SEHEMUO1; MPANZI WA PENZI (Cheka na Kaka Emma)

0

 

                  SEHEMU 01
Naitwa Prince,sijui ni Kwanini nimeitwa jina hilo,Baba yangu si Mfalme Wala hajawahi kuwa hata Balozi wanyumba kumi au labda ni kwasababu baba ana watoto wengi wakike na kuwa na mtoto wakiume Mmoja,Unauliza ni nani huyo mtoto wakiume? Ndiyo ni mimi Prince Masumbuko. Mpaka Muda huu Nina Umri wa miaka 28 Sina mke,sina mchumba wala mtoto wakusingiziwa,yani Kuna Muda na waza Peke yangu “Au ubavu wangu wakushoto bado ninao haukutolewaga? au wameupikia supu.? Au wale wanao Oa mke zaidi ya mmoja wameoa na mke wangu? au Mke wangu bado hajazaliwa? je akizaliwa na umri huu atakuwa mke au mjukuu.?” Kwakweli nakosa majibu kabisa na muda huu nimekuwa Mwenyekiti wa chama cha wanaume ambao mpaka sasa hawajaona ubavu wao wa kushoto.Unafikiri Nilikuwa sijui kutongoza.?labda ndiyo sababu niko peke yangu mpaka sasa? “Hahahaha Kama unamawazo hayo basi unakosea sana”. Kwataarifa yako nimeachika Siku kama Tano zilizo pita na Mchumba ambae nahisi yeye ndio peke yake alinihurumia baada ya Kupanda Mbegu(kutongoza) kwa wasichana si chini ya elfu moja na mia tano hivi!NAJUA UNABISHA.! Lakini mimi ni Fundi mzuri sana wa kupanda mbegu(kutongoza) ila Kuota ndiyo  Ngumu.Nina uwezo kupanda mbegu kwa wasichana Sita kwa siku  na Kuwapandia mbegu Marafiki zangu kwa wasichana wao hata wa nne,lakini Mashamba yangu yote Sita hayaoti Mbegu Kabisaa na ya marafiki zangu yanaota hadi wanashindwa kuvuna,hapa ndipo nagundua kwanini “Kapteni Komba Aliwaimbia Viongozi wenzake Nyimbo za Msiba Pindi walipo kufa lakini Yeye alipofariki hajawahi kutungiwa hata Beti moja”.

      Nikikwambia sikuwa domo zege nikweli,yani nilikuwa vizuri sana. Nilivyokuwa kidato cha Nne katika Shule Moja Huko Shinyanga nakumbuka nilitongoza wasichana wote kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita na nikala chaga(kukataliwa) kwa wote,ni kahisi labda walikuwa wananipima kama ninamaanisha nilichokuwa na waambia hivyo nikawatongoza tena wote kwa Mara ya pili na Muda huu nikapigasound kidato cha kwanza hadi chasita lakini KIBUTI kikawa palepale,nikaona sio neno acha nijiongeze kwa baadhi ya walimu wale wanao anza kazi nao wakanichezeshea chaga. Sikukata tamaa nikaona nibadili upepo kidogo “Daah Sijui nikatongoze Wapishi jikoni?” niliawazaa baada ya kuona sipati mahali penye nafuu,huwezi kuamini hata Wapishi nao hawakuwa na hata chembe ya huruma na kiumbe mimi “Sijui walikuwa wana ambizana wanikatae.” Nimepokea majibu Mengi sana lakini yote yalikuwa yanamaanisha JARIBU PENGINE. Mara huyu anakwambia “Ntakufikiria” utafikiri namuomba mkopo. Majibu mengine mpaka unafikiri huyo msichana yeye ni jamii ya mimea kama mahindi kumbe nae ni mnyama kama mimi tu,eti anakujibu “Wewe sio type yangu”. Wengine utaskia “Acha utani bwana” “utaniweza” kama vile unataka kumbeba. Muda mwingine nahisi kama kupanda mbegu ni kama kuwahi namba shuleni eti “Umechelewa”. Kuna wale ambao hawaeleweki wako kundi gani utawaskia wakiniambia “Siko tayari kwa sasa” . Majibu ya Amina Ntobolwa ndio yalinifanya nihisi kama kutongoza nikuomba ajira,maana yeye alisema eti “kama unanipenda nenda  kwa wazazi wangu wakupe cheti Cha ndoa”.
Labda nikuhakikishie tu kuwa ile methali inayosema “MVUMILIVU HULA MBIVU” niliielewa kuliko methali zote za wahenga kwamaana pamaja na majibu yote hayo sikuwahi kuumia Moyo wala kukata tamaa. Sihata maneno ya Mungu yanasema “Kila Mwanaume kaumbiwa Msaidizi kutoka kwenye ubavu wa kushoto” Hivyo nikawa naamini Ubavu wangu Upo sehemu unaniangalia ninavo poteza muda kuutafuta. Basi baada ya elimu yangu sekondari,muda na miaka kadhaa ikapita,huku nikiendelea na kujaribu bahati yangu ya kupanda Mbegu bila mafanikio yoyote. Nilijiunga na elimu ya juu mkoani Dar es salaam,ambako nilichaguliwa kusoma Kozi ya Uwalimu wa Historia na Kiswahili,hapo ndipo nili amini kweli “Mungu si Athuman na mungu havai dera” Maana nakumbuka siku yangu ya kwanza mimi kwenda pale chuo nilikuta wanafunzi wenzangu wamekwisha anza masomo siku nyingi na kwa siku hiyo wenzangu nilio kuwa nasoma nao kozi moja walikuwa wako kwenye kipindi na mimi sifahamu vizuri watakuwa wapo chumba gani haswa hivyo nikapata wazo la kuuliza,wahenga wanasema “kuuliza si ujinga” ila hawajasema unamuuliza nani? Vipi ukimuuliza mtu mjinga?Vipi ukiwa peke yako? Nikaangalia kushoto na kulia,mbele na nyuma nikiwa natafuta mtu sahihi wakumuuliza,kwakweli nikaona wote hawaeleweki wasije nielekeza kwenye kituo cha polisi bure,na kimsingi nilikuwa nataka hata huyo nitakaemuuliza lazima awe binti mzuri ikiwezekana nipande mbegu na hapo,yani ni mwendo wa kuuwa ndee wawili kwa jiwe moja. Nikafika eneo lenye kamgahawa nikaenda kupata chai yangu na mihogo “Basi siku ya leo nitaitumia kwaajili ya kujua maeneo ya chuo vizuri” yalikuwa ni mawazo yangu huku nikiwa nakunywa zangu chai. Baada ya Dakika kama tano hivi macho yangu yalishuhudia binti mzuri mfano wa malaika kamasio jini akiwa anakuja uelekeo wa pale kwenye mgahawa nilipo kuwepo. Mtoto alikuwa kavaa gauni lake refu lillilo mkaa vizuri kwenye mwili,gauni lilikuwa jeupe limenakshiwa na mauwa Mengi kiasi kwamba nyuki wanaweeza mfuata.Binti ni Mweupe eti,Ameenda hewani kama Mlingoti wa bendera ya taifa,jicho lake akikuangalia Unaweza uza shamba la urithi pesa yote umpe yeye, na zile neema za Allah pia anazo,Anavotembea kwa maringo sasa,kama ameongezewa mshahara,akanimaliza na tabasamu lake utafikiri tunafahamina. Nilikuwa Siamini ninacho kiona kwakweli,maswali mengi yakawa yanarindima kwenye kichwa changu “Hivi naota? au nimwambie mama Muuza animwagie maji usoni,usikute naota,sasa na huu ufupi wangu huyu mtoto si anaweza hisi mie ni kama mdogo wake,mmmh.! lakini si kwa tabasamu lile,huyu mtoto atakuwa kanielwa bwana” Nilizama kwenye dwimbi la mawazo bila majibu,nilishtuliwa na sauti taamu ya yule binti “Kaka Mambo?” Yani kwajinsi nilivokuwa mbali kwa Mawazo nilikurupuka na kujikuta naropoka “Mbuzi kafia kwa Muuza Supu” hilo lisitoshe nikaangusha na kile kikombe kilicho kuwa na chai ikamwagikia yule dada. Yani nilijua tu nimekwisha haribu tayari maana nimeropaka maneno yakipuuzi bado nimechafua gauni la dada wa watu na chai “DUUH KWA HALI HII NAONA PEPO LA KUKATALIWA LINAENDELEA HADI CHUO,HATA KABLA SIJAPANDA MBEGU” niliwaza mweyewe,huku nikitafakari kitu chakufanya,maana mtoto ni Mzuri kweli na siwezi Muacha aende bila Kupanda Mbegu.
ITAENDELEA………
***********Na KAKA EMMA***********

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.