Matendo Ya Donald Trump Yanavyowapa Wakati Mgumu Waandishi Wa Filamu Za James Bond

0

Kauli na matendo tofauti ya Rais Donald Trump yamekuwa yakipingwa na baadhi ya wanasiasa na watu maarufu duniani na jambo hili halijawa geni kwenye masikio ya watu.

Hivi karibuni waandishi wa filamu za James Bond 007 wamesema dunia imekuwa tofauti sana na mtu kama Donald Trump kuwa rais na matendo anayofanya ni ngumu kuandika filamu ya James Bond sababu tayari matendo ya adui wa filamu hio yanafanyika duniani kwenye maisha ya kawaida.

Neal Purvis na Robert Wade walioandika filamu sita za mwisho za James Bond wanasema dunia imekuwa kama maisha ya filamu na sasa wanaumiza kichwa kuandika kitu tofauti na cha kutisha zaidi.

Mpaka sasa haijulikani nani atafanya filamu mpya ya James Bond baada ya mwigizaji Daniel Craig kukata ofa ya Pound milioni £120 kutoka MGM kuigiza kwenye filamu mbili za 007.

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.