SERIKALI IMUUNGE MKONO ASKOFU DR. GWAJIMA KATIKA MPANGO WA KUNUNUA TRENI YA MWENDO KASI..!!!

0

Baba Askofu Dr. Gwajima, ameanza mchakato wa kunua Treni ya mwendo kasi ambayo itakua inatoka Dar hadi Morogoro. Katika usajili bado anawekewa Zengwe, ila nia yake ni nzuri kabisa.
Katika Tanzania ya Viwanda, hatuwezi kufanikiwa Tanzania ya viwanda kama hatuna Usafiri wa Uhakika wa kutoka sehemu moja hadi nyingine.
Tayari kashafanikisha Mpango wa kujenga chuo cha Urubani, anasubiri ruksa ya Rais Magufuli. Dr Gwajima alishampeleka Mkufunzi wa mambo ya ndege kusomea kufundisha mambo ya ndege. Kwa Tanzania watu wengi wanapenda Urubani lakini garama za masomo ni kubwa. Hivyo kampeleka Kaka John kusomea Ualimu wa ndege. Nadhani wote mnamjua John wa Ufufuo na uzima. Ni kijana mwenye akili sana.
Hadi sasa Dr Gwajima kushirikiana na Msukuma(Mbunge) wameshaanza mchakato wa kumuona Rais ili awape sehemu ya kujenga chuo cha Urubani.
Vilevile ameshaagiza Chopa tatu kwaajili ya wanafunzi.
Wito wangu
Naomba Serikali isilete siasa katika hili Swala kwani lina manufaa kwa Watanzania. Tutawanyanyasa wawekezaji lakini Kenya ikiwachukua tunaanza kulalamika.
Askofu Dr Gwajima kwa wasiomjua, ni Askofu wa Makanisa ya Ufufuo na Uzima ambayo ni Zaidi ya Makanisa mia nne(400) Dunia. Vilevile ana makampuni mengi kama makanisa mengine yalivyo na mabank mfano Mkombozi, Efatha Bank nk.
Dr Gwajima ni Mwalimu ambaye Hulipwa zaidi ya dola 1,000/= kwa saa. Anafundisha Mambo ya Kiroho Duniani na huwa anaalikwa kufundisha hata kwa miezi mitatu.
Kwa sasa anamiliki ndege ambayo humuwezesha kuhudumia Ibada katika Makanisa Matatu Tofauti mikoa tofauti kwa siku.
Watanzania tuache wivu na kijicho cha roho mbaya, bali tuwaunge mkono Watanzania wenzetu ambao Mungu Kawainua.
Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.