TAFITI: Kufanya Mapenzi Kunaongeza Umri Wa kuishi

Kama wewe ni moja ya watu ambao hufanya mapenzi kwa msimu basi utakuwa upo kwenye hatari ya kupunguza umri wa kuishi duniani hii ni kwa mujibu wa tafiti.

Watafiti kutoka chuo cha Coventry University cha nchini Uingereza wamebaini kuwa kufanya mapenzi mara kwa mara kwa watu wenye umri kuanzia miaka 28 kwenda juu huimarisha afya zao na kuongeza nguvu ya ubongo kufanya kazi kikamilifu kuliko wale ambao wanafanya kwa msimu.

Watafiti hao walibaini kuwa watu ambao wanafanya mapenzi mara kwa mara hupunguza msongo wa mawazo hivyo huimarisha afya ya moyo na kupunguza uwezekano wa kupatwa na magonjwa ya moyo kama Shinikizo la damu (High Blood Pressure), Koronari za moyo (Coronary Heart Diseases), Mshituko wa moyo (Heart Attack), Peripheral Vascular Disease magonjwa ambayo huwakumba watu wenye umri mkubwa.

Watafiti hao mbali ya kuorodhesha magonjwa ambayo utayaepuka kutokana endambo utafanya mapenzi mara kwa mara wamesema walichukua idadi ya watu 5000 kutoka nchi 10 tofauti tofauti wenye umri kuanzia miaka 50 hadi 80 ambapo asilimia 78% kati yao walikiri kuwa hufanya mapenzi kwa wiki mara 5 hadi 6 licha ya kuwa na umri mkubwa.

Asilimia 10% walisema kipindi wakiwa vijana walikuwa wanafanya mapenzi mara 2 kwa siku kabla ya kufikia umri wa miaka 40.

Asilimia 12% walisema hao hufanya mapenzi kawaida kwa wiki mara 1 ingawaje walisema kipindi walivyokuwa vijana walikuwa wanafanya mapenzi mpaka siku mbili tu kwa wiki.

Hata hivyo watafiti hao wamesema asilimia kubwa ya watu ambao hawafanyi mapenzi mara kwa mara wana asilimia kubwa kupata ugonjwa wa Kansa ya tezi dume (Prostate Cancer) wakieleza kuwa Tezi dume huwa zinakua kadri ya umri unavyozidi kuongezeka na huanzia miaka 25 kwahiyo kama mwanaume hatajihusisha sana na mapenzi tezi dume zitazalisha wingi wa mbegu na baadae kujaa na kupelekea kuzuia mkojo kutoka vizuri na dalili za ugonjwa huanza kujionesha hata kabla ya kufikisha miaka 50.

Watafiti hao wamesema mapenzi hayo ni lazima yawe salama kwani kuna uwezekano wa kupata magonjwa mengine makubwa endapo wahusika hawatazingatia afya ya miili yao kabla ya kukutana kimwili.

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.