JE UTAJUAJE KAMA UNAKIPAJI ?, HIZI HAPA NJIA KUU NNE(4) ZITAKAZO KUWEZESHA KUTAMBUA KIPAJI CHAKO

0

Zipo namna mbalimbali za kelezea maana halisi ya neno KIPAJI,lakini kwa uelewa ambao Mungu kanijalia na weza kuelezea kipaji katika TABIA kuu tatu(3) 1.Kipaji ni UWEZO 2.Kipaji ni kitu CHA ASILI 3.kipaji ni CHATOFAUTI.Kwa kutazama tu hizi tabia Tatu tunaweza kupata picha kodogo kuwa tunapozungumzia KIPAJI tunaongelea Uwezo wandani ambao mwanadamu anazaliwa nao(kutoka kwa Mungu),Uwezo huu unamwezesha mwanadamu kufanya jambo husika kwanamna yatofauti na wengine.
Kuwa na kipaji ni swala moja dogo,lakini kutambua kama unakipaji gani ni swala lingine gumu sana kwa watu wengi ambao nimekutana nao!KUMBUKA!Unaapokosea kutambua kipaji chako ulicho zaliwa nacho na ukafajaribu kufanya kipaji cha mtu mwingine italeta Madhara makubwa sana hasa ktk swala la Hisia!Ushawahi kuwaza mtu Mwenye ulemavu wakuongea ambae amejaliwa KIPAJI cha Uandishi wa story akakosea na kujiaminisha kuwa anakipaji cha uimbaji AU yule ambae shuleni alikuwa akiambiwa achole Microscope anachola mchoro unafanana na jagi si jagi torch si torc, lakini bila kutambua kipaji chake kuwa ni uimbaji akajiingiza ktk uchoraji,labda nikuhakikishie tu kuwa Michoro naoe watanunua Marafiki zake alio soma nao kidato cha kwanza kipindi hicho ili wakaendelee kucheka wakiwa nyumbani na watoto wao!
Zifautazo ni njia nne(4)nyepesi sana ambazo ukizingatia kwa uzuri kabisa ninahakika baada ya kumaliza tu kusoma makala hii utakuwa umetambua kipaji chako;-
  1. ULIZA WATU
Hii ni njia rahisi ya kwanza ambayo wala haihitaji uwe na Elimu ya chuo kikuu ili uwezekuuliza.Nasema ni rahisi kwasababu kama mbavyo hujui unapoelekea unakuwa wakwanza kuuliza nakupata majibu ya unapoelekea,basi hata katika maswala ya kutambua KIPAJI au uwezo wako unaweza kuuliza Marafiki,Wazazi,Majirani au yoyote yule ambae unaamini anaweza kukupa majibu ya kweli na si masikhara.Wala usitumie nguvu saana kuuliza!Iko hivi!ukiwa umekaa maskani na washkaji mnapiga story basi tumia nafasi hiyo hiyo uliza“JAMANI KWA TULIVO ISHI WOTE KWA MUDA HUU,MNADHANI MIMi NITAKUWA NA KIPAJI GANI.?”Nakuhakishia ni swali dogo sana lakini litakupa majibu mengi mno mbayo kwa kiasi kikubwa utapata muelekeo wakwenda kutambua kipaji chako!
 2. SIKILIZA WATU WANASEMA NINI JUU YA UWEZO WAKO.
Wanao kuzunguka wanakufahamu zaidi!zingatia sana pale ambapo unafanya jambo alafu mtu anakusifia au naweza asikusifie lakini akasema “DAAH JAMAA UNACHEKESHA..” hapa napo unahitaji mganga kujua wewe ni Eric Omondi ajae.“EEH BWANA UNAJUA KUCHORA” jamani!!na hapa unataka malaika wa vita ukubabadulie kuwa wewe ni Masoud Kipanya,wakati mwingine wanaweza tumia lugha za kejeli,NDIYO!wanahaki si Marafiki zako,ukisikia “WE MJINGA HILI LI SAUTI LAKO LILIVO KUWA BAYA UNGEKUWA MSANII WA HIPHOP UNGE BAMBA SANA” Kaka usikasirike kuitwa MJINGA,BWEGE SAUTI BAYA wewe zingatia maneno haya“UNGEKUWA MSANII WA HIPHOP” & “UNGE BAMBA SANA” haya maneno machache yanatosha saana kukuonyesha kuwa wewe ni mrithi wa ChidBenz.
3.KITU GANI UNAKIFANYA KWA URAHISI?
Kabla hatuja endelea mbele,hebu tumia walau dakika tano kujiuliza je?nijambo gani au kazi gani ambayo unaifanya kwa urahisi!Natumaini umekwisha pata majibu mengi sana!ONGEZEA!Jambo hilo au kazi hiyo inafikia wenzako wengine wamekuwa wakiona hiyo kwao nikama adhabu lakini wewe Umekuwa ukishukuru na kufanya jambo au kazi hiyo kama unasukuma mlevi kwenye Matope.Kama umeendelea kupata majibu basi Kaka yangu ni kwambie hicho ndio kipaji chako,Dada yangu huo ndio uwezo wako wa tofauti Mungu aliokujalia,Komaa humohumo wala usitetereke na Mungu ni mwaminifu iko siku moja utakuja kusema “Kaka Emma ulisema” namimi nitakujibu kwatabasamu paana kabisa “SIKUSEMA,NILIANDIKA LAKINI IMEKUWA”
     4.KITU GANI UKIKIFANYA UNAFURAHI?
Nimekuwa balozi wa FURAHA na nitaendelea kuwa balozi mpaka pale kila mtu dunia atakapo kuwa na furaha,hivyo basi nitakuwa sijajitendea haki kama sitamalizia na hili swali au njia nyingine ndogo lakini ya Muhimu sana ktk kuwezasha kutambua Kipaji chako.SIKILIZA!Kipaji ni uwezo waasili wakufanya jambo fulani,Uwezo huu unaotoka kwa MUNGU,kama unaweza kupigia mstari neno “kutoka kwa MUNGU ”pigia!Kitu ambacho Umepewa na Mungu kama zawadi nilazima Uifurahie na upende kuifanya wala usijiskie aibu au kuwa na manung’uniko wakati wakuifanya!NDUGU!ukiona Jambo au kazi fulani uifanyapo unajiskia amani,furaha Komaa humo humo wala usitetereke ndo Kipaji chako hiko mwanawane!

Wewe ni watofauti,Una uwezo watofauti ndani yako!Ninaamini kabisa kama umepitia Vizuri hatua zote kwa umakini kabisa Utakuwa umetambua Kipajia chako!Mungu ni wetu sote!Mungu ni mwaminifu.

soma makala nyingine bofya hapa

Usiache kutoa maoni yako

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.