Mourinho anusurika kwenda jela

Kocha Jose Mourinho amelipa faini na kufutiwa kesi iliyokuwa inamkabili ya kukwepa kodi nchini Hispania kati ya mwaka 2011 na 2012 akiwa kocha wa Real Madrid.

Mourinho alikuwa anatuhumiwa kukwepa kodi ambayo ni kiasi cha Euro milioni 3.3 zaidi ya bilioni 8,100 za Kitanzania. Kesi yake imemalizika leo kwenye mahakama ya Pozuelo de Alcarcon jijini Madrid.

Baada ya kutoka mahakamani mchana huu Mourinho ameongea na wanahabari ambapo amesema kuwa kesi yake imemalizika baada ya kulipa faini na sasa yupo huru.

“Kesi imeisha na sijajibu lolote kwasababu sikuwa na hoja ila nimelipa na kusaini na serikali kuwa sina tena tuhuma na kesi imefungwa ndiyo maana niko hapa, hakuna kitu kingine chochote”, Mourinho amewaambia Wanahabari.

Mourinho anatarajiwa kusafiri mchana huu kwa ndege binafsi kurejea jijini Manchester kwaajili ya kusafiri na timu kuelekea jijini London ambapo Jumapili timu yake itacheza na Chelsea kwenye mchezo wa EPL.

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.