S1Ep08;CHEKA NA KAKA EMMA(School Commedy)

0

 

               SEHEMU08
Mwl babu alifika maeneo ya Shule tangu saa kumi na moja jioni nakukuta ofisi zote zimefungwa na isipokuwa wanafunzi wa darasa la saba ambao walikuwa Wanaratiba yakubaki na Mwl Kipingu kusoma hesabu, alijaribu kumpigia simu Mwl mkuu kwa muda wote aliofika mahali pale bila mafanikio yoyote asifahamu kwa kipindihicho chote mwl mkuu alikuwa kwenye Matatizo makubwa “yani nimemsubiri hapa kwa nusu saa nzima,nampigia simu wala hataki kupokea simu zangu,nitapiga simu polisi” alijisemea moyoni maneno yale akizani labda mwl mkuu anataka kumtapeli pikipiki yake Akawaza “au kaibiwa anaona aibu kuniambia,ngoja nijaribu kumpigia kwa mara ya mwisho” alijaribu tena kuipigia ile numba ya Mwl Mkuu, muda huu iliita kwa muda mrefu na kumfanya Mwl babu akate tamaa,lakini kabla haja kata simu,upande wa pili ilisikika sauti..

Mwl mkuu;hallo mwalimu nipo njiani nakuja.

Mwl babu;sasa muda wote huo ulikuwa unafanya nini.?

Mwl mkuu;Babu tena naomba uniache maana yalio nikuta huko ni makubwa, nimeishia kutiwa makofi na huyo sijui unamuita mzee Masumbuko

Mwl babu;hahaha.. Si nilikwambia mimi kuwa ile siofamilia ukanibishia..tena uje haraka niku kabidhi haya makaratasi ya majina maana hii kazi isha nishinda..

Mwl mkuu;kwakweli hili la leo ni balaa,nipe dakika kadhaa nitakuwa hapo,kisha akakata simu,
lakini muda wote huo alikuwa anawaza kuhusiana na ukorofi wa familia ya mzee masumbuko kwanza alikuwa nawaza nijinsi gani Emma  asivo kuwa na adabu kwani baada tu ya kuachwa ofisini akawajazia wanafunzi wote wenye madeni pesa zote,hivyo kufanya hakuna Mwanafuzi hata mmoja anae daiwa na jambo la pili ni jinsi alivotaka kumsaidia Mzee masumbuko kutokana na Mipombe alokuwanywa lakini akamgeuka na kumzibua makofi yasio na idadi.
Baada ya dakika tano nikweli Mwl Mkuu alifika pale Maeneo ya shule ambapo alipanga kukutana na mwl babu,lakini tatizo lilikuwa kwa Mwl Babu ambaye muda wote alikuwa akimtolea macho Mwl mkuu tangu anatokea maeneo yale kana kwamba kunakitu kilikuwa cha tofauti sana kwa Mwl mkuu,kwa kadri alivokuwa akikaribia ndivyo sura ya Mwl babu ilivyozidi kuharibika kwa kukunja ndita,lakini kubadilika huko hakukumfanya Mwl mkuu ashindwe kumfata hadi alipo na kusimama,na alivo simama tu mwl babu alianza kwa swali aisee pikipiki yangu umepeleka wapi..?
Mwl mkuu baada yakusikia swali lile naye alijibu kwa hasira akiwa amesahau kuwa alipewa pikipiki “wewe mzee unamapepo nini…??pikpiki yako ipi ulioyo nipa?”.
Mwl babu alivoona mkuu anajifanya kama haelewi somo ikabidi ampe shule kwanza “wewe usijitie ukichaa asubuhi si uliniomba pikipiki uwahi vikao vyako huko wilayani,bila kunipa  hata mia na hisi lile kofi la kisogoni alokuzibua nalo Masumbuko lili futa kumbukumbu zote” lakini pia baada ya somo lile bado mwl mkuu alionyesha kuto lielewa kabisaa “wewe mzee unatatizo kweli mimi nimeenda na baiskeli yangu hapa na nimerudi nayo,labda kama unataka hii baiskel nikupe maana naona una njaa sana”.
Mwl babu kwa jaziba na hasira nyingi alimshika tai Mwl mkuu na kumchomoa kutoka kwenye ile baiskeli “hivi mwl nikufanye nini? Kwa miaka yote niliofanya kazi nimeishia kunumua  pikipiki harafu wewe unaniambia upuuzi gani sijui”.
Waliendelea kukamatana mashati pale na kupigana mitama bila hata aibu ya kujali kama wao ni walimu napale walipo kuwepo wanafunzi waliokuwepo darasani waliona lile tukio wakanza kukimbilia na kwenda kushuhudia,lakini walimu wale  wali endelea kupigana, Emna ambaye alirudi tena shule kwaajili ya kipindi cha jioni pamoja na wenzake hawakuwa na njia ya kuwaamulia walimu wale..lakini Emma alikuwa mtundu sana akaja na wazo “jamani pale kwenye shamba la shule  niliona upupu kama vipi twendeni tukauchukue tuje tuwamwagie” lilikuwa ni wazo la kipuuzi lakini lilipokelewa kwa shangwe kubwa na marafi zake Emma ambao hawakuwa na muda wakupoteza kwani walianza safari ya kwenda kuchukuwa upupu kwa kuwa haukuwa mbali walirudi mapema na kuwakuta walimu bado wameshikana wakwanza kupuliza upupu alikuwa ni Emma ambaye bila kuangalia uelekeo wa upepo aliupuliza ule upupu ambao haukwenda kama alivyopanga kwakuwa upupu wote ulirudi kwa Emna mwenyewe pamoja na wanafunzi wote waliokuwa nyuma yake papo hapo walianza kujikuna lakini Beny baada ya kuona ambavyo mwenzake alikosa umakini yeye alihama upande mzuri ambapo aliupuliza ule upupu vizuri ambao uliwafikia vizuri walimu nakilichotokea waliachiana na kuanza kujikuna..ilikuwa kama wanaigiza lakini ki ukweli  hapakuwa na njia nyingine zaidi ya kujikuna “hivi wewe Emma una matatizo gani?mbona mmetumwagia upupu” Emma aliona kama anaonewa kwani si yeye alie mwaga ule upupu _mimi pia nawashwa hapa..tena nyie ndo mmesababisha mlivokuwa mnapiga mlitegemea tuwasaidie nini?.”
Mwl babu alizidi kuamini kwamba ile sifamilia bali ni balaa “hii si familia yani natamani hata leo asubuhi ulivogongwa na mlango ungekufa kuliko hizi kero unazo tufanyia”
Kwa upande wa Mwl mkuu yeye alikuwa anawaza pesa za mlinzi na chakula tu  “wewe mzee acha kelele unataka kuniambia hukumbuki kabisa majina ya wanafunzi ambao hawajalipa pesa ya mlinzi” mwl babu nae hakuwa nyumaa kwani alikuwaa anawaza pikipiki yake tu we _paka wa madoadoa acha kunitia doa,kwahiyo uliuza pikipiki yangu iliupate hizo pesa za mlinzi na chakula   walianza kukamatana tena,lakini muda si muda waliona mlio wa pikipiki ukielekea ule upande wa shule na ilibidi kila mtu Akaekimya na kutaka kujua alikuwa ni nani.Baada ya ile pikipiki kufika pale ndipo walipo gundua kuwa alikuwa ni Mzee masumbuko na dereva ambae walikuwa hawa mfahamu Mzee masumbuko hakuwa na cha salamu “haya we Emma  mbona unagalagala hapo na niliambiwa umegogwa na gari,nimeenda hospitali sijakukuta au walimu wamenidanganya” hakuna alietaka kumsikiliza kwani kila mtu anajua tabia zake za pombe huwa naropoka tu na kusahau, Emma na wenzake walikimbilia darasani na kumuacha hapo pamoja na Walimu “hii pikipiki yangu umeitoa wapi..?” lilikuwa ni swali la mwl babu kwa dereva wa ile pikipiki,lakini Mzee masumbuko alijibu kwa kejeli “heeh kumbe pikipiki si yakwako mkuu.”
Mwl babu alishangaa kusikia pikipiki ni ya Mwl mkuu “atoe wapi pikipiki  huyu au ndo kakuuzia wewe ”
Mzee masumbuko ilibidi amuelezee mwl babu kilichotokea  “mwalimu wako mkuu anajikuta baba huruma anataka kunijazia watu nika mtia makofi mawili tu akachanganyikiwa akaona pikipiki imekuwa nzito akaacha pikipiki yako na kubeba baiskeli ya huyu kijana niliokuja nae na bahatii yako kama isinge kuwa huyu kijana  kuwa na tabia za kilokole ungekuwa huna pikipiki”
Mwl babu alipoona story zinakuwa nyingi na yeye shida yake ni pikipiki yake aliichukuwa na kuanza safari “kijana asante kwa ustaarabu wako chukuwa baiskeli yako” kinaja nae alianza safari ya kuondoka na baiskeli yake lakini mzee Masumbuko hakuta kuachwa pale alidandia pikipiki na kuanza safari pamoja na mwl babu “babu itabidi tupitie pale baa tukatie vyombo kidogo au unaonaje?”aliuluza mzee masumbuko, “hilo ndo  lilikuwa wazo langu haswaaa “mwl babu alijibu huku akitia gea ya pikipiki na kuvuta mafuta.
Mwalimu mkuu alishangaa sana kuona Mzee masumbuko anarudi tena kupiga vyombo bila wasiwasi huku akiwa hajala kitu chochote alienda hadi darasani nakumuuliza Emma “hivi huyu baba yako amerudi nyumbani kula kweli leo?” wanafunzi walicheka sana kwani walijua tabia za baba yake Emma.
Basi Emma akiwa anatabasamu “mimi niliwaambia huyu mzee hamta wezana nae sasa we unashangaa kurudi kula leo na wakati tangu ijumaa hajarudi nyumbani”.
Mwl mkuu alivoona kumbe hata watoto wanamtambua vizuri mzee masumbuko alijilaumu sana kwa kutaka kumfanyia usamalia wema,akaona nibora aende zake nyumba akapumzike.

Usikose Sehemu Inayofwata kwa kumalizia…..

***********Na Kaka Emma********

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.