S1Ep5A;CHEKA NA KAKA EMMA(SCHOOL COMMEDY)

0

SEHEMU 05
Mwl babu aliandika pembeni namba ya mzee Masumbuko nakwenda nayo ofisi ya walimu wote(stuff)ambako ndiko simu ya shule ilipo,aliingiza ile namba ya Mzee masumbuko na kubonyeze kitufe cha kupigia na kusubiria,simu iliita kwa muda bila kupokelewa,mwl babu hakukata tamaa aliipiga tena kwa mara ya pili nakusubiri,simu haikuita kabisa maana iliishia kuandika “user busy” kwa kuwa mwl babu alikuwa anajua mzee Masumbuko ni msumbufu kama jina lake akapiga tena mara ya tatu na mara hii simu iliita kwa sekunde chache na kupokelewa,

Mwl babu;hallow habari za saa hizi,naitwa mwl bamenya mwl mkuu msaidizi wa shule msingi mwi…..!

Mzee masumbuko;akadakia kabla mwl babu hajamalizia kujitambulisha na sauti yake ya kilevi nakufa_h_amu bwa_na ba_me_nya,Leo si_sijakuona ha_hapa maeneo

Mwl bamenya; Mzee masumbuko kuna tatizo limejitokeza hapa shuleni kijana wako amepata ajali.

Mzee masumbuko;Acha u_ooongo wewe mwanangu amepata ajali..??(alihoji) kwanza huko shule amefwata nini leo?

Mwl bamenya;alikuendelea na masomo  kama kawaida ndipo hilo tukio lili mkuta.

Mzeemasumbuko;Pumbaaavu!! nyie walimu ndio mnatuharibia maadili ya watoto,

Mwl babu;mzee masumbuko unanikosea heshima.

Mzeemasumbuko;Aaaaagghh…!!mama watoto ananipigia anasema kijana anataka hela ya kanisani nikatuma sadaka kijana wangu leo aende kanisani alafu wewe unanambia amepata ajali akiwa shule,unataka kuniambia leo kanisa limehamia shule.

Mwl babu;kanisani leo akafanyaje??mzee masumbuko tafadhali naomba uje shule mara moja.

Mzee masumbuko;(akauliza kwa upole)kwani bamenya leo lini..?

Mwl babu;leo ni juma tatu,kwani wewe unajua leo ni lini..??

Mzee masumbuko;mi najua leo jumapili ndo maana jana sijarudi nyumbani ili niimalizie weekend hapahapa..daah..!!

Mwl babu;pole sana mzee,basi sasa naomba uje tujadiliane.

Mzee masumbuko;subiri kwanza..!!kama leo ni juma tatu mbona asubuhi mama watoto alisema Emma hataki kwenda kanisani bila hela ya nauli na sadaka.

Mwl babu;mmmh hilo sijui
kwakweli!!labda alikuwa anaomba pesa ya mlinzi na chakula cha machana,na ijumaa ilyo pita niliona jina la Emma lilikuwepo kwenye majina ya wanao daiwa.

Mzee masumbuko;pombe ikiwa kama imeanza kupungua kichwani kweli pombe sio chai.!!hebu nielezee kilichotokea maana naskia mwanao kapata ajali ya bodaboda sijui..

Mwl babu;hapana masumbuko si ajali ya bodaboda,kili chotokea ni…(alimuelezea tukio zima)

Mzee masumbuko;aaaah!!mungu wangu(alihuzunika sana)nakuja sasa hivi.

Mwl babu;usijali mzee kijana yuko katika hali nzuri.

Mzee masumbuko;sawa bamenya asante,nakuja sasa hivi,kwanza pesa ya pombe imesha niishia hapa nakunywa ofa tu.

Mwl babu;asante! mwl bamenya alikakata simu na kurudi ofisi ambako alimuacha Emma peke yake akisubiria.”unafanya nini tena huko kwenye meza yangu,kiki potea hata kitu kimoja baba yako atakuja kulipia” Emma alipo sikia habari za baba yake kuja akashangaa,huku akiwa anatoka kule ilipokuwa meza ya mwl babu ikabidi amuulize vizuri mwl babu “umeongea nae akasema nakuja huku shule au kasema utakutana nae huko kwenye pombe zenu, maana yule mzee namjua tangu ijumaa iliyo pita hadi leo hajarudi nyumbani mwl babu akamwambia eandelee kusubilia kwenye kochi,kwani yeye alikuwa anataka kuendelea na kazi zake na hakuwa anataka usumbufu.Emma alikaa kimya akiwa haamini kama kweli mwl babu ameongea na baba yake wakaelewana vizuri na sasa yuko njiani anakuja.mwl babu aliendelea na ratiba zake huku Emma akiwa amepitiwa na usingizi palepale kwenye kochi la ofisi.
********************
Mzee masumbuko alitoka pale bar akiwa anayumba yumba kwa kuwa alikuwa amelewa chakali,alianza taratibu safari ya kuelekea shule alikoitwa “huyu mtoto ananipashida kweli yani(alianza kuongea mwenyewe)itabidi niache pombe kabisaaa maana inafanya hadi nasahau siku,mi najua leo ni juma pili kumbe juma tatu,pombe pumbaaaavu !! sinywi tenaa..” aliendelea kuongea mwenyewe akionesha kuchukia ile tabia yake ya ulevi huku akijitahidi kujikongoja kuelekea shule alikoitwa.Akiwa njiani nyuma kidogo ya kiwanda cha mikate kulikuwa na shimo kubwa ambalo huwa wanainchi waeneo hilo walilitumia kwa kutupia takataka mbalimbali.Siku hiyo palikiwa pame tupwa chupa nyingi za bia mzee Masumbuko alipo ziona alikasirika sana jambo lilofanya ashuke kwenye lile shimo kwa jaziba nakubingilika mpaka pale zilipo kuwapo zile chupa za pombe “nyie wa shenzi mmeniharibia maisha yangu sana,leo mtanikoma” akaanza kuokota chupa moja baada ya nyingine, Ya kwanza alii tikisa kwa hasira kisha “we mshenzi umesababisha nikafukuzwa kazi” akaitupa chini kwa hasira ikapasuka.Ya pili,nayo aliitikisa kwa hasira kisha akasema “wewe mwanaharamu kwasababu yako ulifanya nika tumbukia kwenye shimo la choo nika vunja mguu” akaitupa chini ikapasuka.
Ya tatu;hiyo nayo pia aliitikisa kwa jazba nyingi kisha akasema “kwasababu yako umfanya niisahau familaia yangu ,nalala nje kama mdudu” akaitupa chini ikapasuka.
Ya nne;nayo aliiokota alipotaka kuitikisa alimshinda ikaanguka ikapasuka na kumwagika kwa kuwa ilikuwa haijatumika “mzee Masumbuko alivona vile alisikitika sana “Ah aha aha!!nisamehe sana mimi nilijuwa wote mnatabia mbaya kumbe hapa mmechanganyika wazuri na wabaya,sasa nikikuta bado hujatumika utakaa upande wangu wa kulia nyie hamna tabia mbaya na nyie wengine kama mmeshatumika mtakaa huku kushoto mtakuwa na tabia mbaya nitawapasupasua kama wengine” baada ya hapo mzee Masumbuko alizitenga zile ambazo hazijatumika akazinywa zote bila hata kujali kuwa zilitupwa kwakuwa zilikuwa hazifai kwa kutumika tena,baada ya saa alizidiwa na pombe akalala palepale jalalani…..ITAENDELEA
*************

Na Mpishi wa Furaha KAKA EMMA

 

 

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.