Raila Odinga Aamua kumkodia Ndege binafsi Alikiba

Hit maker’ wa wimbo Seduce Me, Alikiba inadaiwa alikodiwa ndege binafsi na kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga mwishoni mwa wiki.

Imeelezwa mwanamuziki huyo alialikwa kusherekea kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi wa Urais nchini Kenya uliofanyika mwishoni mwa mwezi uliopita yaliyompa ushindi Rais Uhuru Kenyatta.

Kufutwa kwa matokeo hayo kulipokewa kwa shangwe na Muungano wa Nasa unaongozwa na Raila Odinga ambaye wafuasi wake wamembatiza jina la Joshua au Baba.

“Ni kweli (Alikiba) ameitwa Kenya lakini nisingependa kulizungumzia hilo kwa undani. Kikubwa niwashukuru Watanzania na niwaombe tuendelee kusapoti muziki mzuri kutoka kwa Kiba na wanamuziki wote wa Rockstar,”
 Aidan Charlie alimweleza mwandishi wa Gazeti la Daily Nation la Kenya.

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.