Z Anto Awatolea Uvivu Wasanii Wenzake Wenye Tabia Hizi….!!

Msanii mkongwe wa muziki, Z Anto ambaye amewahi kufanya vizuri na nyimbo kibao kama Binti kiziwi, Mpenzi jini na nyingine ngingi, amefunguka na kuwachana baadhi ya wasanii wa bongo ambao wanatumia mahusiano ya kimapenzi kama njia ya kutafuta kuzungumziwa katika jamii na kusema huo ni ushamba.

Z Anto amesema kuwa kutoka kimapenzi na mtu ambaye amekuzidi umri kwa lengo la kutaka kuzungumziwa kwenye jamii au kutafuta kiki si jambo jema na halistahili.

“Mapenz ni uhuru haitajalisha ulimpenda yupo vipi mrefu mfupi, mnene au mwembamba, mkubwa ama mdogo ila kutoka kimapenzi na mtu aliyekuzidi umri kwa lengo la kutaka watu wakuzungumzie kwenye jamii inayokuzunguka kwa wasanii wenzangu wanasema kutafutia kiki ni ushamba” Z Anto aliandika Instagram.

Mbali na hilo Z Anto pia amesema anatarajia kurudi rasmi kwenye muziki wa bongo fleva kwa kuachia ngoma yake mpya na kichupa kipya Septemba 8, 2017 siku ya Ijumaa na kusema anaamini ngoma yake hiyo itamrudisha kwenye nafasi yake, kwa kuwa yeye siku zote hufanya muziki mzuri akiamini mashabiki wake.

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.