“Sitazami Mtu Ananifanyia Nini Kitandani” – Nisha

Baada ya watu kumuandama Nisha kuwa mpenzi wake ni serengeti boy, ameibuka na kusema hakuna kitu kama hicho na si kweli masuala ya kitandani zaidi ndio yanawafanya baadhi ya wastaa wa kike kupenda kutoka kimapenzi na vijana wadogo (serengeti boy).

Muigizaji huyo wa Filamu Bongo amesema kuna vitu vingi vya kuangalia kwa mtu kabla ya kuingia naye katika mahusiano na mambo ya kitandani yanakuja mwishoni kabisa.

“Sitazami mtu ananifanyia nini kitandani, before hatujafika huko, tumekutana, tumeonana, tumefahamiana, tumekubalina halafu yanafuata hayo mengine. Mpaka nimefikana nae pale hakunionyesha yeye ni mtundu sana,” Nisha ameiambia FNL ya EATV na kuongeza.

“Bahati nzuri au mbaya mapenzi hayajaribiwi unaweza kuwa fundi mkubwa lakini ukakosa nidhamu, wanawake wa siku hizi hatuangalii hivyo na mimi ni mmoja wapo,” amesisitiza.

Pia Nisha amewajibu wale wanaodai kuwa mpenzi wake sasa ni serengeti boy au kiben ten.

“Kitanzania watu wengi tumezoea kukariri matukio, wamezoea kuona watu wakidate watu wamewazidi umri lakini mkija mkadate mpo sawa, basi wataita serengenti boy, he is not serengeti boy, ni zaidi ya ngorongoro,” amesema Nisha.

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.