RANIERI ”OUT” LEICESTER CITY

0

Klabu ya soka ya Uingereza Leicester City leo hii(alhamisi) imetangaza kuachana na meneja wake Claudio Ranieri.

Ranieri aliteuliwa kuwa meneja wa Leicester Julai 2015, aliwaongoza The Foxes kuandika historia ya miaka 133 ya klabu hiyo baada ya msimu uliopita(2015/2016) kuiwezesha kunyakua ubingwa wao wa kwanza kabisa wa ligi kuu nchini Uingereza.

Meneja msaidizi Graig Shakespeare na kocha wa kikosi cha kwanza Mike Stowell watakiongoza kikosi hicho kuelekea mpambano dhidi ya Liverpool katika uwanja wa Kings Power Stadium hapo jumatatu mpaka pale meneja mpya atakapoteuliwa.

Naibu katibu wa Leicester City, Aiyawatt Srivaddhananaprabha alisema:

‘‘Huu umekuwa ni uamuzi mgumu zaidi kuwahi kuufanya katika kipindi cha miaka saba iliyopita tangu King Power wawe mmiliki wa Leicester City’’
‘‘Claudio ni kocha mzuri, ameleta mabadilko makubwa katika kikosi chetu kwa kweli hatutamsahau na siku zote tutamshukuru kwa kile alichotusaidia kukipata.
Lakini maslahi ya timu inabidi yawekwe mbele ya vitu vyote’’

Alisema Srivaddhananaprabha.

Leicester wanapigania wasishuke daraja ikiwa ni miezi sita sasa tangu msimu huu wa ligi kuu nchini Uingereza uanze, ambapo wamejikusanyia pointi 21 tuu wakiwa nafasi ya 17 kwenye msimamo wa ligi baada ya kucheza michezo 23 ya ligi hiyo.

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.