Tenesi: Fedeer Amkaribia Andy Murray Viwango Vya Ubora Duniani

Mshindi wa mataji nane ya michuano ya wazi ya Wimbedon, Roger Federer amepanda kwenye viwango vya ubora wa mchezo huo duniani kutoka nafasi ya tano hadi nafasi ya tatu.

Kwenye viwango hivyo Muingereza, Andy Murray ameendelea kushika nafasi ya kwanza huku akifuatiwa na Rafael Nadali katika nafasi ya pili, Novak Djokovic akiwa nafasi ya nne na Stan Wawrinka akishika nafasi ya tano.

Hata hivyo, Marin Cilic ambaye aliingia fainali ya michuano ya Wimbledon na kufungwa na Roger Federer amepanda nafasi mbili juu kutoka nafasi ya nane hadi ya sita.

Kwa upande wa wanawake Karolina Pliskova ndie kinara akifuatiwa na Simona Halep nafasi ya pili huku Mjerumani, Angelique Kerber akishika nafasi ya tatu, Johanna Konta nafasi ya nne na Garbine Muguruza anakamilisha tano bora .

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.