UMUHIMU WA MITANDAO YA KIJAMII KWA WASANII

0

Umuhimu wa mitandao ya kijamii katika muziki duniani ni kitu ambacho hakifichiki,leo hii wakitokea wasanii wakubwa 10 kutoka pande zote za dunia basi asilimia 99% watakua na fanbase kubwa kwenye mitandao yao ya kijamii, mitandao ya kijamii mbali na kuwafanya wasanii wawe karibu na mashabiki zao lakini pia huwasaidia wasanii kujua nini mashabiki wanataka kwa kukosolewa ama kusifiwa.

 

Jicho la uswazi leo limeamua kuangazia swala hili la mitandao ya kijamii kwa kuangalia potential yake kwa wasanii

 

1 KUWAKUTANISHA WASANII NA MASHABIKI

ni mitandao ya kijamii inayowakutanisha kwa ukaribu wasanii na mashabiki na kuweza kuchat kwa lolote na kwa ukaribu kabisa,hapa wasanii huweza kukosolewa au kusifiwa.

 

2 KUJUA MAISHA HALISI YA MSANII

kwenye mitandao mingi unaruhusiwa kupost matukio mbali mbali,matukio ya picha na video kulingana na hitaji binafsi, kulingana na trend kubwa ya post zinazoonekana mitandaoni,mashabiki wanapata kujua maisha halisi ya msanii husika.

 

3 HUSAIDIA MCHAKATO MZIMA WA KUPIGA KURA

mitandao ya kijamii inawasaidia wasanii kwenye mchakato mzima wa upigaji kura kwenye tuzo mbali mbali nje na ndani ya nchi,inamfanya msanii aweze kujitangaza mara nyingi juu ya namna anavyoweza kupigiwa kura kwa kuweka link which gonna direct you straigt up

 

4 CONNECTION ZA HARAKA

mitandao ya kijamii imesaidia kukutanisha wasanii wengi kwa haraka tofauti na kipindi cha nyuma, kabla ya kuenea kwa mitandao ya kijamii ilikua ngumu kupata connections kwasababu ya ufinyu wa mawasiliano but this time arround ni rahisi sana inafanya wasanii wengi wakutane na kuweka aggrements za awali mitandaoni then mengine hufata baada ya hapo, tunaweza sema imerahisisha mawasiliano sana

 

5 MITANDAO YA KIJAMII INAONYESHA UKUBWA/UDOGO WA MSANII

Ingawa hii sio moja kwa moja but ni uhalisia na ukweli uliowazi kwamba mitandao ya kijamii husadifu ukubwa ama udogo wa msanii,ukubwa wa msanii huonekana wazi pale anapofwatwa na mashabiki wengi mtandaoni, tuchukulie Diamond Platnumz na Timbulo unaweza kuona moja kwa moja kuna utofauti wa wafuasi mitandaoni,utofauti huo unaonyesha wazi ukubwa na udogo wa hawa wasanii wawili.

 

 

Baada ya kuangazia faida za mitandao ya kijamii,kaa karibu na JICHO LA USWAZI badae upate kujua madhara ya hii mitandao kwa wasanii na kazi zao.

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.