S01Ep4;CHEKA NA KAKA EMMA(SCHOOL COMEDY)

0

SEHEMU 04
Emma akiwa amepiga magoti mbele ya darasa akishuhudia hali ya darasa inavyo zidi kubadilika asijue nini cha kufanya kwakuwa yeye alikuwa haoni nje labda angeona kama wanafunzi wenzake labda nae angeanza kuvurugika “hamjambo wanafunzi” ilikuwa ni sauti ya mwl wa hisabati mwl kipingu alie zoea kuingia kwenye kipindi chake kwambwembwe za kufungua mlango wa darasa kwafujo na kuwasalimia wanafunzi akiwa na moto wakufundisha na asijue ndani ya chumba cha darasa kulikuwa na mwl mkuu pamoja na mwl mgeni,lakini mbaya zaidi Emma alikuwa karibu ya ule mlango amepiga magoti,kilicho mshtua mwl kipingu nikelele za wanafunzi alio wasalimia “hahahaha hahah Emma kafa..!! akome umbea..!mwl kipingu kamkomesha..!!!amezibuliwa na mlango..!!Daaah haamki tena maskini..” wanafunzi walikauka kwa vicheko baada ya kuona Emma amebamizwa na ule mlango baada ya mwl kipingu kuufungua mlango kwa fujo kama kawaida yake,mwl kipingu hakuweza kusema wala kufanya chochote alitulia vilevile akiwa ameshika mzigo wake wa fimbo mkona wa kushoto na vitabu mkono wa kulia,ilibidi mwl Mkuu awatulize wanafunzi huku naye akiwa haamini kilicho tokea maana alikuwa anashindwa kuelewa nikitugani hasa kilimpata Emma baada ya kubamizwa na lile li mlango la uso Emma alianguka chini nakulalia tumbo baada ya hapo hakufanya jambo lingine lolote Zaidi ya kuwa kimya kama kuku aliye nyeshewa na mvua.Wanafunzi nao walianza kuwa Kimya baada ya kuona mwenzao haamki kwani waliingiwa na wasiwasi na kufanya watulie na kushuhudia nini kitatokea kwa mwenzao japo kwa upande mwingine waliona furaha kwani walijua Mwl kipingu hata fundisha tena, kwani wakifundishwa na mwl kipingu lazima wachapwe
Mwl kiping akiwa na wasiwasi mwingi naye akiwa anashangaa kilicho tokea “unajua mkuu mimi nilikuwa sijaona kabisa kama hapa mlangoni kulikuwa na mwanafunzi” mwl mkuu alikuwa kachanganyikiwa sana na yale maelezo ya mwl kipingu ndo yalizidi kumvuruga zaidi na kumfanya amjibu hovyo “sasa unaniambia mimi ilinifanyeje” mwl kipingu alivoona mkuu anamjibu vibaya akazidi kumuomba msamaha mkuu wake huyo japo alikuwa kijana zaidi yake apumguze hasira wapate kufanya maamuzi sahihi “mkuu huu sio muda wakulaumiana,tushauriane tunafanyaje” Mwl mkuu alivosikia maswala ya kushauriana chakufanya alikuwa kama ndiyo anamkanyaga nyoka mkia “ushauriane na nani..??we bwege unaingia darasani kama litembo bwana namna gani wewe.” Mwl kipingu alivoona mwl mkuu anamuita bwege mbele ya watoto na wengine walianza kucheka ikabidi akae kimya. Mwl mgeni mwl walalaze aliingilia kati yale maongezi ya mwl mkuu pamoja na mwl kipingu baada yakuona yange weza kuleta ugomvi kati yao “jamani walimu hebu tuache haya malumbano mbele ya watoto na tuangalie tunamsaidiaje huyu kijana” mwl mkuu alikuwa hataki tena kusikiliza chochote kile kwani alikuwa amechanganyikiwa sana na hajui atawaeleza nini wazazi wa Emma “mwl walalaze hapa hakuna chaku saidiana,mimi naondoka zangu huyu anae jifanya anaingia darani kama trekta lakulimia atajua ni nini cha kuwaeleza wazazi wake huyu mtoto, mimi sihusiki” mwl mkuu aliuelekea mlango na kumruka Emma aliyekuwa amelala kifulifuli pale chini na kutoka zake nje akiwa hataki kuhusika kujibu mashtaka. Emma alilala pale chini alikuwa kama vile anasikia yale marumbano maana mara tu mwl mkuu alivo mruka na kupita na kutoka nje Emma alijigeuza na kulalia ubavu wa kushoto,kitendo ambacho kilianza kuonekana na wanafunzi na kufanya wajawe na furaha tele na kuanza kupiga kelele za furaha “anachezesha miguu..!!oyooooo anaamka jamani….” Mwl kipingu aliivoona lile tukio la Emma kugeuka alipata tumaini kidogo alimsogelea Emma na kuanza kumtikisa “we Emma amka kijana wangu” kwa upande wa mwl mkuu baada ya kusikia zile kelele za shangwe za wanafunzi alirudi kwa haraka na kutaka kujua kilichotokea “jamani kwani kumetokea nini mbona naskia kelele hapa” Mwl kipingu kwa kejeli na dharau “kwani we unahisi nini kimetokea, sasa hivi ndo unajifanya unajali sana,lakini mwanzo ulikimbia” mwl kipingu alitumia ile nafasi kulipiza maneno machafu ya mwl mkuu,lakini nusura ugomvi uanze tena ni Mwl walalaze aliamua kuingilia kati kwa mara ya pili “aaah walimu naomba tuangalie hali ya kijana sasa kwani kaonyesha dalili zote za kuweza kuamka” walimsikiliza mwl walalaze na ndipo Mwl kipingu alimsaidia Emma kuamka pale chini kwa kumshika mkono na kuvuta juu huku akimjulia hali yake “pole sana Emma umeumia sana??” Emma akiwa na wenge na kupepesuka akionesha kutokuwa na hali nzuri sana lakini alikuwa anajikaza mimi niko vizuri kwani kumetokea nini” Mwl mkuu aliiona hiyo hali ya kupepesuka “wewe bado hauko vizuri ulivogongwa na mlango vile bado unasema uko vizuri,inabidi twendo hospitali” Emmaalivosikia habari ya hospitali aliogopa, akaona ni bora ajikaze alimradi tu aonekane hajaumia ili asipelekwe hospital “Mwalimu mimi ndo nimegongwa na huo mlango mimi mzima wa afya sijaumia popote” Mwl walalaze nae alijaribu kumshauri “hapana kijana umeumia wewe unapaswa upelekwe hospitali hujioni ulivo na linundu kama pembe la ng’ombe……..mmmh..!!! mbona naskia harufu ya mkojo hapa” baada ya ile kauli ya mwl walalaze ya kusikia harufu ya mkojo kila mwanafunzi alitumbua macho yake mbele ili ashuhudie mkojo ulitokea wapi,Waliona kitu!ndipo kelele ba vicheko vikaanza tena “Emma kajikojolea…hahahahaha” baada ya kugundua Emma ndiyo amejikojolea walimu wote walistaajabu sana Mwl mkuu alizidi kumlaumu mwl kipingu kana kwamba alikusudia kumgonga na ule mlango “haaaah…mwl kipingu ungemuuwa huyu mtoto wa watu… Hebu twende hospitali inawezekana amepata hata shida ya ubongo..mpaka kajikijolea kweli sio mchezo”
Ben alivo sikia mwl mkuu anasema Emma inawezekana amepata shida ya ubongo alimkejeli “mmmh sipati picha kama Emma atapata matatizo ya ubongo maana hivi alivo tu nikama mkichaaa” wanafunzi walicheka sana baada yakusikia ile kauli ya Ben kwani walijua ni kweli Emma anamatatizo.Mwl kipingu alitaka kujua watampeleka vipi Emma hospitali na ile mikojo,ndipo lilitoka wazo la kumpeleka ofisi akapumzike kwanza wafwatilie hali yake “wazo zuri mkuu” Ben pamoja na wanafunzi wengine walifurahi sana asante mungu maana kwa leo sidhani kama kutakuwa na pindi la hisabati nikama maombi yao yalifika kwa Mungu,Ikatoka kauli kutoka kwa Mwl kipingu “kutokana na hali ya Emma itabidi akatibiwe hivyo basi nitaingia kufundisha kipindi kingine cha hesabu,tumeelewana..???”Ili kuwa ni kauli ya mwl kipingu iliyopikelewa na Wanafunzi kwa shangwe “Ndiyoooo..tumekuelewaaa” walijubu kwa shangwe si kwamba walifurahia mwenzao anaenda tibiwa bali tu nikwasababu hakutakuwa na kuulizana maswali ya table.
Emma pamoja na walimu walielekea ofisini huku wakiwa na harufu zake za mikojo, wanafunzi waliokuwa nje walishangaa kumuona Emma akiwa na walimu huku kaptula yake ikiwa imejaa mikojo kitu kilichofanya Emma ajiskie vibaya alijikuta anaropoka “mmmh..hii ya leo sio blue monday ni black monday” walimu walimsikia vizuri sana alichoongea, Mwl walalaze alishangaa sana,kwasababu anajua Emma kiingereza hayuko vizuri sasa inawezekanaje kuongea yale maneno,ikabidi amuulize ni kitu gani alikizungumza,Emma huku akiwa anatabasamu alijibu “nimesema nilisha wahi kuumia mguu nilipo angukiwa na kabati, ” mwl kipingu aliposikia ile kauli alishangaa sana “naomba tumuwahishe hospitali huyu mtoto maana kaanza kuchanganyikiwa kama hakumbuki hata alicho kiongea.” Mwl mkuu alipoona ule wasiwasi wa mwl kipingu alimtoa wasiwasi kwani walijua Kwa utundu wa Emma atakuwa anatania “Kwani hamja mzoe huyu pimbi,ngoja tumpeleke ofisini kwanza tuone maendeleo yake”
Walipo fika katika ofisi ya mwl mkuu ambayo anaitumia mkuu pamoja na msaidizi wake aliejulikana kama Mwl Bamenya lakini kutokana na umri wake kuwa mkubwa kuliko walimu wote wanafunzi walipenda kumwita mwl babu na yeye alifurahia kuitwa mwl babu kwani alikuwa akipenda sana utani.Mwl Bamenya(babu) alikuwa akiendelea kuandika majina ya wanafunzi walio lipa na wasio lipa pesa ya chakula pamoja na ya mlinzi,Mwl babu akiwa anaendelea na kazi zake ghafla aliona mwl mkuu na Emma wakiwa wanaingia ofisini,Emma aliambiwa apumzike pale chini kutokana na bukta yake kujaa mikojo.
Mwl babu alishanga heeh we Emma leo umekutwa na nn.??maana unanuka mikojo,na hilo bichwa kama limevimba,huyo aliyo kuzibua leo kakukomesha.” Mwl mkuu alishangaa kuona na mwl babu pamoja na kwamba hafundishi tena lakini alifahamu tabia za Emma “kumbe na ww unamfahamu huyu kijana alivo mtundu.” Mwl babu aliemuelezea mwl mkuu jinsi anavyo mfahamu vizuri “Namfahamu vizuri sana ni mtoto wa mzee mmoja mtaani kwetu anaitwa masumbuko,kifupi huyu mtoto mtaani nikichefuchefu kama haja piga mtu basi atakuwa kapigwa.” Mwl mkuu alimuelezea mwl babu tukio zima lilivo tokea na kwasababu wanafahamiana na mzee Masumbuko basi akaona amkabidhi majukumu “sasa mwl bamenya nakuachia huyu kijana naomba umfatilie, mimi naenda Wilayani kuna kikako cha walimu wakuu kitaanza muda sio mrefu.”
Mwl babu alikubali yale majukumu bila shida yoyote “usijali kabisa mkuu,hili nitadili nalo ikiwezekana nita mpigia baba yake ilitujadiliane nae.” Emma alishangaa kuskia wanataka kumpigia baba yake kwasababu anajua hatakuwa na msaada wowote kutokana na ulevi wa pombe,isitoshe tangu ijumaa hajarudi nyumbani “msimpigie baba hata kuja,labda mama anaweza kuja” mwl mkuu hakuta kusiliza ushauri wa Emma akiamini hawezi kutoa wazo lenye maana hata siku moja “wewe unatufundisha kazi sisi,mwl bamenya naoana kumpigia baba yake ilikumjulisha niwazo zuri.!!unaweza ukatumia simu ya ofisi.
**************************

Na KAKA EMMA

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.