MATUMIZI YA KONDOMU ZA KIKE ZA “LADY PEPETA”

Kondomu za kike ni mipira nyororo kabisa inayovaliwa katika uke wakati wa kufanya mapenzi ili kuzuia mimba na kupunguza uwezekano wa kupata maambukizi ya magongwa ya zinaa. Huenda kukawa na aina nyingi za kondomu za kike, lakini hapa ninaangazia kondomu aina ya “Lady Pepeta”ambayo ni mashuhuri.

Wakati wa kufanya mapenzi kwa wapenzi wawili, ni jukumu la kila mmoja wenu kujilinda kwanza peke yake bila kujali kuwa swala la kinga ni jukumu la mmoja wenu. Wanawake kwa kiasi kikubwa wamekuwa hawafanyi maamuzi pekee katika swala la kutumia kinga, kwani imezoeleka kuwa wanaume ndio wanaopaswa kuvaa kondomu.

Itakuwa ni dhana potofu endapo ukimtegemea mwenzio akulinde kwa kuvaa ndomu wakati wote, unapaswa kujadiliana na mwenzi wako na kufanya maamuazi sahihi kuwa nani anapaswa kuvaa kinga kwa wakati huo. Lady Pepeta ni kondomu ya kike ambayo ni rahisi kabisa kuvaa na ukafurahia tendo la kufanya mapenzi.

 

MASWALI NA MAJIBU KUHUSUKONDOMUYA LADY PEPETA


1. Je ninaweza kutumia Lady Pepeta moja zaidi ya mara moja?
Hapana isitumike zaidi ya mara moja. Tumia Lady Pepeta kwa kila tendo la ngono.

2. Je kunawakati maalum ambapo sipaswi  kutumia Lady Pepeta?
Hapana. Unaweza kutumia Lady Pepeta wakati wowote, hata kama uko kwenye hedhi.

3. Je nivae Lady Pepeta muda gani kabla ya kujamiiana?
Unaweza kuvaa Lady Pepeta hadi masaa sita kabla ya kujamiiana.

4. Je ninaweza kutumia Lady Pepeta na njia nyingine za uzazi wa mpango? 
Ndio. unaweza kutumia Lady Pepeta na njia nyingine za uzazi wa mpango kama vile, vidonge, kitanzi na njia za asili. Usitumie kondomu ya kiume unapotumia Lady Pepeta. Msuguano wa kondomu mbili unaweza kupasua kondomu. Kumbuka kondomu ikitumika kila mara kwa usahihi hupunguza hatari ya maambukizi ya magonjwa yasababishwayo na ngono zembe pia hupunguza uwezekano wa kupata mimba zisizotarajiwa.

5. Mafuta yaliyopakwa kwenye Lady Pepeta yanasaidia nini?
Mafuta yaliyopakwa kwenye Lady Pepeta yanarahisisha uume kuingia na kutoka kirahisi ukeni wakati wa kujamiiana. Mafuta yaliyopo upande wa nje humsaidia mvaaji wakati wa kuvaa..

6. Je Lady Pepeta inachanika wakati wa kujamiiana?
Hapana. Lady Pepeta si rahisi kuchanika wakati wa kujamiiana.

7. Je Lady Pepeta inaweza kuzama na kupotea ndani ya mwili wangu?
Hapana. Lady Pepeta haiwezi kuzama wala kupotea mwilini. Mlango wa kizazi ni mdogo sana, saa zote huwa umejifunga.

8. Je nifanye nini iwapo uume umeingia kati ya uke na Lady Pepeta?
Endapo uume haupo ndani ya Lady Pepeta uchomoe. Hakikisha pete ya nje imekaa kwenye midomo ya uke uelekeze uume ndandi ya Lady Pepeta.

MAELEKEZO YA MATUMIZI YA KONDOMU ZA KIKE ZA “LADY PEPETA” KWA NJIA YA SAUTI… FUATILIA KIPINDI CHETU CHA “DANGER ZONE LIFE” kinachowekwa katika mtandao huu na mingineyo kila wiki na ni bure kabisa kudownload na kupata mafundisho kibao ya kijamii. “FUNGUKA OKOA JAMII”.

Lady Pepeta inatengenezwa na “The Female Helth Company” Hapa nchini inasambazwa na T-MARC kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.

 

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.