ZIFAHAMU SIRI KUU NNE(4) ZITAKAZO KUFANYA WEWE KUWA MPISHI WA FURAHA YAKO KILA SIKU

0

 

       MPISHI WA FURAHA YAKO
Wakati fulani nilipokuwa Mwanafunzi wa Shule ya Msingi,nakumbuka nilikuwa Mwanafunzi mtundu sana,kiasi kwamba hata tukiwa tunapewa adhabu za kuchapwa mimi nilikuwa sionyeshi dalili ya kukasirika,kimsingi uso wangu ulikuwa na FURAHA,tena nikiwa na chapwa bakora kwa kosa nililokuwa nimelifanya ndiyo kabisaa naweka na tabasamu!
Siku moja mwl wangu Kiingereza aliona anitolee uvivu akaniuliza“Emma kwanini unapenda kuchekacheka.?
“,,,kwasababu nina FURAHA,,,,” nilimjibu,lakini mwl hakurizika na majibu yangu,akaniuliza tena“Unaishi na nani nyumbani na hapa shule ni nani marafiki zako.?”
“Naishi na babu na bibi yangu na kwa hapa shule wote ni marafiki zangu” nilimjibu tena mwl wangu bila kuelewa kwanini alikuwa akiniuliza maswali yale!Alinichapa kama ambavo nilitakiwa kuadhibiwa kwakosa la kuchelewa kuwahi shule na nikarudi Darasani nikiwa na sikilizia maumivu lakini kama kwaida nilipo waona marafiki zangu nilicheka na siku ikaendele bila tatizo lolote.
Kwa wakati ule sikuwa nafahamu ni kwanini mwl alikuwa anataka kujua naishi na nani na nacheza nani,lakini sasa nimetambua kuwa FURAHA   ilikuwa inaanza Nyumbani asubuhi nikiamka huwa nakutana na Babu pamoja na Bibi yangu ambao nilikuwa nawapenda sana na baada ya hapo nilikuwa naelekea Shule na nilikuwa na tabia ya kusalimia kila mwanafunzi nitakae kutana nae,awe na mfaham au hatufahamiani nilazima nimsalimie.Sasa siku ikitokea Nimeamka babu hayupo,awe ame safiri au kaenda kazini mapema basi siku hiyo nitakuwa mwenye huzuni sana.Kimsingi nazijutia siku zote ambazo nilikosa FURAHA kisa tu babu alikuwa hayupo nyumbani asubuhi ilihali ningeweza kujiaminisha kuwa Babu kaenda kazini na akirudi nitamuona na nitamsalimia na kwa kufanya hivyo nisingekuwa na siku nakosa FURAHA ndani ya Moyo wangu,kwani ninatambua MIMI NDIYO MPISHI PEKEE WA FURAHA YANGU.
Katika Makala hii ya MPISHI WA FURAHA YAKO tutakwenda kuona njia mbalimbali ambazo ukiweza kuzizingatia utakuwa ni Mpishi Mzuri sana wa FURAHA yako.Twende pamoja!
    1.USIHIFADHI CHUKI.
NDIYO.!kama unataka kuwa moja ya viumbe wenye FURAHA zadi duniani basi jitahidi kwa hali yoyote ile Kuuweka Moyo wako Huru kutoka ktk vifungo vya chuki na hasira juu ya mtu,kitu au hali yoyote.Ladba nikukumbushe  “KUWA NA UPENDO KWA KILA MTU NI LAZIMA,LAKINI KUWANA UHUSIANO NA NI CHAGUO LAKO” Haya si maagizo yangu kwani hata Mungu wetu alie tuumba anaagiza Upendo kwa kila mtu na si kuwa na uhusiano na kila mtu,Hivyo basi unatakiwa kujiepusha na kumchukia Mtu yoyote kwa halia au namna yoyote.
Ukiweza kuwa na UPENDO na kila Mtu utakuwa umefanikiwa kwa kisi kikubwa kuwa na FURAHA isiyo na mipaka
 2.AMINI KTK UNAWEZO WAKO.
Natambua wapo ambao wanakosa FURAHA kwakuwa wanahisi kuna badhi ya mambo hawawezi kufanya!SIKILIZA!Wewe ni watofauti,Unauwezo na Akili ambazo si sawa na Mtu mwingine,wala haufananishwi na mtu yoyote,WEWE NI WEWE KAMA AMBAVYO YEYE NI YEYE.Iko hivi ndugu yangu!inawezekana unahuzuni ndani ya nafsi yako kwasababu rafiki,jirania au ndugu yako anauwezo wakufanya vitu ambavyo wewe huvuwezi kuvifanya,Labda kwa hali hii ikakufanya ujenge chuki juu yake,nakama tulivosema ukiwa na chuki ndani ya moyo wako FURAHA utaisikia kwa Jirani,USIJALI!kwamaana huyo ndio yeye na sio wewe! Chafunya sasa
JITAZAME,JIAMINI,JARIBU.Hakika hizi J3 zitakufanya utambue kuwa unaweza kufanya kitu tofauti na wenzako kwa maana wewe ni Watofauti!Kisha Muombe Mungu aendelee kukupa nguvu.Ingia kazini(jaribu)Fanya kwa namna yako wala hauhitaji kutazama wengine wanafanya vipi kwakuwa Mungu niwetu sote na wewe utafanikiwa.

       3.RIDHIKA NA KIDOGO UKIPATACHO,ENDELEA KUTAFUTA KIKUBWA.
Kiungo hiki chatatu kina Umuhimu mkubwa sana,Hata nikisema niandike yote hapa tutakesha,Labda nikupe mfano mdogo,Nilikuwa na marafiki wawili(X&Y) wote wa kiume na kwa nyakati tofauti walitokea kumpenda msichana mmoja mzuri sana na Mungu alimjalia kupata ufahamu wakutambua kuwa yeye ni Mzuri na wathamani kubwa au kwa lugha ya kawaida unaweza sema alikuwa ANAMARINGO TOLEO LA KWANZA,basi rafiki X alienda kutupa karata yake ya kwanza kwa binti mrembo,baada ya dakika chache zilizofuata rafiki Y nae alienda kutupa karata yake ya kwanza na kwakua mimi nilikuwa rafiki wa wote hawakuona haya kuja kunipa Majibu ya maombi yao.Siku ya manibu ilikuwa hivi,Rafiki X alikuja akiwa kainamisha kichwa chini,akiwa wenye huzuni sana,amekosa amani ndani ya Moyo wake,nika muuliza “vipi kaka bint mzuri kasemaje?” akanijibu “aah!Mimi sijui nina mkosi gani,eti kasema nisubiri anifikirie kwanza” kwakweli sikuwa na msaada wa kumpa zaidi ya kusubiri Majibu ya Rafiki Y ambaye alikuja akiwa nafuraha mnoo,kicheko kilikuwa cha kiwango cha Lami!nNikamuuliza “vipi kaka, bint mzuri kasemaje?” akanijibu “sikutegemea kabisa eti kanambia Nisubiri anifikirie kwanza” Heeeh!nilishangaa tena,nika hoji“Sasa mbona unachekelea wakati bado hujakubaliwa?” Majibu yake ndio ningetamani hata wewe uyatafakari ikiwezekana yatumie,alinijibu hivi “Mwanzo ni Mugumu lakini huu wakwangu Unamatumaini,kwanini nisifurahi?”alijibu na kuniacha swali,baada ya kuona simoi majibu akaongozea “Kesho tena naenda kumkumbusha” hii simulizi ni ndefu mno lakini kifupi ni kwamba leo hii unavosoma makala hii Rafiki Y amefanikiwa kufunga ndoa na bintmzuri wakati Rafiki X bado anapambana na hali yake!UNAONA!mimi nimejifunza kitu,naamini na wewe umejifunza pia,kuwa inatupasa kuridhika na kufurahi kwa hatua yoyote tunayo piga ktk kila jambo lakini tusisahau kuwa tunapopataka bado hatujafika.Kwakufanya hivi utakiwa ni mtu wa FURAHA siku zote.

   4.KUMBUKA KUJIPONGEZA.
Hapa ule Usemi wa“ Kazi na dawa ”ndiyo utahusika zaidi,Labda nikuulize, ww ulivo sikia DAWA ulijua ni dawa ya malaria au?Basi kama ulikuwa hujui Dawa inayo zungu mziwa hapa ndiyo kujipongeza kwenyewe.Wapo wachache ambao huwa wanapenda Kufanya jambo au kazi yoyote wakisubiri Pongezi kutoka kwa watu wanaowatazama,POLE! kaka na Dada yangu unaesoma makala hii binadamu wengi wanachuki na wivu sana,yawezekana kabisa wanajua unastahili kupongezwa lakini kutokana na wivu na kinyongo au kwamslahi yao binafsi Wanayo jua wao wakaacha Kuku Pongeza,zaidi ya yote wanaweza kukwambia “eeh! Kiongozi!hapa hakuna ulichofanya” INAUMA! Kwamaneno kama Haya ni lazimana wakuharibie siku yako na Ukajikuta na huzuni siku nzima.!
SIRI ni moja tu ndugu yangu JIPONGEZE MWENYEWE,Skiliza.!Mungu alipo umba Dunia na kila kilichomo ndani yake alikuwa peke yake,hapakuwa na kiumbe wakumsifia au kumpongeza,Lakini Mungu alijua ipo sababu ya yeye kujipongeza nandiyo maana alipo maliza uumbaji alitazama kazi aliofanya nakuona kuwa ilikuwa bora na ya kupendeza,akajipongeza na mapunziko ya masaa 24 ya siku ya saba.
Inawezekana wewe ni mwanafunzi umepasua vizuri mitihani yako au mfanyakazi ofisi au shughuli yoyoyte ile ambayo si ya kiofisi na unaona umefanya vizuri katika eneo lako husika!Fanya hivii,itazame kazi yako kisha sema maneno haya“hakika nilichofanya ni chema sana na chenye kupendeza,nahitaji pongezi” baada yakusema maneno haya haraka bila kupoteza muda nenda kajinunulie zawadi yoyote,ai lazima iwekuubwa hata ndogo inatosha,mfano saa,simu,eaphones au unaweza kwenda Beach,fanya jambo lolote la kukufurahisha.Kwaufanya hivi Utakuwa Umejipa thamani kubwa ambayo yawezekana Ungeisubiri Miaka mia kutoka kwa Mwanadamu Mwenzako.
Ni imani yangu Kuwa ulifautana na mimi tangu niliopaonza sehemu ya utangulizi wa makala hii ya MPISHI WAFURAHA YAKO nakuona viungo mbalimbali vinavyo hitajika ktk Upishi wa Furaha, Natumaini sasa utakuwa ni Mpishi bora wa FURAHA yako na mpishi wa FURAHA za wengine kama mimi “FURAHA YAKO MAISHA YAKO”                                      

Usisahau kuacha Maoni yako hapa chini

 

 

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.