MAMBO 5 MUHIMU MWANAUME UNATAKIWA KUWA NAYO KABLA YA KUWA NA MWANAMKE

0

Ukubali au Ukatae popote pale tunapo zungumzia Mahusiano Laziama tutaagalia Mfano halisi wa Binadamu wakwanza kuumbwa na Mungu.Hapa tutamtazama Adam lakini pia Hawa ambae alikuwa Ubavu wake.Mungu Haku mkabidhi Hawa kwa Adam kabla ya kuhakikisha kuwa Adam yuko tayari au anazo sifa sahihi za kuwa na Mwanamke.!Twende pamoja;-

1. UNAHITAJI UWEPO WA MUNGU
Sita kudanganya ktk hili kaka unahitaji kuwa na Mungu ktk kila eneo.Sijui unaamini ktk nini lakini Kwa Mwanaume kamili nilazima Uwe unaamini ktk Mungu.!Nikuhakikishie tu kwamba Mwanaume unahitaji Kuwa na Mungu kwanza Kabla ya kuwa na mwanamke.Mwanamke anatakiwa kukuta ukiwa unaamini ktk Mungu.

2. UNAHITAJI KUWA NA KAZI YA KUFANYA.
Hii nilazima!Kama unahisi unataka kuwa na Mwanmke bila ya kazi kaka au Baba yangu unapotea,Mwanaume ni lazima uwe na kazi ya kufanya ya kukuingizia kipato.Sikiliza Mungu alipo Muweka Adam ktk bustan haku muacha ale tu matunda na kila kilichopo pale bustanini lakini pia alimwachia KAZI kubwa ya kutunza ile bustani.!Hivyo basi kama Mwanaume unahitaji kuwa na Mwanamke kwa sasa hakikisha Unakuwa na KAZI ya kufanya ya kukuingizia kipato.

3.UWE NA UWEZO WA KUJIONGEZA
Utanielewa tu..!Kuwa na Ajira au kazi ya kufanya ni swala Moja lakini kutumia kile unachopata kutoka katika kazi yako na kufanyia maendeleo Mengine ni swala lingine!Kaka kama unataka kuwa na Mwanamke ni Muhimu kwanza Wewe kama wewe uwe na uwezo wa kutumia kila aina ya Uwezo uliopewa na Mungu ilikuleta Mabadiliko ktk uchumi wako na hata kwa jamii inayo uzunguka.

Usitegemee kupata kitu kutoka kwa mwanamke.Mwanamke atahitaji kupata ushauri na Mawazo kutoka kwako sasa kama hujui kujiongeza kaka utweza kweli kumshauri au ndo utamwambia “BABY AMUA WEWE” utahekesha sana.!Labda tu nikukumbushe tu kuwa pale bustani ya Edeni aliyepewa majikumu yote alikuwa ni Adam na yeye ndiyo alikuwa na kazi ya kumfundisha mkwe mambo yote ambayo aliambiwa na Mungu kam Kutokula Tunda la Mti wakati.

4.UWE NA UWEZO WA KUMTENGENEZA MKEO WEWE MWENYEWE
Labda tu nikwambie mwanamke unae muwaza wewe ktk mawazo yako hayupo dunia hii.!hivyo niwajibu wako wewe kama mwanaume kumtengeneza mwanamke unaemtaka wewe mwenyewe!Skiliza usije ukamchukuwa mwanamke ndani ya mwezi mmoja usha mchoka eti kisa ni mnene,ukion ivyo ujue bado haukuwa tayari kuwa na mwanamke.Iko hivi kaka Mwanaume ambaye yuko tayari kuwa na mwanamke ni yule Ambaye mwanamke wake akiwa hajui kuongea kiingereza vizuri anafanya uamuzi wa kwenda kumlipia mkewe pesa ili afundishwe kiingereza,Mwanaume ambaye yuko tayari kukaa na Mwanamke ni yule ambaye akiona mwanamke wake anavaa nguo za kishambashamba anafanya uwamuzi wakumpeleka kwenye duka kubwa la NGUO na kumchagulia Nguo nzuri za kisasa nazo zipenda yeye.

5. UNAHITAJI KUWA NA UWEZO WA KUMLINDA MWANAMKE WAKO.
Mungu alivo kuumba mwanaume alikupa mwili mkubwa wenye misuli mikuwa na mifupa komavu zaidi ya mwanamke si kwasababu ya kumpigia mkeo la! Ni kwaajili ya kumlinda mwanamke wako.Kabla ya kuwa na mwanamke ni lazima uwe unamtazamo wa kumlinda mwanamke wako kwa hali yoyote ile.

Labda tu ni malizie kwa kusema kama huna hizo sifa au hivyo vitu vitano Muhimu tulivo vizungumizia bapo juu unakila sababu ya kubaki peke yako kwa Muda wako wote mpaka pale utakapo kuwa na sifa hizi.

Na KAKA EMMA

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.