TRUMP Amtumia Rais Magufuli Salamu za Pongezi ya Muungano wa Tanzania..!!!

0
Rais Donald Trump wa Marekani ametuma salamu za pongezi Tanzania kwa kuadhimisha mwaka wa 53 wa Muungano.
Katika salamu zilizotolewa jana jioni na kuwekwa katika tovuti ya Wizara ya Mambo ya Nje, Trump ameeleza uhusiano baina ya Tanzania na Marekani na matumaini yake ya kuuendeleza.
“Kwa niaba ya Rais Trump na wananchi wa Marekani, nawapongeza wananchi wa Tanzania wakati mnaposherehekea mwaka wa 53 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” anasema Rex W. Tillerson, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani.
“Tanzania na Marekani zina uhusiano mkubwa, unaoonyeshwa na juhudi za pamoja kufikia malengo yetu na ushirikiano wa karibu katika programu na jitihada mbalimbali, kuanzia katika afya na elimu, kuendeleza ukuaji uchumi na uongozi wa kidemokrasia na kukuza usalama wa kanda. Katika mwaka unaokuja, tunategemea kufanikisha malengo yetu ya pamoja kadri tunavyoendeleza juhudi zetu.
“Wakati Watanzania wakisherehekea Siku ya Muungano, naungana nao katika matumaini ya kuwa na amani, afya, na ufanisi.”
Hizi ni salamu za kwanza kwa Trump na Serikali yake kwa Tanzania tangu kiongozi huyo kutoka chama cha Republican asimikwe kuwa Rais wa taifa hilo kubwa duniani Januari 20 baada ya kushinda katika uchaguzi uliofanyika mwaka jana.
Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.