TAFITI: Bodaboda Vinara Wa Unyanyasaji Wa Kimapenzi Kwa Wasichana

Kwa sasa jinsi hali ya uchumi ilivyo mtu akihitaji usafiri wa haraka hususani nchini Tanzania basi wazo lake la kwanza ni Bodaboda kwani ni usafiri ambao una gharama ndogo na ni wa haraka pengine kuliko Taxi, swali je, usafiri huu ni rafiki kwa wasichana? Utafiti unaonesha kuwa usafiri huo sio rafiki kabisa kwa Wasichana kwani Madereva huwanyanyasa kimapenzi na kuwafanyia ukatili wasichana ambao wanaokataa kushirikiana nao kimapenzi.

Tokeo la picha la bodaboda

Bodaboda

Kwa mujibu wa matokeo ya Utafiti uliofanywa na shirika lisilo la kiserikali la Maadili Center na kutolewa jana na Mwenyekiti wa shirika hilo, Florentine Senya, watoto wengi wa kike walitaja kero kubwa kuwa ni waendesha pikipiki hao (bodaboda) kuwanyanyasa hadi kufikia hatua ya kutishia kuwagonga kwa pikipiki zao wasichana hao wanapokataa kujihusisha nao kimapenzi.

Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu utafiti wa malezi na maadili ya watoto wa kike uliofanywa na shirika hilo, Senya amesema utafiti huo unaoendelea hadi sasa ulifanywa katika shule za sekondari na msingi kwa mikoa mitatu ya Dar es Salaam, Arusha na Kilimanjaro.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo, utafiti huo pia umebaini kuwa asilimia 78 ya familia nyingi zina matatizo ikiwemo wazazi kutelekeza familia zao na kuwaacha wengi kujihudumia wenyewe jambo linalochangia kuwapo ongezeko la watoto wasio na maadili.

Senya ameongeza kwa kusema kuwa utafiti  umebaini watoto wa kike 10 kati ya 50 sawa na asilimia 20, wamepitia vitendo mbalimbali vya ukatili ikiwemo kupigwa na wazazi, kuchomwa moto wanapokosea, na hata kutishiwa maisha wanapokataa kujihusisha kimapenzi na watu waliowazidi umri.

Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji wa Maadili Center, Bi. Rosaline Castillo alitaka jamii ikubali ukweli kuwa wazazi wengi wametelekeza watoto katika malezi.

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.