NJIA TANO(5) ZA KUKUFANYA UONGEZE UFANISI KATIKA KAZI YAKO

0

Uwe ni mmiliki wa biashara au ni mwajiriwa, kuna uwezekano mkubwa ukawa unafikiria kuhusu kuboresha ufanisi wako kazini. Ufanisi huongeza utendaji wa biashara, faida, na huinua morali ya wafanyakazi, na ufanisi una uhusiano wa karibu sana na tija. Hapa chini utaona mambo kumi ya kufanya ili uwe na tija zaidi kazini.

1.Uwe na Mpangilio.

Kuwa na mpangilio ni hatua ya kwanza kuelekea kuwa mfanyakazi mwenye ufanisi na tija, lakini, inawezekana hauna mpangilio kama vile unavyojua unapaswa kuwa. Kuanzia yale makaratasi kwenye dawati lako mpaka mafaili yaliyopo kwenye kompyuta, kuwa na mpangilio ni ujuzi mhimu sana kujifunza. Kama ukiweza kuwa na mazingira yaliyopangiliwa vizuri si tu utaweza kuzipata taarifa kwa muda mfupi pindi unazihitaji, lakini pia hali hii itakuongezea morali. Kwa sababu usafi na mpangilio ni vichocheo vikubwa vya kufanya mtu ajisikie vizuri,vinasaidia kuleta utulivu,vinaongeza umakini,na kuongeza morali; kukisha kuwa na morali ufanisi pia utakuwepo.

2. Punguza vishawishi vinavyoweza kuondoa umakini wako.

Ingawa msamiati wa ‘’kufanya kazi zaidi ya moja kwa wakati mmoja’’ unatumika sana katika jamii hii ya leo yenye kutingwa na majukumu, ukweli wa mambo ni kuwa ni watu wachache sana wana ujuzi wa kufanya kazi zaidi ya moja kwa wakati mmoja. Ukitoa watu wachache, wanadamu wanaweza kufanya kwa ufanisi jukumu moja tu kwa wakati mmoja, kwa hiyo, katika mazingira ya kawaida, kufanya kazi zaidi ya moja inabidi kuepukwe.

Labda kama jukumu moja sio la msingi, kujaribu mambo mawili kwa wakati mmoja,utakuwa huyatilii maanani majukumu yote mawili. Kwa hiyo, ili kuchochea ufanisi na tija kazini, punguza vishawishi vinavyokuzunguka ili kuboresha umakini wako. Kila wakati inapowezekana, simu za mkononi ziwekwe katika hali ya mtetemo, viashiria vya barua pepe zilizoingia vizimwe, na uangalie barua pepe kwa wakati maalumu. Kama wazo la kuwa mbali na teknolojia linasababisha upaniki, jiipe moyo, na kumbuka si zamani sana jamii ilifanya kazi vizuri bila barua pepe na simu za mikononi.

3. Jifunze kuweka vipaumbele.

Kuwa na vipaumbele ni mhimu sana katika kufanyika mfanyakazi mwenye ufanisi. Kama hauna ujuzi katika kuweka vipaumbele, baadhi ya majukumu yako ya mhimu kabisa yanaweza yasikamalizike, au mzigo wa majukumu yako utaanza kuwa mkubwa sana. Namna bora ya kuweka vipaumbele ni kuandaa orodha ya majukumu ya kufanya. Yachanganue majukumu mpaka upate maagizo maalumu, na halafu yapange kulingana na umhimu wake (kutegemeana na ukubwa wake, namna kila jukumu linavyoathirika na muda, kujipongeza).
Unapokuwa unaifanyia kazi orodha yako ya majukumu,hakikisha hauanzi kwanza kufanya jukumu jepesi ili ujione una ufanisi. Baada ya kuwa umeyapangilia majukumu yako kutokana na umuhimu wake, ni mhimu uyakamilishi katika mpangilio huo.

4.Tenga muda maalumu kwa ajili yako.

Tambua ni muda gani katika siku unakuwa na morali zaidi na ufanisi zaidi,na uyaweke majukumu mhimu ndani ya muda huo. Kwa kuweka muda maalumu kwa majukumu Fulani unasaidia kudhibiti tabia ya kuahirisha. Tegemea angalau kiwango Fulani cha vitu ambavyo hukivipanga na uviingize katika ratiba yako ya kila siku. Ili uendelee kubaki katika msitari, jipongeze baada ya kufikia malengo Fulani. Kwa mfano, kama umeweza kudumu na mpango wako kwa kipindi maalumu cha muda, jipe mapumziko ya dakika kumi, unaweza kwenda kwennye mitandao ya kijamii,nk. Hakikisha kuwa utaweza kurudi kwenye jukumu lako mara baada ya mapumziko.

5. Maliza matatizo ya nyumbani.

Maisha ya nyumbani na kazini hayajaachana sana kama zamani, teknolojia imechangia kwa sehemu, na kama maisha yako ya nyumbani yamejaa purukushani na kusongwa sana, ufanisi wako kazini hautakuwa mzuri. Matatizo na mwenzi wako, shida ya kifedha, na tu ile hali ya kusongwa,vyote vinahusika katika kuathiri utendaji wa waajiriwa kazini, lakini mambo haya yakirekebishwa, si tu utendaji kazi wa wafanyakazi hawa utaongezeka ila furaha yao itaongezeka. Kuna namna nyingi za kupambana na msongo wa mawazo nyumbani, ikiwa ni pamoja na mazoezi, kutafakari, kula mulo kamili, kumuona mwanasaikolojia, na kadhalika. Ili wafanyakazi wawe katika kiwango cha ujuu cha ubora wao, wanapaswa kuhakikisha kuwa wanalala muda wa kutosha, kutumia muda wa kutosha na familia zao, na kufanya juhudi kuhakikisha maisha ya nyumbani yanakuwa bora na hayakosi kitu.

Ingawa ufanisi wako kazini unaweza usiwe wa kiwango cha juu kabisa kinachoweza kufikiwa,kuna namna nyingi unaweza kuzitumia kuboresha utendaji wako. Kwa kujipanga, kuweka vipaumbele, na kugawa majukumu, unaweza kufanya majukumu mhimu ndani ya muda uliopangwa. Kupunguza vishawishi vinavyoondoa umakini ni mhimu sana, kwa kuwa wanadamu kwa asili hawana ujuzi wa kufanya jukumu zaidi ya moja kwa wakati mmoja. Na mwisho, kwa kuwa haiwezekani kuyaacha maisha ya nyumbani nyumbani na kwa kuwa matatizo ya nyumbani siku zote hupunguza ufanisi kazini, ni lazima ufanye kila kitu kupunguza matatizo na ukosefu wa furaha nyumbani. Na matokeo yake wewe na kampuni yako mtakuwa na furaha zaidi.

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.