kusaha tukio hilo kama unavyojua mtu unae mpenda akikufanyia kitu cha kuumiza  maumivu yake huwa

hayaelezeki na hata ukimu elezea mtu hawezi elewa jinsi unavyo jisikia   au uanavyo hisi ndani ya moyo wako .

Siku kadhaa baadae Rajabu nae alipata mwanamke mwingine ambae alishika nafasi ya pendo kipindi Pendo yupo mbali na Rajabu  bila kuwa na mawasiliano yeyote kwa muda wa miezi kadhaa

kama unavyo jua mwanaume hawawezi ishi kwa muda mrefu bila kuwa na mahusiano na mwanamke nikutokana na kutofautiana kwa maumbile ila mwanamke anaweza kuvumilia bila kupata usumbufu  hapa sasa tunaongelea masuali ya kisayansi na jinsi ya uumbaji wakimaumbile yetu  yalivyo na utofauti.

Mara baada ya Rajabu kupata mwanamke mwingine na kumuamini huwenda Pendo hatorudi tena kumbe mawazo yake yalikuwa tofauti ,wakati anawaza hivyo  kumbe Pendo alikuwa  anajiaanda kuja kumuomba radhi ili waweze kuendeleza mapenzi yao wakati huo pendo tayari Alisha amuwa kuachan kabisa na Yule sponsor wake .

Pendo alirudi kwa Rajabu na kumuomba radhi ili warudi kuwa wapenzi tena kwani mapenzi yao yalikuwa yana fahamika na yalisha barikiwa hadi na ndugu pamoja na wazazi ,Rajabu alikubali  kwakuwa alikuwa ana mpenda sana pendo na kumwambia  amemsahe na bado ana mpenda na yeye ndio mwanamke wa maisha yake  ,bila kumwambia kuwa tayari anae mahusiano na mwanamke mwingine

Hapa ndipo unakuja usemi usemao  ukipenda  utapendwa na ukitendwa utatenda.

Pendo;Rajabu mpenzi nisamehe nishetani tu alinipitia ila mimi bado nakupenda

Rajabu;mmmh usijali pendo nilisha kusamehe kabla hujaniomba msamaha na yote  nikwasababu nakupenda

Pendo;kweli umenisamehe  nawasiwasi sana mana najuwa nimekukosea pakubwa

Rajabu;ndio wala usiwe na wasi wasi mimi nimekusamehe kabisa mpenzi wangu

Pendo ;nashukuru mpenzi naahidi sito rudia tena

Rajabu ;sawa usijali kuwa na amani tu mpenzi

Msamaha ulipita maisha ya wapenzi hao yaliendelea bila Pendo kujua kuwa mpenzi wake tayari alikuwa na mahusiano na mwanamke mwingine .

Siku moja pendo aliamuwa kum sapraizi mpenzi wake kwa kwenda kumtembelea nyumbani kwake mjini Morogoro bila kumwambia, kama unavyojua kwenye mapenzi kuna vitu vingi vya kufanya ili tu kulifanaya penzi lenu lizidi kunoga .

Pendo alikua anatoka zake Mwanza kikazi akaona sio mbaya safari yake iendelee hadi nyumbani kwa mpenzi wake Morogoro ili kumsabahi baada ya hapo ndipo arudi Dodoma kwaajili yakuendelea na kazi.wakati anapanga safari hakumwambia mpenzi wake kama atafikia Morogoro ila alipo karibia akampigia sim na kumwambia nakuja Morogoro na nimeshakaribia .

 

Pendo;mpenzi nakuja Morogoro nime kumisi   na nimesha karibia kufika hivyo naomba  uje kunipokea

Rajabu;sawa mpenzi usijali karibu

Pendo ;asante mpenzi

Pendo alofika Morogoro mjini  Rajabu alikuja kumpokea ,ila rajabu alionekana kama hayupo sawa ndipo pendo akaamuwa kumuliza kuna tatizo gaani

Pendo;vipi mpenzi mbona kama haupo sawa kuna tatizo

Rajabu;hapana ila leo hautaweza kufikia kwangu mana nina wagweni marafiki zangu wamekuja kutoaka mkoani

Pendo ;hilo ndolina kufanya uwe na wasi wasi hivyo kwani hao rafikizako hawajui kama wewe unae mwanamke mwenye mahusiano nae

Rajabu ;hapana sema najisikia tu vibaya wewe kuto kufikia nyumbani

Pendo ;basi sawa nipeleke tu kwa dada

Rajabu;sawa mpenzi ila usijisikie vibaya

Pendo;wala usijali mpenzi

Basi rajabu ali mchukuwa pendo nakumpeleka kwa dada yake ambae nae alikuwa anaishi hapo hapo Morogoro ,kama nilivyo kwambia pendo pia nimwenyeji wa mjini Morogoro .Basi rajabu alimfikisha pendo hadi kwa dada yake na kumuacha kisha yeye kurudi zake nyumbani kwake.

Kutokana na wasiwasi alio kuwa nao rajabu ilipelekea pendo kutilia mashaka kwamaba mbona mpenzi wake kama hayupo sawa  kuna tatizo gani ,ikabidi atoke kwa dada yake na kwenda kwa mpenzi wake ilikujuwa kuna tatizo gani ,alipo fika nyumbani kwa mpenzi wake  doooo;;;;;;;;;  pendo hakuwamini alicho kikuta  nakubaki na  mshangao mkubwa  baada ya kumkuta Rajabu yupo na mwamke mwingine ndani;

Pendo hakuongea sana wala hakutaka kuleta vurugu aliamuwa kumwambia rajabu ampe vitu vyake vilivyopo ndani ili aweze kuondoka

Pendo;Rajab???? Naomaba vitu vyangu vilivyopo ndani niende zangu

Rajabu ali ingia ndani na kumpa pendo  vitu vyake bila hata kusita  kisha akamwambia

Rajabu;pendo haya yote umeyasabisha wewe  kwa kipindi kile ulivyo nifanyia yale matukio yali  pelekea na mimi kuchukuwa uwamuzi huu

Pendo; lakini siuliniambia umenisamehe   na kwanini hukusema kama ulikuwa na mwanamke tayari ?

Rajabu; mwanamke huyu nilikuwa nae kwajili ya kunifariji kipindi wewe umeniacha na kwenda kwa mwingine ,naomba unisamehe mbona mimi nilikusamehe.

Pendo hakujibu nakuamua kuondoka  ,kama unavyo juwa mtenda akitendwa huwa anaona kama katendwa sana.

Pendo alirudi nyumbani na hakupata usingizi kabisa alichukua simu na kumpigia Rajabu ili waweze kuongea vizuri kwani aliondoka akiwa na hasira nakushindwa kuzungumza ,Rajabu hakuweza kupokea simu kwa wakati ule.

Pendo  aliamua  kupumzika  nakusubiri pakuche ili aweze kuwasiliana na mtu wa karibu na mpenzi wake ili aweze kumsaidia japo kwa ushauri tu ,palipo kucha alimpigia rafiki wa mpenzi wake alie fahamika kwa jina la Hafidhu na kumuelezea yalio tokea siku ya jana .

Pendo;Hallo  shem habari yako umeamka salama ?

Hafidhu;salama tu shem kwema ?

Pendo ;sio kwema shem nipo Morogoro nimeingia jana  sijafikia kwa Rajabu mana aliniambia  kwake kuna wageni  akanipeleka kwa dada yangu ,alivyo niacha tu nyuma nika toka kumfuata ilikujua ni wageni gani alionao ambao wamefanya mpaka  akawa na wasiwasi nakushindwa kunipeleka    kwake sasa chakushangaza nimefika kwake nimemkuta na mwanamke mwingine basi nikamwambia anipe vitu vyangu vilivyopo ndani na akanitolea kweli na akabaki na huyo mwanamke nilie mkuta nae ina maanisha mimi sina umuhimu tena kwake  shem hapa nilipo nimechanganyikiwa kabisa.

Hafidhu ;pole sana shem ,kwa yalio kukuta ila hiyo hali ya kukutolea vitu  huwenda alikuwa anaepusha vurugu ,na vitu si ulimwomba wewe mwenyewe akashindwa lakufanaya ,hata ingekuwa wewe shem ukikutwa katika hali kama hiyo lazima utashindwa lakufanya nakujikuta unatoa maamuzi ambayo hata wewe huta elewa ni nini unafanya.

Msomaji hapa sasa ndipo unakuja usemi wa shemeji nikama mjumbe unakula nae unachekana nae mwisho wa siku anakuja kukugeuka,  hahahah;;;;;;;;;;;;;

Basi pendo hakukata tamaa aliendelea kuhangaika kumtafuta mpenzi wake Rajabu ili waweze kuzungumza kwanini kafanya hivyo jitihada zake zilifanikiwa na mwisho Rajabu aliweza kupokea sim  na wakaanza kuzungumza.

Pendo;hallo ;;;Rajabu kwanini umefanya hivi jamani?

Rajabu;kimya …….

Pendo; si nina kuuliza ?

Rajabu ;sina cha kukujibu mana sina cha kujitetea bora ungekuta ata sms au picha ila umenikuta na kuniona kwa macho yako  kikubwa nisamehe tu nakiri nimekosa  ,mbona wewe ulinikosea na nika kusamehe ?

Pendo;kimya

Rajabu;nisamehe wewe  ndio mwanamke wa maisha yangu nakupenda ,huyu ulie mwona nimwanamke niliekuwanae kipindi kile umeniacha  alikuwa ananifariji  na nilivyo kupekleka kwa dada yako sikuwa nania mbaya .

Pendo;kimya

Mpaka sasa pendo ameshindwa kutoa jibu kwa mpenzi wake yupo njia panda hajui ni nini afanye

Penzi hili limeingia dosari  na kuwaacha wawili  hao wakiwa katika migogoro ya nafsi zao

Na kama unavyo juwa penzi likiingia dosari  linakuwaga chungu kama shubiri na inaweza kupelekea hata moja kuchukua uamuzi usio sahihi.

Msomaji  wangu una nini cha kumshauri Pendo pamoja na Rajabu ili waweze kurudi na kuishi kama hapo awali  na kuepusha kuchukua uamuzi utakao leta maafa kati ya wote wawili?

Write A Comment