Wolper Amuwashia Moto Harmonize…!!

Mwanadada Jackline Wolper Kupitia Mtandao Wake Wa Instagram Aamua Kumtolea Maneno mazito Aliyekuwa Mpenzi wake wa Zamani “Harmonize” Baada ya Msanii Huyo kutoa Wimbo Wenye Kumponda Mrembo Huyo Uitwao “Nishachoka”

Hizi Ni Baadhi Ya Post Ambazo Mwanadada Wolper Amepost Kupitia Ukurasa Wake Wa Instgram

Soma Ujumbe wa kilichoandikwa Kwa Kila Post Aliyoandika Jackline Wolper Soma Hapa Chini

Jamani kweli maisha magumu sijui ndo stress kiufupi sielewi sasa naona umeamua umrithi mzee Yusuph baada ya kuacha yeye Taarabu uimbe ww kijana 😂😂Sikia buana ww umeto wimbo wa dk mbili sijui lkn jua mm nikisema niingie kwenye kazi yangu ya sanaa nitatoa SERIES ambayo itakuwa na mfanano wa ISIDINGO maana haitoisha!Sasa ww umenivumilia kwa lipi??Usitake nikufuru nipate dhambi ambazo hazina mashiko 😏Unanitungia nyimbo alafu unasema ooo unifikirii mtu mpk unaingia studio unaimba mipasho yako si inamaana nimekujaa kwenye koo mpk mwili yani mpk tukikupima group lako la damu tunaweza kupata WOLPER MASSAWE 😂😂😂Sikiliza nimelala chini,Nimekufumania,Nimekuta msgz za wanaokutafutia wanawake lkn sijawahi kuongea kwasababu najua nn maana ya mahusiano kuna kuachana alf mbaya zaidi nimepitia relationship tofauti so siwezi Kukuwekea sura ya choyo hivi ningekuwa na sura ya choyo ningekupokea ww ulivyonitongoza 🤣Maana niliwekwa vikao na watu tofauti kwa ajili nikuache!Eti una mabaya yangu!Kwa nilivyousikia wimbo wako ungekuwa na yangu ungeongea yoooote buana weeh Sasa una yangu Afu uingie studio uyaache??🤣😂Ur not serious!Nimekuvumilia nisikuongelee nikaona mashabiki wanataka sn kujua na watu walikua wanaongea mengi cz nilinyamaza!sasa Nimeongea kidogo tu umenijia na wimbo chaaaa!Hivi si utunge hata nyimbo ya kumsifia Sarah mzuri km Kim kardashian 😂😂😂Au nikupe mistari?Acha hizo buana watu tumepata magwiji wa kuziba viraka vya mioyo ilioumia basi usitafute choko choko Yakhee me napambana na penzi langu embu kaa tuliza roho yako na mwili ujue Sarah anahitaji muda wako kuliko muda wa ww kunitungia vijembe na vipanga na vikisu hehehehe…Mara umemtaja mama ako sasa,mm na yule mama wa watu tuna ugomvi gani km sio unataka uonekane huna hatia kwenye wimbo!Naheshimu sn wazazi kwasababu nimekuwa ktk mazingira ya kumuheshimu kila mtu!Mbona mm sijamtaja mama ako alikua anahusika na fumanizi…bwana bwana wee!Next time ukiimba hakikisha unaimba,Nililala sn studio ili nikusubiri ww,Nililia sn kwa ajili ya maumivu ulionipa,Yaani km ulivyoimba kwenye niambie huna kazi na senti lkn nikakupenda hivyo hivyo sasa uiweke kwenye matukio yako mabaya niliyoyavumilia!

Kwahiyo baada ya kuona mm nimeendelea na maisha yangu ukaona unitungie wimbo sumu hahahaha!Uongee ya kurudi asubuhi kisa kwenda kuchukua ela kwa Sarah afu Mm siimbi lkn kuna kitu kinaitwa call recorder nikisema nifanye kitu uenda Sarah atafika Italy kwa mabawa!Unasahau kuwa nina voice zako za juzi kati hapa ulizonipigia unalia lia km king’ora cha wagonjwa wenye hali maututi??Usitake niseme vyote usinichokonoe nimwage mivoice Afu mm sina hasara maana simfich m2 wangu k2. Ila ww na penzi lako la biashara ndo utakaepambana na yule mama kija wako!Niache kidogo bwana imba hata nyimbo ya kuhusiana na Tundu Lissu afu jina unaweka wasiojulikana asee utauza sn kuliko kumuongelea mtu ambae mmeachana afu kaamua ku moooooove on…..!Hivyo yani km umenimiss nipitie hata kwenye kale kanyimbo ulikoniopaka mafuta kwa mgongo wa chupa (#Niambie.) lkn sio kuniendea studio kuniimbia taarabu 🤣🤣Ujue tatizo lako unahisi mwanaume upo ww tu bongo 😝😝Polyeeee sn wimbo nimeusikia lkn nimependa beat tu….!Afu kuongea sipangiwi,kukwepesha ndo kitu niliachaga toka enzi nacheza makidamakida hehehe Kunyamaza kwa vitu vya kijinga pia siwezi hilo ndo tatizo langu….Haya wenye kutoa mapovu toeeeni weeeh nakuja na beseni,pipa km yatalipa ntapeleka dry cleaners niwauzie tupate wateja…!Afu mtakao pata ujumbe pia mscreenshot tu!afu pia sijaongea yotee cz nimejua sikuhizi watu wanauza mziki kwa kuchamba watu,so endelea kufanya kazi yako….!lkn kumbuka na mm msanii nikitoa series ntauza sn cz ni ukweli mtuuuupu

Haya kijana post nilizopost zinazo kuhusu zitachukua masaa mawili tu!Maana ukute navyokuweka hata hivi nakupa viewers wa nyimbo yako yenye stress,Na usije ukapata wanaume wenzio wenye stress za wanawake km ww!Tusilazimishane kuongea nimeshaachana na ww kiusalama ongelea vilivyopo sasahivi kwako na sio mm,Nilishatokaga huko kiurahisi unaweza ukadeal na style yako ya mziki bila KUNIHUSISHA maana unampa hofu pia BFF anahisi labda kuna kitu kumbe hakuna,Usiniharibie mahusiano yangu mapya kwa taarabu zako,BFF wangu ni bora kuliko wewe Afu nahisi km hayupo km Huyu yani huyu ni adimu staki kumpoteza kwa ajili ya watu km ww!Km aliweza kuziba maumivu yako na nakuona km trakatraka basi naomba uniache kijana Nimeandika nikijiamini km mtoto wa kike bila kumuogopa mtu yoyote….Nikuahidi usidhani mm Yesu akipigwa shavu la kushoto ageuze na la kulia ili apigwe tena,Mimi ni Jackie Wolper tena Massawe!Ambae siwezi kuacha kuongea ukinianza na maliza!Kwa wale wanaosema bora kunyamaza subirini ya wakute afu ndo mjipe huo ushauri nyie!ASANTENI
#NyamazaKuliaStudio
#NdioUkubwaHuo
#UlipendaPesaKulikoTrueLoveSasaPambanaNaPesaZake

#UmakondePiaAchaUshafikaMjini

Wolper Hakuishia Hapo Ili Kumuumiza Zaidi Aamua Kupost Picha Ya Boyfriend Wake Mpya Akiwa Kifua Wazi

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.