Ndoa Ya Dogo Janja Na Irene Uwoya Bado Ni Gumzo..!!?

Mwanamuziki wa Bongo Fleva anayetamba na ngoma ya Ngarenaro, Dogo Janja akifanya yake muigizaji wa filamu, Irene Uwoya, ambaye kwa sasa anaitwa Sheila.

Eh! Bwana kweli! Mwanamuziki wa Bongo Fleva anayetamba na ngoma ya Ngarenaro, Dogo Janja,  amethibitisha kumuoa muigizaji wa filamu, Irene Uwoya, ambaye kwa sasa anaitwa Sheila.

Akifanya mahojiano na Redio ya Clouds katika Kipindi cha Leo Tena, Dogo Janja amesema kwamba aliamua kumuoa mwanamke huyo kwa kuwa tu moyo wake ulimsukuma kufanya hivyo kutokana na  upendo mkubwa aliokuwanao kwake.

“Sikulazimishwa! Niliamua kwa moyo wangu kumuoa Sheila. Nilipeleka posa, ikakubaliwa na hatimaye kufunga ndoa,” alisema Dogo Janja ila baada ya kuulizwa mahali ndoa ilipofungwa, hakuwa wazi kulijibu hilo.

Akiendelea kufanya mahojiano kwenye kipindi hicho kuhusu kuoa mtu ambaye tayari ni mke wa mtu aliyefunga ndoa kanisa Katoliki na mumewe Ndikumana ‘Katauti’ raia wa Burundi ambaye hawajawahi kutalikiana, Dogo Janja alisema yeye si mtu sahihi wa kujibu hilo ambapo alisema mtu sahihi wa kulijibu ni Irene.

Dogo alimsifia mkewe huyo akisema wakati anamfuata hakutia maanani kwamba ni staa, alimchukulia tu kwamba ni mtu wa kawaida ambaye ana matunzo ya kawaida si ya gharama kama wanavyodhani watu wengine.

Aliendelea kumsifia mrembo huyo akisema anampenda na angemshirikisha mambo yake yote ambayo hawezi kumwambia mtu mwingine na kwamba anamwamini.

Kuhusu kuthohudhuria kwa mama yake kwenye harusi hiyo, alisema alimwambia mama yake anayeishi Arusha ambaye alimjibu kuwa jambo hilo alisimamie mwanamuziki wa Bongo Fleva, Hamad Ali   ‘Madee’ ambaye amemleta mwanamuziki huyo hapa mjini tangu anatokea jijini Arusha miaka kadhaa iliyopita hadi sasa.

Ndoa hiyo alidai ilifungwa Ijumaa iliyopita wakati wa sala ya adhuhuri huko Mikocheni, jijini Dar es Salaam ambapo miongoni mwa watu maarufu waliohudhuria ni Madee, msimamizi wa ndoa hiyo, Kassim Mganga, mwigizaji wa filamu, Blandina Chagula ‘Johari’ waigizaji Monalisa, Natasha na wengineo kibao.

Ndoa hiyo imeendelea kuleta mkanganyiko katika mitandao ya jamii ambapo watu wengi hawaamini wakidhani kwamba ni maigizo kama anavyosema Irene Uwoya kwamba yote hayo yalikuwa ni maigizo ya muvi.

‘Muvi’ itaishaje? Tusubiri tuone!

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.