Mdogo Wake Vanessa (Mimi Mars) Afunguka Kuhusu Vanessa Na Jux

Msanii wa Bongo Fleva, Mimi Mars ambaye ni mdogo wake Vanessa Mdee amezungumzia taarifa za kuachana kati ya dada yake na Jux.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya ‘Dedee’, amesema hawezi kujua kama kweli wameachana ila bado anawaona pamoja.

“Unajua bado wanawasiliana, wanaongea kwa hiyo sielewi, (mambo ya mapenzi) kuna kuachana, kuna kurudiana kwa hiyo hatuwezi kujua hicho kitu kilichokuwa kinapita hapo katikati kilikuwa nini,” Mimi Mars amekiambia kipindi cha Twenzetu cha Times FM.

Alipoulizwa kama anadate na msanii yeyote katika Bongo Fleva au alishafikiria kufanya hivyo ili kupanda kimuziki, Mimi Mars alijibu, “hapana kabisa, kuzushiwa nimezushiwa lakini sijawahi kuwa na mtu kwenye Bongo Fleva”.

“Kwangu mimi si kitu ambacho nisingetaka kufanya, so sijui kama ingenishusha au kunipandisha, ni kitu ambacho hakipo katika dictionary yangu,” amesema Mimi Mars.

 

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.