Watu Sita Washikiliwa Na Jeshi La Polisi Kwa Kosa La Kuchoma Nyumba 3

Kamanda wa polisi mkoani Pwani, (ACP) Jonathan Shanna ,amewataja watu hao kuwa ni pamoja na Omary Athumani, Abdallah Shomari, Seif Shomari, Uzalimala Selasela,Salum Shomari na Jumanne Omary wote wakazi wa Vikumburu .

Aidha RPC Pwani amesema watu wote hao wanadaiwa kuchoma nyumba moto ya Bwana Joseph Simbayi, Rebeka Yona na Selina Simon .

Hata hivyo ,kamanda Shana ameeleza watuhumiwa hao pia waliingia kwenye mazizi na kukatakata mifugo ambayo walichukua nyama na vichwa ambapo utumbo waliuacha licha ya idadi ya mifugo hiyo kutofahamika.

Watuhumiwa wote hao wanashikiliwa na jeshi la polisi na pindi uchunguzi ukikamilika watafikishwa mahakamani

Chanzo : Eatv

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.