SEHEMU 01;CHEKA NA KAKA EMMA(SCHOOL COMMEDY)

0

Ni 1:00 asubuhi siku ya jumatatu kama ilivyo kawaida ya Mama Emma, Mama mwenye umbo kubwa lakumfanya akae siti ya watu wawili kwenye gari,na leo kama siku zote akiwa anajiburudisha na nyimbo za taarabu maarufu kama Mipasho, huku akiwa anaendelea kufagia uwanja wa nyumba yake karibu na chumba cha nje kilicho pakana na Jiko lake gafla alisikia sauti “Moja mara mbili ni mbili,mbili mara mbili nne,aaaah mara aaaah aaaah”alishindwa kuelewa alikuwa ni Mlevi wa gongo au ni nani,lakini alikuwa hataki kuamini kwasabubu sauti alio sikia aliifahamu vizuri sana na kikubwa ilikuwa ikitoka katika chumba cha mwanae wa mwisho aliejulikana kama Emma,Mwanafunzi darasa la saba shule ya msingi Mwizange na kwa muda ule alitakiwa awe Shuleni,lakini amelala,MamaEmma alijikuta anapiga ukunga Uwiiii!!mwenzenu nina hasara ya mtoto,yaani saa moja hii bado hili toto halijaamka tena linaota na ndoto,kwa jazba na hasira mama Emma alitupa fagio alokuwa ameshika na kwenda jikoni kwakwe kuchukua mwiko,nakuuelekea mlango wachumba cha mwanae, mama emma alitumia ule mwiko alio shika kuugongea mlango “ ngo ngo ngo we prince hebufungua mlango,inamaana leo huendi shule,ngo ngo ngo ” Emma aliisikia vizuri zile kelele za mama yake pale mlangoni lakini alikuwa akiwaza sana adhabu ambazo angeweza kupata huko shule kwa muda alio amka, aliwaza “mmh kiukweli leo shule siendi hata kwa dawa,yaani sijashika table yoyote,bado nimechelewa namba asubuhi halafu hii nizamu ya mwalimu Kiwia,yule lazima aje atutie mboko,mama Emma baada ya kuona ule ukimya aliendelea kuugonga ule malango We mtoto(kimya),si wanifahamu vizuri niikingia humo ndani utajua kilicho mtoa kanga manyoya,Emma akiwa bado pale kitandani akaona mama yake alikuwa na dalili za kuung’oa ule malango ikabidi aamke nakuulekea ule mlango na kumfungulia huku akianza kumuigizia mama yake kwa kujishikilia tumbo na sauti ya kigonjwa kwa kweli mama leo siwezi kwenda shule tumbo lina niuma sana mama Emma baada ya kuingia pale ndani na kumkuta Emma ambaye muda sio mrefu alikuwa akikoroma na kuota,mara hii amekuwa katika hali ya kuumwa namna ile ilibidi ashangae sana Tobaah mungu wangu!! haya ndo nini kujikunja hapo kitandani kama beberu anae subiria kumezwa na chatu,nahiyo sura kama unakamuliwa ndimu ya jicho,huna haya wewe mtoto si ulikuwa unamwaga mate kwa kukoroma sasa hivi,hili tumbo limekuanza saa ngapi?Emma alikuwa kesha zoea kelele za mama yake wala hata hazikumpa shida, kwani alikuwa amejipanga vilivo na alidhamiria kabisa leo hawezi kwenda shule,alianza kugalagala chini huku akitoa povu mdomoni na kutoa sauti za kigonjwa “tumbo mama linaniuma, ndiyo maana nimechelewa kwenda shule” Mamaemma alivoona mwanae kaanza kutoa povu mdomoni alishtuka Povuu!! haya ya leo ni makubwa kwakweli umekunywa sumu we mtoto,utaniuwa kwa pressure jamani! Mamaemma aliongea kwa huzuni sana,lakini Emma alianza kupata furaha baada gundua kuwa mama yake alianza kuingiwa na uwoga akaendelea kusisitiza swala lake lakutotaka kwenda shule “Mimi sijanywa sumu, sinilikwambia naumwa wewe ukawa huamini,leo siwezi kabisa hata kwenda shule mama, lakini kitu alicho sahau Emma ni kwamba mama yake huyo alisha walea kaka zake wawili wakubwa na wote walisha Umwa na tumbo mara nyingi na hawajawahi hata siku mmoja wao kutokwa na povu na hivyo kulimfanya mamaemma machale ya mcheze na kuhisi kama kuna kamchezo Emma anataka kukaleta pale Mmmmh..tumbo gani hilo linafanya utoke povu?Emma akawa kimya kitu kilicho mfanya mama yake aamini kama kuna namna pale, akaanza kupepesa macho huku na kule kuzunguka chumba cha Emma bila kuona kitu chochote kinacho husiana na kutoka kwa povu, lakini alisikia harufu! mbona naskia harufu ya sabuni humu ndani,nakuuliza we mtoto hii harufu ya sabuni inatokea wapi,tena ni sabuni yangu ya unga. Emma baada ya kuona mama ake anataka kumstukia sasa ilibidi asimame na kuacha maigizo yake,alijua njia hiyo imekwisha shindikana.Kikituambacho kilizidi kumhakikishia mama emma kuwa mwanae huyo alikuwa haumwi na kitu chochote HEEEEEEH!!,kweli hi ni hasara ya mtoto kwahiyo umeona ule sabuni yangu ya unga utoe povu unidanganye kuwa unaumwaa,pole weee,hapa kwangu utanyooka mimi sindanganyiki kizembe,huo uhuni unaofanya wewe leo mimi nilishapitia zamani!!
Emma aliona hana ujanja tena na anamfahamu vizuri mama yake  kwa kuongoea sana,kila mtu pale mtaani angefahamu  na kumuona mjinga wa kula sabuni,ilibidi aendelee kujitetea Mama bwana sisi mwalimu wa sayansi alituambia tumbo likiwa lina uma ujue umekula kitu kichafu kwahiyo nikaona ninywe sabuni nisafishe tumbo..lakini mama Emma hakuwa mjinga wa kukubali uongo wa namna ile alijua tu Emma leo hataki kwenda shule,hivyo alianza kumburuza kutoka pale chumbani,huju akiendelea kumshambulia kwa maneno ya kejeli we bogazi kweli,hiyo ni sayansi ya chini mwembe,hebu toka nje ujiandae uende shule.
Emma:Mama mi naenda kuchapwa huko shule,sijawahi namba sijashika table.
MamaEmma:Heeeh!!darasa la saba huoni hata aibu kusema hujui table sasa unafauluje hizo hesabu.
Emma;kusoma sio kufaulu mama,na kujua hesabu sio kama nywele kila mtu anazo,vingine vipaji mama.
MamaEmma;hizo ni shida zako we tangu ijumaa hujajiandaa unategemea nini?
Emma;sawa hizo nishida zangu..lakini hela ya mlinzi na hela ya chakula cha mchana ni shida zako.
MAMA emma;hayo mambo ya hela za walinzi ni shida za baba yako sio mimi..
Emma;basi ili isiwe shida ya mtu kati yangu mimi wewe na baba mi naona nibora nisiende shule kabisaa, kila siku mi nazibuliwa fimbo kama punda wa kijiji kisa sina hela ya milinzi,wenzangu wanakula chakula mimi na waangalia tu,alafu mama wewe si unasemaga kila siku watu wakiwa wanakula ukiwaangalia ni vibaya.
MAMAemma;wewe mtoto usinitibue kabisa hapa shule utaenda hela ya mlinzi mwambie huyo mlevi(Baba Emma) na kama nichakula cha mchana utarudisha hizo ngoko zako uje ule nyumbani.
Ni saa 1;30 Emma amemaliza tifu na mama yake,kajiandaa na kuanza safari ya kuelekea shule japo ni kwa shingo upande ,maana alikuwa na mawazo mengi yakitakacho enda kumtokea huko shule.Lakini alipo kuwa njiani uso wake ulianza kupata furaha baada ya kukutana na mchelewaji wasiku zote aliye julikana kama Benard.Huyu Ben alikuwa Muoga sana lakini kila siku huenda shule saa mbili kama vile yeye ndo mwl mkuu Daah!afadhali nimekuona mchelewaji mwenzangu ,si unajua kifo cha wengi sherehe, Emma aliongea kwa furaha sana.
Ben naye alionyesha tabasamu lakini la kwake halikuwa la kupata mchelewaji mwenzake Hahahahahah…we kila siku unachelewaa,tatizo unapenda kulala sana Emma alishangaa kidogo baada ya kumsikia Ben akiwa anamsema vibaya kuwa yeye anapenda kulala sana ilihali Ben ndiyo fundi wa kuchelewa Kwahiyo we ndo umewahi saambili kasoro hii…we nikama mimi tu,tena sidhani kama table umeishika vizuri, tujiandae na kichapo tu hapa.Mimi mwenzio naweka daftari kwenye makalio bakora zinakuwa hata haziingii, Ben alizidi tu kufurahi maana anajua leo hakuwa kwenye kundi moja na Emma,hivyo hakuwa na sababu ya kuogopa,akazidi kumkatisha tamaa kabisa Emma Mimi sio mwenzako bwana kwa taarifa yako niliwahi tena namba yangu sita lakini nikarudi kuendelea kulala,swala la table nikawaida pale darasani wengi tutachezea bakora.Emma baada ya kuona hata huyu mchelewaji mkubwa leo amewahi, alizidi kuvurugika zaidi akajihisi niyeye peke yake aliye chelewa leo Mmmh!leo!we unafikiri Mwalimu Kiwia ukimwambia uliwahi namba ukarudi nyumbani atakuelewa kweli? Emma alihoji,lakini Ben hakuonyesha kuwa msaada wowote kwa Emma zaidi ya kuendelea kumtia wasiwasi Unaniuliza mimi tena,we twende ukale kichapo Emma alikaa kimya kwa muda,lakini walipoanza kufika maeneo ya Shule wasiwasi na kawaogo kambaali vilianza kumuingia, akajaribu kuuliza kuhusu pesa ya mlinzi vipi unapesa ya mlinzi..?? Kabla ya Ben hajajibu swali la Emma wali sikia sauti ya ukali ya mwl kiwia wewe Emma na huyo popo mwenzako kuja hapa haraka, mnakuja shule muda mnaotaka!! baada ya kuangalia mbele nakumuona mwl Kiwia amebeba Bakora ya maana,wote walijawa na uwoga na wasiwasi mwingi,Ben akiwa anatetemeka kama katoka kunyeshewa na mvua akataka kujitetea kwakuwa yeye alikuwa amewahi namba asubuhi Mwa-li-li-mu mi mi ni me-wa…lakini alishindwa kuongea kutokana woga na kutetemeka kusiko kuwa na mfano!Emma alivoona Ben anashindwa kujitetea akaona awahi yeye kuongea ,maana aliamini kwa kujitetea kwakwe mwl kiwia angeweza kuwa elewa na asingeweza wachapa Mwalimu sisi tuliwahi namba asubuhi tukarudi kulala,mimi namba 5 na Ben namba 6. Ema ndio alikuwa kama kamkanyaga nyoka mkia ni bora ange muacha Ben na kigugumizi chake ajitetea kuliko pumba aliyo iongea Unasemaje we mtoto.??Hebu niachieni upumbavu wenu,lazima leo mkawe wa mfano,nyie mnakuja shule muda mnaotaka,mnasema mliwahi mkarudi kulala.Hahahahahaha!!nyie leo nitawafundisha adabu. Ben alikuwa haamini kama Emna alimuingiza kwenye matatizo,lakini hakuwa na njia nyingine ya kujitetea.
Walipo fika shule wakawakuta wenzao wote walio chelewa wamekusanywa kwa pamoja eneo la paredi(mstalini)Mwl KIWIA akawa anawasimulia walimu wenzake kituko alicho ambiwa na Emma kuhusu kuwahi namba nakurudi kulala,walimu wengi hawa kumshangaa sana kwakuwa walikuwa wanamjua Emma na tabia zake za kuropoka utafikiri hana ubongo hahahahahaha..!!huyo mtoto wa mzee Masumbuko si tushamzoea achana naye hutamuweza hana tofauti na baba yake,alisikika mwalimu wa darasa alilokuwa akisoma Emma.Mw kiwia alipo sikia walimu wana mwambia hata muweza Emma,alikasirika zaidi kwani Emma alikuwa mtoto mdogo hivyo asinge mshindwa Mtoto wa miaka kumi na tatu huyu hawezi kunishinda mimi huyu alidhamiria kuwafundisha adabu akawatangazia wanafunzi wengine walio chelewa wote mliochelewa nimewasamehe kwa leo, nendeni darasani nibaki na hawa wapumbavu wawili wanaojifanya wajaja wa kuwahi namba halafu wanarudi kwao kulala,nataka leo niwatie adabu,akaelekea ofisi ya walimu ambako kulikuwa na mzigo kama wakuni lakini huo ulikuwa umejaa fimbo safi za Mpera ambazo zilikatwa na Mwanafunzi maarufu pale shule kwa kuleta fimbo Daniel Kipingu.Ben baada ya kuona vile alizidi kuchanga nyikiwa zaidi baada ya kuona wamebaki wao wawili tu,wa lianza kunong’ona pale chini wao kwa wao umeona kiherehere chako cha kuropoka umeniponza,mi sikubali kuchapwa Ben alimlala mikia Emma kwasababu aliamini kama isingekuwa kuropoka kwa Emma huenda yeye leo asinge chapwa.Emma alikuwa kama hasikii yale malalamishi ya Ben,alizidi kutafakari lile lundo la bakora nene,zilizo kauka kidogo za mti wa Mpera anazoenda kuchukuwa mwalimu Kiwia,Emma akawaza “chakufia nini?hapa lazima nifanye maujanja siwezi kuchapwa mibakora yote ile kisa kuchelewa namba,Darasani tena kunafimbo za kutojua hesabu bado pesa ya mlinzi sina!mwl atanisamehe bure kwa kweli”
************************************

Usikose sehemu ya pili,Je Emma atachapwa au atafanya maujanja gani?

Acha maoni yako.!


 

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.