S1Ep03;CHEKA NA KAKA EMMA(SCHOOL COMMEDY)

0

*******************************************
SEHEMU 03
“Daniel aliachia liushuzi lake tukajua kajinyea” Emma alidanganya kwa kumsingizia Daniel nakufanya kila mwanafunzi pamoja na walimu wote kuangua kicheko,walicheka kwa muda ndipo mwl mkuu ikabidi akatishe kile kicheko “kimyaaa wote mnacheka nini…?kwahiyo mtu akitoa hewa ndo mnacheka,si mlifundishwa njia mbalimbali za kutoa hewa kuweni na adabu…na wewe Daniel kwanini usiende kujambia nje” Dan alijaribu kujitetea lakini hakuna aliye weza kumuamini kweli mwl mimi sikujamba wananisingizia tu hawa.Baada ya mjadala huo mwl mkuu ilibidi aendelea kutabasamu kutokana na vituko vya Emma.Mkuu aliwasamehe Emma pamoja na mrafiki zake na kumaliza mjadala ule na kumruhusu Mwl Mgeni ajitambulishe “Goodmorning my name is Peter Walalaze i come from Dar es salaam i will be teaching You English language, what i need from You is cooperation,thank You” Baada ya utambulisho huo yalisikika makofi yalioanzishwa na mtu mmoja na kupokewa na wanafunzi wengine yakionesha ukaribisho na uelewa wa utambulisho wa Mwalimu mgeni.Mwl mkuu alikuwa anajua yale makofi yaliyo pigwa ni ya uongo maana anajua wanafunzi wake wengi hajui kiingereza hivyo hawaku muelewa ikabidi awaulize kama wameelewa “did you understand?” Wanafunzi wote walijibu kwanguvu kuonyesha wameeelewa “YES” wengine wakiitika “yeah”ilitu kuumuonyesha mwl mkuu kuwa wako vizuri katika lugha ya kiingereza. Basi mwl mkuu akafurahi baada ya kuona vijana wake wameanza kuelewa lugha “Very good!” Kimbembe kilianza pale Mwl alipoona achague mwanafunzi mmoja aelze alichokielewa,akawauliza wanafunzi “nani aeleze alicho kielewa” Wanafunzi wengi walimtaja Emma kwasababu yeye ndiyo alikuwa wa kwanza kumpigia mwl makofi ya ukaribisho,japo kuwa Emma alikuwa hapendi kujibu lakini mwl mkuu alitaka kujua je ni kweli yale makofi ya Emma yalikuwa ya kweli. “Ok Emma what is the name of our new English teacher?” Emma alivo ulizwa na yeye akauliza kana kwamba hajaskia “Name?” Mwl mkuu lirudia tena kumuuliza Emma kwani aliona kama alikuwa anaelekea kujibu swali “Yes Emma tell us his name.Emma alikuwa anajua Maana ya name tu kuwa ni jina katika sentensi hivyo aliona ni rahisi sana akawaza “Ahaa kumbe mwl mkuu anataka jina tu” Basi akampa jibu “My name is Emma masumbuko” kaulizwa jina la mwl Mgeni yeye kataja jina lake kitu kilichofanya mwl mkuu na mgeni pamoja na wanafunzi wachache walio elewa walicheka sana,mwl mkuu alizidi kuamini kama kweli kiingereza bado ni tatizo “wewe ndiyo pumba kabisa,ulivokuwa unapiga makofi namna ile nikajuwa uko vizuri kumbe kichwani ni box” mwl mkuu baada ya kuona ile aibu mbele ya mgeni ilibidi chague mwanafunzi ambaye angeweza kuelezea alichokielewa “Daniel kipingu hebu tuambie ulicho kielewa.?” Dan alikuwa yuko vizuri kichwani na ndiyo maana hata akiambiwa akalete fimbo anaenda kuleta fimbo za maana,basi alijibu “Mwl mgeni anaitwa peter walalaze anatokea daresalaam” Mwl mkuu alifurahi sana na kumsifia Dan “daah! hivi kama kiingereza chepesi kabisa ni hivi hesabu si ndo itakuwa balaaa na sidhani hatakama mnajua table nyie Wanafunzi” Walipo sikia habari za kujua table wakashtuka maana wanajua hawako vizuri katika hako kamtaa ka hesabu “mmmh leo..!!kimenukaaa..!!kaanza kuongelea mambo ya hesabu tena..!!” Upande wa Emma ndo ulikuwa shida kwani alikuwa keshazoea kutumia vibuti hadi vya table “tuombeni Mungu asije kuuanza kutuuliza table hapa tukakimbiana” Mwl mkuu aligundua kuwa vijana wake hata hesabu pia ni majanga kwani walianza kunong’ona hovyo “mbona mnaguna vipi hamjui hesabu eeh..??” Wanafunzi walishindwa kutoa majibu lakini Mwl walalaze aliingilia ule mjadala wa mwl mkuu pamoja na wanafunzi wake na kufanyaa mada ya hesabu kusahaulika kitu kilichofanya wanafunzinwa mpende nakuona atawafaa “Mwl mkuu naona inatosha kama kunamwenzao Dan amekwisha waelezea naamini watakuwa wameelewa vizuri na hawa wengine wenye vichwa vigumu kama Emma nitawafundisha kiingereza na watakuwa vizuri tu” Lakini lile tukio la Emma kuitwa anakichwa kigumu na Daniel kusifiwa lili mkwaza sana Emma na kufanya watake ahamie mbele haraka sana kwani nafanya watu wanaokaa nyuma hawajui kitu labda Daniel peke yake “wewe muachia Mishuzi urudi uliko kuwa unakaa maana huku kazi umbea baada ya maneno yale ya kejeli aliyo yatoa tena Emma kwenda kwa Dan yalisikika vizuri sana kwa mwl mkuu na kumkasirisha sana “Emma kuja hapa mbele…!!naupige magoti nimekusikia kwa maskio yangu ukiongea huo upuuzi wako, mwanzo nilikusamehe lakini kwasasa sikuachi”. Wanafunzi wengi walihuzunika sana,si kwasababu walikuwa wakimpenda sana Emma ila walijuwa kuendelea kuwepo kwa mwl mkuu kungeharibu hali ya hewa muda sio mrefu “ooh..!!keshaharibu huyu..!!mkuu ndo hatoki tena mambo ya table yataanza hapa.leo tutataftana!!” Lakini kwa ben ilikuwa tofauti kidogo kwani alimhurumia Emma akijua fika kwa pale mbele chochote kitakacho tokea lazima ataanza na yeye “we boya umeona sasa mambo yako yakuropoka sasa nenda huko mbele ukapige magoti nausivojua table ataanza na wewe kilaza..”Emma aliaelekea mbele akiwa hasikii chochote zaidi ya kutetemeka,licha yakuwa mkorofi sana darasani lakini alikuwa ni muoga wa fimbo mwalimu ni samehe sitarudia tena prince alijaribu kuomba msamaha lakini haikusaidia kitu kwa wakati ule mkuu alikuwa amekasirishwa sana na tabia mbaya ya Emma “Nasema piga magoti pale sitaki kusikia chochote kwani nilikukanya tangu mwanzo hukutaka kunisikiliza” Emma alikuwa ni kama sikio la kufa lisilo sikia dawa kwani alipofika pale mbele badala ya kupiga magoti akaanza kutafakari daah!!mambo ya aibu haya kupiga magoti mbele alafu mlango hauja fungwa madogo wakipita siwata niona mtu mzima nime pigishwa magoti” kile kitendo cha Emma cha kusimama kilizidi kumkwaza sana mwl mkuu “Wewe kichaaa unajishauri nini hapo simekwambia upige magoti haraka” Emma alivoona mwl mkuu ameanza kuvimba akaona kabla hajapasuka nibora afunge mlango wa darasa na kisha akapiga magoti kama mwl mkuu alivo mtaka afanye.
Mwl mkuu alianza kuwahusia wanafunzi kuhusiana na kuwa na tabia nzuri “acheni kuwa kama Emma tabia yake haifaikuigwa na asipo angalia atafeli mtihani wa taifa huyu” Emma aliendelea kusikiliza mawaidha ya mwl mkuu lakini akiwa amepiga magoti pale chini aliona wanafunzi wenzake wakiangalia nje kwa kupitia madirisha yaliokuwa upande wa kushoto wa darasa,ilikuwa nikama wameona tukio la kustaajabisha kila sekunde ilivozidi kwenda Emma alishuhudia hali ya utulivu wa darasa ilianza kubadilika asijue nini chakufanya kwani aliona wenzake wakianza kufungua mabegi yao nakuanza kutoa baadhi ya madftari nakuanza kusoma.

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.