S1E06;CHEKA NA KAKA EMMA(School Commedy)

0

SEHEMU YA 06
Mama Emma akiwa anaendelea kuuanda ugali wake wa motoo na maharage pamoja na dagaa zake alizo zitia ndimu vizuri,akasikia mlango unagongwa “Ngo ngo ngo! Mama Emma upo ndani.?” “mmmmh…!!” Mama Emma hakuweza kuitambua kwa haraka ile sauti aliwaza atakuwa ni nani huyo anamuulizia muda huu bila kutambua ni sauti ya nani kwani alikuwa anajua sauti yakila mtu pale mtaani,kitu kibaya zaidii ni kwamba ule mlango uliendelea kugongwa tena mara hii uligongwa kwa nguvu,mama Emma kwa kweli kile kitendo kili mkasirisha sana ikabidi aulize “khaaah..!!jamani ni nani tena huyo kwenye nyumba za watu na jua lote hili tena unanigongea mlango wangu kama baba mwenye nyumba amekuja kudai kodi.!” mara hiyohiyo ili sikika sauti nje ikijitambulisha kwa upole kidogo “samahani mama Emma ni mimi” Mama Emma alizidi kujaa hasira baada ya kuskia mtu anajitambulisha kwa kusema ni mimi “heeeh..!!we mwenzangu huna jina? ni mimi ndo nani utakuwa umekosea nyumba labda sio Mama Emma mimi” muda huu iliskika sauti ikijitambulisha tena “Mama Emma ni mimi Mwl babu ni mekuja na mwanao naomba uje ufungue mlango kuna jambo tunzungumze kidogo “Mama Emma baada ya kusikia ni mwl babu ikabidi akimbie kwenda kufungua mlango lakini kabla ya kufungua mlango akakumbuka kuna chakula amekiacha kwenye mkeka na anajua kisinge tosha ikabidi akifiche chini ya kochi moja bovubovu lilokuwa pale sebuleni,baada ya kukificha kile chakula akaenda haraka kufungua huku akitaka kujua ni nini kimempata mwanae mpaka ikafikia kuletwa na mwl babu nyumbani leo “karibu mwl babu,haya ni kitu gani tena kime mpata huyu mtoto..??? jamani mbona Emma unaniletea majanga kila siku”

Mwl babu baada ya kuona Mama Emma amechanganyikiwa kwakuwa hapakuwa tena na cha salamu ikabidi amtulize kwa kumuondoa wasiwasi kuwa hakuna kibaya kilicho tokea,waliingia ndani na kukaa pale sebuleni kwenye yale makochi ya zamani, mama Emma akiwa amekalia lile kochi lililo kuwa amefichia chakula bila kujua “mwl babu naomba unieleze kinaga ubaga ni kitu gani tena kimetokea huko shule mapaka ukaaamua kumleta huyu mtoto saa tisa hii” Mama Emma aliuliza akionyesha shauku ya kuta kajua kilicho tokea.Mwl babu alianza kumuelezea tukuio lote lilivo kuwa mpaka ikafikia Emma kugongwa na mlango hatimae kufikia kurudishwa nyumbani na mwl babu na muda wote mwl babu alivokuwa akiendelea kuhadithia tukio zima ndivyo sura ya mama Emma ilizidi kubadilika “hivyo ndivyo ilivyo kuwa,kwanza nilimpigia mzee masumbuko mapema tu lakini hakufika ndipo nikaamua nimlete mi mwenyewe hapa nyumbani” mama Emma alivosikia hayo maelezo ikabidia aamke pale kwenye kochi kwajaziba nakumuuliza mwl babu “sasa unampigia baba ake aje afanye nini??kwani Masumbuko ni daktari nasema hivi huyu mtoto mpeleke mwenyewe hospitali,unaniletea mimi nitajuaje kama damu imemwagikia kwenye ubongo,heeeh!!kweli nyie walimu wengine ni mabogus sana” Mama Emma aliendela kutokwa na maneno mengi pale sebuleni huku mwl babu akiwa anamsikiliza tu kwakuwa alikuwa anamjua mama Emma anajulikana pale mtaani kwa kuongea na kuchambana na majirani zaje kila siku,Emma alibidi aingilie kati ule mjadala baada ya kusikia kuna habari za kupelekana hospitali “mama mimi sijaumia popote,huko hospitali nenda wewe na mwl babu mimi nitabaki kulinda nyumba” Mama Emma baada ya kusikia mwanae anaongea pumba za namna hiyo ikabdi aachane nae maana anamjua Emma ni mbishi sana “heeeh..!!kweli we tahira sasa mimi niende hospitali nikafanyaje kwani mie naumwa??ndio maana ulijikojolea darasani,mjinga kabisa” Mwl babu ilibidi atulie awache mama na mwana waendelea na fujo zao kwa kuwa yeye alikuwa amechoka kwa ile safari ya kutoka shule mpaka kwa mama Emma,Mwl babu akiwa anaendelea kusikiliza ule ubishani wa mama na mwana, mwl babu aliona moshi ukiwa unatoka chini ya lile kochi bovubovu alilo kuwa amelikalia mama Emma akauliza “jamani mama Emma mbona hili kochi lina toa moshi au lina ungua” Emma na Mama yake walivosikia hivyo ilibidi wakae kimya,mama Emma aligeuka nyuma nakuangalia akaona kweli kuna vimoshi vinatoka lakini vinanukia kaharufu ka dagaa akakumbuka kuwa alikuwa ameficha chakula pale chini ya kochi,lakini akajifanya hajui kinacho endelea “heeeh.!!huu moshi wa nini tena jamani..??” Emma kwakuwa alikuwa anajua tabia za mama yake huyo huwa anapenda sana uchoyo akajua mama yake atakuwa ameficha chakula chini ya kochi,akaona atafute ujanja wa kumtetea mama yake ili aondokane na ile aibu “Mama hao watakuwa wale mapanya buku wameeanza tena kuvuta bangi” Mwl babu alivo sikia hivyo ikabidi shangae tu maana ni ajabu panya kuvuta bangi,lakini angefanyaje wakati wenye nyumba yao wanakwambia ni panya ndio wanafanya moshi utoke pale chini ya kochi lakini kiukweli mwl babu aliponzwa na shauku ya japo kuwaona hao panya wanao vuta bangi,huku akiwa anataka kuinama “jamani acheni uongo khaaah..!!hebu ni chungulie na mimi nione hao panya wanao vuta bangi” kabla haja fika chini ya uvungu wa kochi mama Emma akajitupa hapo kwenye kochi na uzito wake wote”pwaaaaaaaaa….!!!” kochi lika vunjika hapo hapo na ugali wote na dagaaa pamoja na maharage yote yakamwagika,mama Emma alikasirika,alivimba uso wa hasira kwa kile kitendo akaanza kumtukana mwl babu “we mzee ni mshenzi sana,mwanaume mzima kazi umbea tuu,unaacha kufwata kilicho kuleta kazi kuchunguza nyumba za watu nyoooooo.!!!lione ukafanya macho kama saa mbovu,mjaa laana mkubwa wewe,eti nione panya wanovuta bangi,haya chakula chungu ndo kisha mwagika umefurahi sasa??ungesema tu kama unanjaa nika kuletea tunda za ubuyu ushushie na maji,khaaaah..!!kweli kuna wanaume na magumegume,kwanza utoke nyumbani kwangu nisije kukupigia kelele za mwinzi..!!” Mama Emma aliongea kwa jaziba nyingi huku macho ya kiwa yame mtoka na mikono kaiweka kiunoni, Mwl babu alianza kuomba masamaha baada ya kuskia atapigiwa kelele za mwinzi “mama Emma samahani sana usije niitia mwizi wata niuwa mimi hawa raiya” Mama Emma alikuwa hataki tena kusikia maneno ya yule mzee,alichofanya alienda akamnyanyua pale kwenye kochi nakuanza kumkokota kama mwizi kumtoa nje,akishirikiana na Emma kumbebea bagi lake na kumtupia nje,kwa kuwa mwl babu alikuwa akijulikana sana pale,watu wa mtaa ule walijaa sana pale wakiendela kushanga Mwl babu akidhalilishwa na mama Emma,majirani walianza kuulizana”kwani vipi,jamani mama Emma kwakupenda mashari”. Ule mkusanyiko wa watu pale nje ndo ukamuongezea mama Emma hamu yakuendelea kumchamba mwl babu akasahau kama ulikuwa ni wema tu wa Mwl babu wakumletea mtoto wake nyumbani “hili jizee lizima lime acha kutufundishia watoto wetu kazi kuja kudoea vyakula kwenye nyumba za watu,eti ooh mwanao kagongwa na mlango,sasa kama anaumwa unamleta kwangu mie hospitali,wewe sema uliletwa na njaa zako,nyooooooo!!!!haya sasa chakula ndo umekosa sijui utakuala nini leo” Mama Emma aliendele kumtukana Mwl babu pale chini akiwa anajitahidi kusima baada ya kusukumwa na Mama Emma ili aondoke zake maana ilikuwa ni aibu,baadhi ya majirani nao waliendelea kumpamba “mpe mpe huyo akomee,anaacha kufundisha kazi kudoe chakula cha watu” wengine walimzomea,walio cheka walicheka,lakini mwl babu alijikaza akaamka akaokota vitabu vyake na makaratasi yake yalio mwagika pale chini baada ya Emma kutupa bagi lake,lakini chaajabu alichokiona kwenye moja ya karatasi yenye majina ya wanafunzi wa darasa la saba wanao daiwa pesa ya mlinzi ndicho haswa kilifanya aone ile familia ya mzee Masumbuko hawana jema,alipata nguvu na kutoweka eneo lile kwa haraka na kuawacha Ema,mama prince pamoja na majirani wakiendelea kumcheka wakimuita” jipu,jipu,jipu,jipu”

****USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA****

Na KAKA EMMA

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.