UPASUAJI WA KUBADILI JINSIA WA JENNER KUA MWANAMKE WAKAMILIKA

0

Kweli Ukiyastaajabu ya Mussa, utaona Firauni. Caitlyn Jenner ni mwanamke ambaye awali alifahamika kama Bruce Jenner, mshindi wa mbio za Olimpiki miaka ya 1970 na baba wa kambo wa familia maarufu duniani ya Kardashians, wakiwemo Kim, Khloe, Kylie na Kendall. Bruce kwa kutoridhika na jinsia yake, amechukua hatua ya kufanya upasuaji wa kubadilisha jinsia. Hatua ambayo ilianza takriban miaka miwili iliyopita.

Upasuaji huo umekamilika huku Bruce na sasa Caitlyn kwa kubadili jinsia yake ya kiume na kuweka ile ya kike pamoja na kuweka maziwa na ‘hormones’ za kike mwilini mwake

“Ninawaambia kwa sababu nimeamua kuwa mkweli” alieleza Caitlyn,”Mlikuwa mnataka kujua kama nitaweka jinsia hii ama la. Sasa nimeamua kuweka wazi. Hii ni mara yangu ya mwanzo na mwisho kuzungumzia mabadiliko ambayo tayari nimeyafanya.” Caitlyn alimalizia kwa kiusema, “nNisingependa kuyazungumzia tena.”

Kwa mujibu wa chanzo cha karibu na Caityln, mwana mama huyo kwa sasa anategemea kufanya photoshoot ambayo itamuonyesha katika uhalisia wa jinsi alivyo sasa.

Kutoka katika chanzo cha Familia ya Kardashian, akiwemo aliyekua Kris Jenner, mke wa Bruce kwa miaka 25 kabla ya kuamua kubadili jinsia yake, anatamani jambo hili, ambalo hawakutegemea yapite

kwa sababu sio jambo jema kwao.

Na Laila Sued

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.