Mcheza Tenisi Venus Williams Ahusishwa Na Mauji

Afisa mmoja wa kituo cha polisi cha Palm Beach Gardens mjini Florida amesema nyota wa mchezo wa tenisi Venus Williams amehusika katika ajali ya barabarani iliyosababisha kifo cha mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 78.

Msemaji huyo wa polisi alithibitisha hilo kupitia combo cha Jabari cha BBC kuwa mtu mmoja alipelekwa hospitali baada ya ajali hiyo iliofanyika tarehe 9 ya mwezi Juni na kufariki wiki mbili baadaye kutokana na majeraha ,alisema.

Kulingana na chombo cha habari cha TMZ, ambacho kilitoa habari hiyo, maafisa wa polisi wanamlaumu Williams kusababisha ajali inayoonekana imesababishwa na uzembe wakati alipokuwa akiendesha gari kini wakili wa mwana dada huyo amesema ilikuwa ajali tu.

Mwanaume huyo aliyefariki dunia, Jerome Barson, alikuwa akisafiri na mke wake aliyekuwa akiendesha gari hilo kupitia eneo la makutano wakati ajali hiyo ilipotokea.

Mke wa marehemu, Bi Barson pia alipelekwa hospitalini kufuatia hajali hiyo lakini baadae akapata unafuu na kuruhusiwa na madaktari.

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.