Wema Sepetu Mwenyewe Atawapa Maelezo – Country Boy

Rapper Country Boy amepata kigugumizi kueleza ni kwanini mrembo Wema Sepetu ameweka link ya video yake mpya katika bio yake ya instagram.


Country Boy ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ya Turn Up aliyomshirikisha Mwana FA, ameiambia Times Fm kuwa Wema ana nafasi kubwa katika muziki wake ila hakutaka kuliongelea kiundani zaidi suala hilo.

“Wema ana play part kubwa lakini nadhani ni suala ambalo mimi siwezi kuliweka official kwa sababu sijaruhusiwa kuongea chochote, ila ambacho naweza kukiongelea link inapatia pia kwa Madam. Hillo swali nilikuwa na expect kuulizwa sana lakini uongozi umeniambia Wema mwenyewe atawapeni maelekezo, mtaelewa kwanini ameweka katika bio yake ile link,” amesema Country Boy.

Pia ameongelea mafanikio iliyopata tangu ngoma yake ya Turn Up ilipotoka mwaka huu na kueleza kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kuja kufanya kazi na Patoranking kutoka Nigeria.

“Ngoma yenyewe inakupa ile confidence ya kuongea na mtu yeyote kwa sababu production ni kubwa na imekaa kimataifa zaidi, ngoma ni kali nimepita melody ambazo zinatrend duniani.  Nimeweza kuwashawishi baadhi ya wasanii wakubwa ambao ninaweza kufanya nao kazi lakini kwa uhakika zaidi, mtu ambaye tumefikia hatua za mwisho ni Patoranking,” amesema Country Boy.

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.