Rosa Ree: “Tulikamatwa Na Polisi Wakati Tukishoot Video Ya Up In The Air”

Rosa Ree kutoka lebo ya The Industry inayomilikiwa na Aika na Nahreel amefunguka alichokutana nacho wakati wanashoot video ya wimbo wake mpya ‘Up In The Air’.

Rapper huyo wa kike ambaye anafanya vizuri hapa Bongo amedai kuwa wakati wanashoot video hiyo walikamatwa na polisi kwa madai kuwa waliuingilia msafara wa Rais mstaafu.

“Tulikamatwa jamani wakati tunashoot video ya ‘Up In The Air’ tukapandishwa kwenye defender tukapelekwa polisi pale Oysterbay. Walichodai kuwa tuliingilia msafara wa Rais mstaafu, actually mimi sikujua kama ni msafara japo niliuona mwanzo,” Rosa Ree amekiambia kipindi cha On The Eight cha ETV.

Hitmaker huyo wa One Time, ameongeza kuwa siku ya pili waliendelea kushot video hiyo ambayo imeongozwa na Hanscana.

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.