NIKKI WA PILI NA G-NAKO WAMTOLEA MAPOVU YOUNG KILLER KUTOKANA NA KAULI YAKE YA JOH MAKIN KUBEBWA

0

 

 

Ngoma mpya ya Young Killer, Sinaga Swagga ina utata mwingi. Mmoja wa mstari ambao tayari umeanza kumtokea puani rapper huyo ni ule usemao, wanasema Joh anabebwa mpaka nahisi ni ukweli

Joh Makini hana jibu lenye hasira kama wengi wanavyotarajia kwasababu kwenye mahojiano na kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, rapper huyo alisema,” Hiyo kamba, hiyo mbeleko hiyo toka 2005 mpaka mpaka 2015 basi hiyo kamba ngumu.”

Jibu lilikuwa tofauti kwa G-Nako aliyesema, “Sometimes watu kama hawa wanakuwa wanaongea tu kwasababu wanataka wasikike kwamba kuna vitu wanaviongea kwenye mistari, inabidi wakifika kwenye interview kama hapa muwe mnawachallenge, kwamba wewe umeongea hivi kwenye mistari yako, umeshafuatilia hiki na hiki? Maake sio mistari tu.”

Kwa upande wake Nick wa Pili alisema, “tatizo ninaloliona katika mstari kama huo ni kwamba unaharibu history sababu Joh amefanya kazi kubwa sana so tunategemea artist wadogo si lazima kumjua Joh Makini ila kuijua historia ya Joh Makini sababu pale ndo kuna mafunzo mengi ya kujifunza.”

Ameongeza, “Kwahiyo anavyokuja mtu akitoa neno kama hilo anaharibu ile historia sio kwa Joh, kwa mtu ambaye anakuja mdogo. Mtu ambaye anatakiwa kumjua Dullah hatakiwi kumjua leo, unatakiwa kujua Dullah alianzaje kufika hapa kwasababu kila mtu anaanza moja, unaweza ukarelate na hiyo story kikawaida.”

Joh alirejea tena kuelezea kwanini mambo kama hayo huwa hajibu akisema, “Katika historia ya interview yangu na jinsi ambavyo nafanya kazi, huwa sitoi nafasi kwenye vitu vya kipuuzi, navipaga tu mgongo naendelea na mambo yangu ya msingi sababu end of the day hata nitakachosema, hakitaleta maana sababu kama hawajui history.”

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.