Mwanafunzi darasa la tatu apigwa mimba

Mwanafunzi mwenye umri wa miaka 13 wa darasa la tatu katika shule ya msingi Makutano, kitongoji cha Igole kijiji cha Makutano wilayani Kilombero amelazimika kukatizwa masomo yake kwa kufukuzwa shule baada ya kupewa ujauzito.

Mtuhumiwa anayesadikiwa kutenda kosa hilo Samuel Daudi  ametoroka  na kwenda kusikojulikana.

Hali ya mimba za utotoni kwa wanafunzi wakiwemo wa shule za msingi wilayani Kilombero inadaiwa kuchangiwa na sababu mbalimbali ikiwemo vishawishi na kurubuniwa kwa wasichana wadogo kutokana na umbali wa shule hizo na makazi ya watu, ambapo wazazi wa binti huyo ambaye hutembea umbali mrefu sana kwenda shule, wamesema hawakugundua mapema kama kwa umri wake binti yao angeweza kubebeshwa ujauzito.

Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Makutano, Fabian Undole amesema wamekuwa na taratibu za kuwapima afya wanafunzi wa kike shuleni hapo kila baada ya miezi mitatu na kwamba jamii ya wafugaji imekuwa ikiongoza kwa matatizo hayo.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero Denis Londo amekiri changamoto kama hizo kujitokeza katika baadhi ya maeneo ingawa wameendelea kuchukua hatua kali na sasa wanaongeza nguvu kudhibiti kabisa hali hiyo.

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.