THAMANI YA MUDA WA FARAGHA KTK KUIMARISHA MAHUSIANO.

0

Mahusiano ili yawe na nguvu na ya dumu,yana hitaji vitu vingi sana kama vile Mawasiliano(communication),Kuheshimiana(respect),Kutumia/kutengenga Muda wa faragha pamoja(spending time together) na nyinginezo nyingi.

Katika Makala hii tutaona Makosa yanayo fanyika katika Matumizi ya Muda wa faragha katikia Mahusiano.Hapa wapo wengi sana wanaona hata hakuna Maana ya kuweka muda kwaajili ya wapenzi wao kwani haileti matokea yoyote ktk kukuwa kwa mahisiano yao.Usilalamike rafiki yangu leo nataka tuone kwa pamoja jinsi gani unatumia huu Muda wa pamoja na Mpenzi wako.

Je ni Muda wa ZIADA kwako au ni Muda MAALUM kwaaajili ya Mpenzi wako.?

Natumaini Umejiuliza swali hili na Unamajibu yako.Ndugu yangu Mahusiano ni Muingiliano wa hisia na kitu chochote kinacho husisha hisia kinahitaji umakini mkubwa sana Katika kila jambo unalo fanya iki usije kuumiza hisia zako au za mwenzako.Unaweza ukadhani kwakutenga Muda wako WAZIADA(free time) kunaweza kuongeza nguvu katika Mahusiano yako!hapana!Unatakiwa kutumia Muda MAALUM(special time).Labda ni kuakikishie tu kuwa Mpenzi wako akifahamu Ulemuda unauwa nae ni Muda Maalum kabisa kwaajili yake itaongeza thamani yako kwake kwa kiasi kikubwa kuliko kuliko akijua Uko nae ni kwasababu ni Muda wako wa ziada,maana hii ni kusema kuwa kama ikitokea kuna ratiba yoyote labda ya kikazi ungeondoka na kwenda kufanya Mambo yako.Rafiki Kila mtu anapenda kuthaminiwa,lakini huwezi kuthaminika kama wewe huthamini wengine.Kama unataka mahusiano yako yawe na Nguvu kwa kutumia Kutenga Muda wa pamoja na mpenzi wako basi hakikisha unatenga Muda Maalum kwaajili yake,na sio kutumia Muda ambao wewe ni ziada na pande zote zikifanya hivi hakika thamani ya kila Mtu itaongezeka kwa mwenzake na Mwisho wa siku mtakuwa na mahusiano yenye nguvu sana.

Je Unafanya vitu vidogo vya kukumbuka au unafanya Mambo makubwa yasio na maana!

Swali linaweza kuwa halijaeleka kwako kwa mara moja lakini usijali utanjelewa tu kwa mfano huu,Zipo couple mbili moja imeamua kutoka na kwenda kwenye hotel kubwa ya nyota tano lakini walipo fika mwanamke ankula chakula wakati mwanaume anaangalia movie.Couple ya pili imeamua kutulia kwenye nyumba ya mmoja wao nakuandaa chakula cha pamoja,wakala chakula pamoja na kisha wakatulia kwenye couch moja na kuanza kuangalia movie kwa pamoja.Swali ni Je?ni ipi couple ambayo kati ya hizi imetumia vizuri Muda wa faragha kwa mustakabali wa kukuza uhusiano wao.

Naamini umesema ni couple ya kwanza kwasababu kwanza wao wameona hakuna sababu ya kuto kwenda mbali nakutumia pesa nyingi lakini mwisho wasiku matukio yalio fanyika huko si ya kukumbuka na wala hayajengi uhusiano mzuri baina yao,Lakini wao waliamua kutumia kidogo lakini matukio haswaa yaliofanya wawe pamoja ndio yalikuwa ya maana.Haita kuwa na maana kuwa pamoja na mpenzi wako muda wafaragha halafu baadala ya kufanya matukio ya kuwajenga kihisia unaanza kuelezea jinsi shughuli zako za kila ziku zinavyo kuchosha,kaka au dada yangu kila jambo linawakati wake wazungu wanasema SPEND A QUALITY TIME AND NOT A QUANTITY TIME Kutoka na Mpenzi wako sio mahali pakuanza kuonesha unauwezo kiasi gani bali ni mahali paku Muonesha Mwenzi wako anathamani kiasi gani katika Moyo wako.
Najua Yako mambo mengi ya kufanya,na hapa sizungumzii kujamiiana,Unaweza ukawa na Mpenzi wako hata kwa masaa Machache lakini akayakumbuka hayo kuliko hata ungekaa nae wiki moja lakini ufahamu na akilizako zisiwepo hapo,ndugu QUALITY TIME TOGETHER ina maana kila kitu kizuri chenye dhana ya kujenga mahusiano yenu kinatakiwa kifanywe kwa pamoja,kuangalia movie kwa pomoja au kupika chakula kwa pamoja inaweza kuonekana nijambo dogo lakini lina matokeo makubwa sana ktk mahusiano.

Hivyo basi unapoamua kuwa na Mpenzi wako hakikisha kwanza huo unakuwa Muda maalum kwaajili yake na si vinginevyo.Hakikisha matukio yote yanayofanyika hapa ni yale ambayo yatakuwa na dhana ya kujenga Mahusiano yenu.

Na KAKA EMMA

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.