Namna ya kumfanya Boyfriend wako aku Propose(Kukuvisha Pete): Mambo 10 ya kumfanya akuvishe Pete

Mpo katika mapenzi mazito na yenye furaha iliyo ya juu kabisa, lakini hajawahi kukuuliza lile swali. Zifuatazo ni tips kubwa zitakazomfanya mwanaume wako aombe muoane(propose)

Wanawake wengi huiwazia sana makubwa hii siku tangu wakiwa wadogo. Gauni zuri jeupe, na refu, kutembea kwenye kapeti jekundu lenye maua ya nakshi, kumuona mwanaume wa ndoto zako anakusubiri pale mbele – inapendeza sana. Lakini unawezaje sasa kuyafanya haya mawazo yako yawe halisi na mpenzi wako aombe muoane?

Hii ina mtego sana ndani yake. kama unadhani/ unafikiri huu ni muda muafaka wa kupeleka uhusiano wako katika level nyingine na uwe katika ndoa kabisa, hicho ni kitu chema. Lakini mara nyingi,

 mwenzako anaweza kuwa halitambui hili jambo. Kuvishwa pete ni hatua kubwa na linahitaji ujasiri, kwa hiyo unatakiwa kumfanya ajue huu ndo muda muafaka bila ya kusita. Unaweza kuta hajakuvisha pete kwa sababu haujafanya vitu vya kumshawishi aku propose.

Namna ya kumshawishi boyfriend wako akuvishe Pete
Nini cha kufanya? Zifuatazo ni tips 10 ambazo zitamfikishia ujumbe kuwa wewe ni wife material.

#1 Kuwa mpole – Tulia! Kitu kibaya kinachoweza kumfanya boyfriend wako asiwe hata na wazo la kukuvisha pete ni wewe kuwa unahangaika – kiruka njia, hautulii. Hii itamfanya akutilie shaka na hivyo kukushushia CV, kitakachofata atakuona haufai na kwenda kumtafuta mwingine.

Unaweza kuwa umekata tamaa ya kwamba hautaolewa tena, lakini unatakiwa utambue ya kwamba hili jambo ni kubwa na litabadilisha sura nzima ya maisha yake. Kama wewe utakuwa unamshinikiza na kumuwekea presha nyingi ili akuoe utamfanya akutulie shaka, ha hutavishwa pete. [Soma: Ishara 13 zinazoashiria anataka akuoe na anatamani kuishi na wewe!]

#2 Mwambie. Wakati ukizingatia suala la kuwa mtulivu, bado unatakiwa uhakikishe kuwa yeye anajua kuwa wewe unataka uolewe naye – aelewe kuwa unataka muishi wote. Kama utakuwa mpole wa kupitiliza na kushindwa kumueleza, hatakuwa na wazo la kwamba wewe unataka uishi naye, hivyo, atakosa msukumo kwa vile hataona ulazima wako wewe kutaka kuishi nae – hivyo hatakuuliza lile swali.

Kama mmekuwa mkitoka kwa pamoja kwa muda mrefu, lazima itakuwa mlishaongelea masuala yenu ya baadae. Lakini kama haukuwahi kuongelea hilo jambo la ndoa, mfanye ajue kabisa kuwa mawazo yako ni nini juu ya uhusiano wenu. Angalao hapo atajua kichwa chako umekielekeza wapi. [soma: Sababu 11 za kwanini hajakuomba muoane!]

#3 Usijilinganishe wewe na wenzako. Eti kwa sababu marafiki zako walishaolewa miaka miwili iliyopita, na wewe bado hauyjaolewa, haimaanishi kwamba sasa ni zamu yako. Kila uhusiano ni tofauti, na watu wengine huitaji muda mrefu kidogo wa kujiandaa zaidi ya wengine.
Kama utaendelea kueleza jinsi wenzako walivyokuzunguka walivyo olewa, ataone kama unamlazimisha na pia atajua hauna utayari wa wewe kuolewa ila unataka uolewe kwa sababu wenzako wote walishaolewa – hivyo anaweza asikutilie maanani. Hili ni jambo muhimu sana usilisahau.

#4 Usimfanye awe na chaguo (Dont give hi a choice). Hii inaweza kukushtusha kidogo, lakini kwa kumfanya yeye ndo achague, ni kama vile unampa “mlango wa kutokea” ambapo anaweza aseme bado hajapanga kuoa, kama yeye hajisikii kuoa kwa wakati huo.
Usifanye hilo jambo kuwa la uhuru kihivyo. Kwa kusema maneno kama “Unadhani tutaoana miaka miwili ijayo?” ni vizuri kwa sababu itampa frame ya muda wa yeye kujipanga na kufikiria kuhusu hilo jambo pia. [Soma: Mwanaume na Mwanamke wanaotaka ‘kutoka’ wote V.s Mwanaume na Mwanamke wanaotaka kuoana!]

#5 Mfanye aone na ajisikie kwaba hawezi kuishi bila wewe. Kama unataka kweli uvishwe pete na boyfriend wako, inatakiwa uwe umemfanyia mambo ambayo yeye mwenyewe yatamfanya aseme kuwa wewe ndiye yule ‘the one’ na utavishwa pete pale tu atakapo tambua hilo. Unatakiwa umfanye ajisikie kama akikupoteza wewe, ataumia moyo na atakosa mengi – atajiona mpungufu [Soma: Mambo 15 ya kumfanyia mwanaume unaempenda akuwaze muda wote!]

#6 Share kila kitu na yeye. Kadri anavojiona wa karibu na wewe, ndivyo atakavyokua na shauku kubwa ya kutaka kukuoa. Kama anaweza kujihisi kuwa wewe ni mtu wa pekee anayeweza kumuamini kuliko wote duniani, na mtu ambaye unaweza kuishi nae – kwamba unamchukulia na kumpenda alivyo – bila ya kusita atatamani muishi wote – hapo pete lazima itue mkononi.

#7 Jifunzeni kutoka out na wenzenu alio oana(married couples). Kuwaona marafiki zenu walio oana wanaishi kwa furaha, itamfanya aone ndoa siyo kitu kigumu kama wengi wanavyodai, na hii itamfanya awe tayari kula kiapo cha kuishi na wewe.

Muda mwingine anaweza kuogopa kuwa mkioana unaweza kubadilika – maana hii ni hofu ya wanaume wengi, lakini inatakiwa umuoneshe jinsi ambavyo ndoa za wengine zilivyofanikiwa – hiyo lazima imchote moyo. Kama una marafiki zako ambao tayari wameshaoana, hii inaweza kukupa jeki – kwa namna ambayo wanaweza kuwaambia jinsi maisha ya ndoa yalivyo ya furaha.[Soma: Sababu 20 za kuoa/kuolewa na kuishi maisha ya furaha baada ya ndoa!]

#8 Ijenge ndoa yako taratibu. Usiteke tu harakaharaka uolewe – ijenge ndoa yako taratibu hata kabla ya ndoa yenyewe – na ijenge mpaka ifikie point ambayo ndoa inatakiwa liwe ni jambo au hatua inayofuata.

Kuyasogeza mahusiano yenu mbele na kwa utaratibu wa namna hii, itafanya yale mabadiliko(transition) yaonekane kuwa marahisi na hii itamfanya aropoke tu kuwa anataka muoane
Kwa hiyo kama bado mna date, unaweza ukawa unajitengenezea njia kwa namna hiyo. Usife moyo, taratibu tu utafika – kumbuka mambo mazuri hayataki haraka.[Soma: Nimuone? Ishara 17 zinazoashiria “Ndiyo”!]

#9 Jitahidi sana usiwe Tegemezi. Kuwa na maisha yako ya kujitegemea nje ya uhusiano wenu ni jambo jema, haijalishi unakuwa unawaza kuhusu ndoa au la!. Pia, kumuonesha kuwa wewe ni mwanamke unayejitegemea, na kumpa uhuru wa kuwa na maisha yake na afurahie mambo licha ya wewe kutokuwepo, itamuonesha kuwa unamwamini – na unataka kumuweka huru.

Kwa kufanya hivyo – itaimarisha uhusiano wenu na kumfanya yeye ajisikie tayari kuubeba msalaba wa nyie kuoana.[Soma: Jinsi ya kumfanya mwanaume akuoe fasta – njia 10 zilizothibitika!]

#10 Yakubali mawazo / maamuzi yake. Mwisho wa siku, hauwezi kumlazimisha mtu akuoe! Kama hayupo tayari kuingia katika ndoa, likubali lakini unatakiwa ulifanyie kazi hili wazo. Usipotezee sana na pia usichukie sana.

Inaweza ikawa kwamba anahitaji muda zaidi wa kulifanya hili jambo limuingie kichwani. Na wakati huo, kama hali ya uhusiano inakuruhusu usubiri – utajua tu. Na kama siyo – utajua pia, na hivyo itakua muda mzuri wa kumtafuta mwingine ambaye ataweza kukubali wazo lako!.

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.