Pambano La Ndondi Kati Ya Chriss Brown Na Soulja Boy, Sasa Evender Holyfield Kumnoa Soulja Boy

0

 

Soulja Boy ameamua kujiweka karibu na kocha wa uzito wa juu kujiandaa na pambano lake la ndondi na Chris Brown.

Mtandao wa TMZ umeripoti kuwa, rapper huyo sasa atanolewa na Evander Holyfield, badala ya Floyd Mayweather. Promota wa Soulja, Wack 100, amedai kuwa walimtafuta bingwa huyo wa zamani na kuwaunganisha wawili hao kwa simu.

Amedai kuwa Soulja ndiye aliyempendekeza Evander, akimuaminisha kuwa anatilia uzito pambano lake na Chris. Mtandao huo umeripoti kuwa Soulja alikuwa akijitapa muda wote kuhusu kumtwanga KO Chris, lakini Evender alimpa ushauri wa haraka kuwa, ajifue zaidi, na aongee kidogo.

Evander anadaiwa kumpa moyo Soulja kuwa atamwandaa ili aweze kutimiza azma yake ya kumpeleka chini mpinzani wake. Kama ilivyokuwa imeripotiwa awali, Chris ananolewa na Mike Tyson, hasimu wa zamani wa Evander aliyewahi kumng’ata sikio.

Kuhusu sababu za Floyd kuacha kumnoa rapper huyo, imedaiwa kuwa anahisi yuko busy na mambo mengine na kwamba hawana tofauti yoyote.

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.