S1Ep09;CHEKA NA KAKA EMMA(School Commedy)

0

             Sehemu09
Huko darasani Emma aliona kama hakuna sababu ya kutoka saa kumi na mbili kwasababu Mwl wa hesabu alitoa kazi ya kufanya akaondoka zake,alichofanya nikupiga chabo kazi ya Daniel kipingu na kumaliza,akaenda zake kugonga kengele ilihali yeye sio Timekeeper wanafunzi wote walitawanyika kuelekea Makwao,lakini Emma na kundi lake walipitia kwenye mabanda ya sinema nakufanya arudi nyumbani saa mbili usiku na kukumkuta mama yake akiwa amejawa na hasira “wewe siulirudishwa leo ukiwa unaumwa haya ukatoka ukaelekea wapi..?”
Emma alimjibu mama yake kwa upole sana kwani alijua aaipo kaa vizuri anaweza kula makofi yasio na idadi “mimi nilirudi zangu shule kwenye vipindi vya jioni vya hesabu”
Mama Emma alivo sikia habari za mwl wa hesabu akashangaa sana “hivi wewe mtoto unamatatizo gani wewe si uligongwa na huyohyuo mwl wa hesabu hadi ukajikojolea,kwahiyo ulirudi na nguo zako zenye mikojo,ugongwe tena ili ukajinyee sasa” Emma aliona mama yake keshaanza maneno yake akamtania “zilikauka mama,alafuma ujue mimi ndo kichwa wao wa hesabu pale darasani” Mama Emma baada ya uskia vile alimcheka mwanae kwa kebehi kwani alijua mwanae hajui hesabu “hehehehe halooo wewe kichwa gani wa hesabu hata table hujui,hebu nenda ukaoga uje ule ukajisomee,maana naskia harufu ya mikojo tu hapa” Emma aliona mama yake hamuamini kabisaa “mama hizo sasa zarau,unajua mimi ndo nitakukomboa.”
Mama Emma alivosikia atakombolewa na Emma alizidi kucheka “hebu nitokee hapa unikomboe we yesu.”
Emma alishindwa maneno na mama yake akaenda zake kuoga na kisha alipata chakula pamoja na mama yake.Wakiwa pale mezani Emma anajua mama yake huwa anapenda stori za umbea umbea hivyo alianza  kumuhadithia matukio yote yalio tokea huko shule ya ugomvi wa mwl babu na mwl mkuu kitu kilichomfanya Mama emma kushangaa “heeh! Hivi yule babu anamatatizo gani kwa uzee ule anapiga na vijana si atatolewa macho.”
Emma aliendelea kumhadithia umahiri wa mwl babu na kitendo alicho mfanyiwa mwl mkuu na Baba yake.Walie ndelea na stori mtu na mama yake hadi wakasahau kama Emma alitakiwa kuendelea kusoma table hadi ilipo fika mida ya saa nne usiku “heeh we mtoto si hujui table wewe..!!na hadi sasa hivi unapiga umbea tu haya kwenda ukajisomee sasa na mimi nikapumzike” Emma alishangaa kuona mama yake ana mfokea kwa kupiga nae stori “hahaa yani wewe unaenda kulala mimi nikasome na wakati tulikuwa tunapiga wote stori” Mama Emma alivoona hawaelewani akaokota mwiko uliokuwa umezagaa maeneo yale “haya nenda kasome haraka sana nisije kuku pasua hicho kichwa nikausonga huo ubongo na huu mwiko”
Emma alianza kuondoka kichoovu kuelekea chumbani kwakwe “lakini mama huu uonevu alafu mambo ya kunipiga na mwiko kila siku shauri zako utakosa mkwe”
Mama Emma alitabasamu  “kwenda zako,huyo atakae olewa na wewe anahasara kubwa”
Emma akiwa chumbani kwake alianza  kusoma table ya kwanza akaenda ya tano nakumalizia na ya kumi  kisha   akalala,mama Emma alitoka kuja kumchungulia na kuona kimya sana akaingia hadi chumbani maana alikuwa anajua tabia ya mwanae yakupenda kulala “heeh.!!huyu mtoto haja soma chochote ,kesho utaskia oooh tumbo linaniuma sijui sijalipa hela ya mlinzi visingizio vingi ili asiende shule” mama Emma akiwa anaendelea kulalamika tabia mbaya za Emma alisikia mzee Masuumbuko akiwa anaimba nyimbo yake  ya kilevi levi huku akielekea alipo Mama Emma baada ya kukaa siku nne nje ya nyumba yake kwa kunywa pombe “we mzee hebu tuachie kelele” Mama emma alimfokea Mumewe huyo,lakini pamoja na kuwa mlevi sana wa pombe mzee Masumbuko alikuwa akimsikiliza sana mkewe kwani alikuwa akijua ukorofi wa mkewe “ushaanza ukorofi wako,ndiyo maana sipendi kulala nyumbani” Mzee masumbuko alijibu kistaarabu nakuendelea na nyimbo yake,mama Emma alivosikia ile kauli ya mumewe aliendelea kuongea peke yake huku akimshushia chandalua mwanae asing’atwe na mbu “yani wewe ndo umemrithisha huyu mtoto tabia za kijinga toto halipendi kusoma kabisaa” Mzee masumbuko alivoskia hivyo aliacha kuimba nakumjibu mkewe “hilo ndo dume la mbegu sasa,usimsumbue kabisaa,unasema hasomi lakini tangu lianze la kwanza halija wahi kurudia darasa hata siku moja” mama Emma hakutaka kuendelea kujibizana na Mumewe kwani alijua siyeye anaongea bali pombe,hivyo alizima taa ya chumba cha Emma nakutoka na kurudishia mlango vizuri,na laipotoka nje aliendelea kukutana na nyimbo za mzee masumbuko
?maisha mtelemko?
?kwangu hakuna mateso?
Mama Emma alikuwa hapendi nyimbo za Mumewe alimkataza kuendelea kuimba kwani ilikuwa ni usiku hivyo sauti ilikuwa ikisikika sana, “We mzee si nimekukataza kuimba hizo nyimbo zako unawapigia kelele majirani” Mzee masumbuko alitii amri akawa kimya,walivo anza safari ya kuelekea ndani alisikika Emma akiendelea kuimba ile nyimbo aliyo kuwa akiimba baba yake na kumfanya mzee Masumbuko kurudi pale nje ya chumba cha Emma nakuanza kuimba na mwanae
?maisha mtelemko?
?maisha si mchecheto?
?kula ni bure kulala ni bure?
mama Emma alivoona hivyo ilibido ajichekee  na kuelekea zake    ndani kwake kulala akiongea mwenyewe “khaaa kweli hii ni hasara,huyu mzee kashazoea kulala nje na mwanae kazoea kuchelewa kulala na kuamka,kweli kama baba kama mtoto.”
SEHEMU YA MWISHO
siku ya mtihani wa taifa Emma aliamka mapema kuliko mtu yoyote katika ule mtaa waliokuwa wakikaaa,sikwamba alikuwa anapenda kuwahi mtihani bali ni woga na wasiwasi mwingi aliokuwa nao na kumfanya akose usingizi,akawa anajilalamikia mwenyewe “nikiambiwa nisome kabla ya mtihani mimi nasema muda bado niacheni ni lale,sasa leo ndo nitakiona cha mtema kuni.”
Ilipofika saa kumi na nusu alfajiri aliamua kuacha shuka na kuchukuwa mswaki na kwenda kunawa uso, ili ikiwezekana anywe na chai apate kujisomea kidogo. Alipotoka nje  kulikuwa na giza la kwaida aliingia jikoni kutafuta maji bila mafanikio kwani ndoo zote zilizokuwa pale zilikuwa hazina hata tone la maji “mmmh.!!asa nitanawaje,nikianza kumgongea mama hapa na giza hili ataanza kelele” kabla haja maliza kuongea mwenyewe pembeni kidogo kwa nje ya mlango wa jikoni aliona chupa ya maji ya uhai aliiokota na kuitikisa nakukuta ina maji,Emma alifurahi sana nakuanza kunawa uso na kusukutua baada ya kuyatia tu mdomoni maji yale alistuka kitu “mmh mbona haya maji yana harufu ya tofauti” alivoona si maji ya kawaida akaona ayanywe japo funda moja ,ndipo alipo hisi koo lake kama linaungua hivi,Emma aliipenda ile ladha ya kuungua koo “khaaah..maji gani haya yana choma koo hivi,lakini matamu” akaendelea kuonja onja baada ya dakika kama tatu hivi Emma alikuwa kamaliza nusu chupa ya ile pombe ya gongo ambayo iliachwa na baba yake pindi alipo rudi nyumbani usiku wajana huku yeye akidhani ni maji,alijikuta akisikia kizunguzungu kilicho mfanya miguu kukosa nguvu nakuanza kuyumbayumba kisha kuanguka chini na kulala pale pale.

     **************************
Je Emma atafanikiwa kuamka na kwenda kufanya mtihani wataifa baada ya kunywa pombe ilio achwa na baba yake,vipi akifika kwenye chumba cha mtihani itakuwake.? USIKOSE SEHEMU YA MWISHO YA HADITHI HII.

Na KAKA EMMA..!

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.