Mambo Matano Ya Kufahamu Kuhusu Mpenzi Mpya Wa Rihanna Bilionea Hassan Jameel

1. Ana miaka 29: Hassan Jameel anaumri wa miaka 29 kama Rihanna

2. Ni mfanya biashara kutoka Saudi Arabia: Hassan Jameel ni makamu mwenyekiti wa biashara ya familia ya mzee Abdul Latif Jameel iliyoanza kazi toka mwaka 1955, kampuni hii ina haki za kusambaza magari ya Toyota huko Saudi Arabia na ni miongoni mwa kampuni kubwa duniani.

3. Ana Ligi yake mwenyewe ya mpira, Matajiri tofauti duniani wana timu za mpira, huyu jamaa ana ligi yake mwenyewe inaitwa Jameel League.

4. Ni Billionaire: Kampuni yao inathamani ya dola bilioni $1.5 na Jameel ataridhi kampuni hii siku moja, Forbes wanasema familia ya Jameel ni familia ya 12 tajiri zaidi kwenye nchi za kiarabu.

5. Aliwahi kuwa na mahusiano na mwanamitindo Naomi Campbell: Sio mara ya kwanza Hassan Jameel anatoka na mwanamke staa, alikuwa na mahusiano na mwanamitindo Naomi Campbell.

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.