SOULJA APATA MAJANGA WAKATI AKIWA ANAJIANDAA NA PAMBANO LAKE NA CHRIS BROWN

0

 

 

Wakati akijiandaa na pambano lake la ngumi dhidi ya Chris Brown, majanga yameanza kumkuta rapper Soulja Boy.

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, Jumanne hii nyumba ya rapper huyo iliyopo Hollywood Hills ilivamiwa na mwizi aliyefanikiwa kuondoka na fedha kiasi cha $10,000 pamoja na vitu vyenye thamani ya $12,000.

Hata hivyo imedaiwa kuwa kamera zilizofungwa katika eneo hilo zimefanikiwa kupata picha ya mwizi huyo ambapo polisi wanaendelea kumfuatilia. Japo kumekuwa na mvutano juu ya pambano lake na Chris Brown lakini hakuna ushahidi wowote unaonyesha kuwa wizi huo umefanywa na watu wa upande wa Chris kama kumchanganya Soulja Boy.

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.