Uchapa kazi Wa RC Anna Mghwira Wamgusa Waziri Mkuu

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mama Anna Mghwira kwa kudhibiti usafirishaji mahindi nje ya nchi ambapo yalikamatwa Malori zaidi ya 103 yakisafirisha mahindi nchi jirani.

Waziri Majaliwa ametoa pongezi hizo jana katika kipindi cha maswali kwa Waziri mkuu maarufu kama maswali ya Papo kwa Papo.

“Wote ni mashahidi jana tumepata taarifa Malori zidi ya 103 kwa siku 4 tu, kutoka siku ya Eid mpaka leo hii Malori 103 je kwa mwezi mzima tutakuwa na Mahindi hapa ndani? Tunazo taarifa kupitia kamati za ulinzi na usalama wengi wanaofanya biashara ya mahindi hujakuchukua Mahindi Simanjiro,Kongwa,” alisema Majaliwa.

“Naomba nichukue nafasi hii kumpongeza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mama Anna Mghwira kuendelea kusimamia yeye na kamati yake ya ulinzi na usalama tumeona Malori yale, agizo limebaki palepale na yele mahindi tukijiridhisha kuwa yametoka ndani ya nchi yatarudishwa kwenye hifadhi ya Taifa na Malori yanayofanya biashara hiyo yatabaki kituo cha Polisi,” alisisitiza Waziri Majaliwa.

Na Emmy Mwaipopo

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.