Usipitwe na kisa hiki mume na mke walioana miaka 69 wafariki pamoja………..

0

Wanandoa wawili katika jimbo la Illinois, waliokuwa wameoana kwa miaka 69, walifariki wakiwa wameachana kwa saa moja pekee, jamaa zao waliambia vyombo vya habari Marekani.

Isaac Vatkin, 91, alikuwa amemshika mkono mkewe Teresa, 89, alipofariki kutokana na ugonjwa wa Alzheimer Jumamosi, gazeti la Daily Herald.

Isaac alifariki dakika 40 baadaye. Jamaa zao walisema walifarijiwa kwamba wawili hao walikuwa pamoja hadi mwisho.

“Hungelipenda kuwaona wakituacha,” alisema mjukuu William Vatkin, “lakini hungetaka zaidi ya hilo.”

“Upendo wao kwa kila mmoja ulikuwa mkubwa sana, mmoja wao hangeweza kuishi bila mwenzake,” binti yao Clara Gesklin alisema wakati wa mazishi yao.

“Walipendana sana, hadi mwisho. Hadi sekunde ya mwisho,” alisema Rabbi Barry Schechter, aliyeongoza ibada ya wafu katika eneo la Arlington Heights, viungani mwa mji wa Chicago.

Wafanyakazi katika hospitali ya Highland Park wamesema waliwapata Bwana na Bi Vatkin wakiwa wanatatizika kupumua Jumamosi na wakaamua kuweka vitanda vyao vikiwa vimekaribiana.

Jamaa zao waliweka mikono yao pamoja. Wanandoa hao walikuwa na watoto watatu ambao waliwalea katika eneo la Skokie, Illinois.

Aidha, walikuwa na uhusiano wa karibu sana na wajukuu wao. Bw Vatkin alikuwa mwuzaji nyama naye Bi Vatkin mtu wa kupamba nyumba na kmtunzaji mikono na kucha.

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.