FAHAMU NAMNA YA KUACHA KUJICHUA(PUNYETO)

0

Hebu niambie…umeshawahi kujichua? Mara ngapi? Bado unaendelea na mchezo huo? Vipi, umewahi kusikia watu wakizungumza kuhusu suala hilo? Amini usiamini, asilimia 90 ya wanaofanya mchezo huo,
hawapendi hata kidogo.
Kila wanapomaliza kujiridhisha huahidi kuacha lakini wanashindwa.

KUJICHUA NI NINI HASA?
Ni kitendo cha mtu kujichezea kimahaba huku akivuta hisia za mapenzi kwa mtu ambaye yupo mbali naye hadi anapomaliza haja zake. Namna ya ufanywaji inategemea zaidi na jinsi ya mazoea. Wapo wanaotumia vifaa bandia (artificial) na wengine vifaa halisi kama aina mbalimbali za matunda ambazo zinafanana na sehemu pacha! Wengine wanatumia njia wanazojuawenyewe, lakini wanaume wengi wanatumia sabuni lengo hapa ni moja tu, unatakiwa kufahamu kwamba namaanisha kujiridhisha.

INAWEZEKANAJE KUJIRIDHISHA?
Ni rahisi sana kumaliza tendo la huba kwa kujifanyisha mwenyewe. Silaha kubwa inayotumiwa na waathirika ni kuwavutia hisia watu wa jinsi pacha wakati tendo husika likiendelea kufanyika. Habari mbaya kwa watu wenye mchezo huu ni kwamba, kwanza wakishaanza, inakuwa vigumu sana kuacha. Inashindikana kwa sababu ni jambo la aibu. Si rahisi kupata ushauri kutoka kwa watu maana ni aibu pia kumweleza rafiki yako juu ya mchezo huo. Kutokana na hilo sasa, kinachotokea ni kwamba ‘waumini’ wa mchezo huu wanaendelea kuwa watumwa kwa maisha yao yote.Ni kweli hutaki kuwa mtumwa wa mchezo huu hatari?

UNATAKA KUACHA?
Hakuna dawa kubwa sana ya kuacha mchezo huu.kwasababu kila kitu kinaanzia kichwani(kweufahamu) basi ni lazima KUFUTA kabisa mawazo ya jambo hilo. AMUA kwa dhati ya moyo wako, tambua na
ogopa athari ambazo unaweza kuzipata, kisha ACHA KABISA
mchezo huo ili kulinda heshima yako na kujipa furaha ya maisha.
Ndugu zangu,zifuatazo ni dondoo chache ambazo pia zinaweza kukusaidia kutoka ktk tatizo hili.

Pitia dondoo zifuatazo;
1. Mtangulize MUNGU ktk hili,ndugu yangu ukubali au ukatae kutoka ktk tatizo la kujichua nilazime ujitoe kwa hali na mali na kujitoa huko nilazima umahirikishe Mungu akutie Nguvu,akuwezeshe kushinda hiyo roho chafu ya kujiridhisha Mwenyewe.

2.Acha kuangalia video za Ngono au aina yoyote picha zinazo shawishi mambo ya kingono.Nikuhakikishie tu rafiki yangu haswa wanaume hisia zako zinakuwa rahisi kubadilishwa na vitu vinavyo onekana kama picha uchi.

3.Kaa mbali na simulizi zinazohamasisha mapenzi,nakukumbusha pia usipende kukaa peke yako lakini epuka makundi yanayo penda mazungumzo ya kimahaba.

4.Acha mazoea ya kujishika sehemu zako za siri bila sababu ya msingi.

5.Fanya mazoezi ya viungo angalau robo saa tu kwa siku.Uchoshe mwili.

6. Unaweza pia ukabadili namna yako ya ulalaji.Hapa na zungumza na wale wanaopenda kulala chali,anza kulala kifudifudi ili iwevigumu kwa wewe kupapasa sehem zako za siri.

Na KAKA EMMA

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.