Ugomvi Wa Meek Mill Na Safaree Haumsumbui Nicki Minaj – Rafiki Wa karibu (Video)

Baada ya kuzichapa kati ya Meek Mill na Safaree siku ya Jumamosi kwenye sherehe ya pre-BET party ya Dj Khaled iliyofanyika Penthouse, West Hollywood, mrembo Nick Minaj amefunguka kuwa hajaumizwa na tukio hilo liliofanywa na ma-ex wake hao.

Kwa mujibu wa mtu wa karibu na mrembo huyo ameuambia mtandao wa TMZ, Nicki hana mawazo ya kujali kilichotokea kwa vidume wake hao na kwa sasa anachoangalia ni kampani yake mpya aliyoipata kutoka ka rapper Nas.

Mwezi Mei mwaka huu, picha zilizambaa katika mitandao zikimuonesha Nick Minaj na rapper Nas wakiwa katika mkao wa kimahaba, hata hivyo mrembo huyo kutoka Young Money alidai ni washikaji tu.

Na Laila Sued

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.