MAHUSIANO KABLA YA NDOA, MSICHANA NA KIJANA WA KIUME.

Asanteni tena kwa kujumuika nasi hapa katika ukurasa huu unaolenga kuwafungua watu katika maswala mbali mbali ya kijamii, yanayokwamisha maendeleo ya watu pamoja na kusambalatisha mahusiano ya watu.

Leo tunaangalia mambo ya kuzingatia kabla ya kuingia katika ndoa, na hapa wengi huenda nikaenda tofauti nao, lakini ni jukumu langu kuelimisha jamii na sio kuifurahisha tuu. Kila mtu anafahamu neno mahusiano ya kirafiki kati ya jinsia mbili tofauti.

Kabla ya kuingia katika ndoa, lazima ufanye urafiki na mtu unayetaka kumuoa au kuolewa naye, ili uweze kubaini tabia na mwenendo wake kama unaendana na wakwako, au anamatatizo gani ya kiafya au kiukoo pia.

Tumekuwa tukikimbilia kufanya mapenzi ili kupima uwezo wa injini kama inahimili safari na kusahau usukani wa gari, kwani gari haliwezi kukufikisha pale unapotaka kwenda bila ya kuwa na uskani (staring).

Kwa wachumba na wasio wachumba yani Girlfriend na Boyfriend, kama kweli unampango wa kumuoa au kuolewa, ni vyema usiendekeze kufanya mapenzi na mwenzi wako, kwani kufanya mapenzi na rafiki yako unayetarajia kumuoa au kuolewa naye, hupunguza upendo au hisia na shauku ya kutaka kuishi kama mume na mke kwa baadae.

Kama kimwili utampa mpenzi wako kila kitu anachokitaka, then nini kitakuwa kimebakia katika mwili wako ambacho atakuwa na shauku ya kutaka kukipata? Hisia kubwa ya ndoa ni mapenzi na kupata watoto, na ndio maana wasichana wengi wanachelewa kuolewa au hata hawawezi kuolewa kwasababu hawana mipaka katika maamuzi ya mapenzi.

Kunanjia nyingi za kumridhisha mpenzi wako na akasahau kukuomba kufanya….., zipo nitaziweka katika makala ijayo, lakini cha msingi ni wewe kijana kujitunza na hata kama unafanya mambo haya fanya lakini mbakizie mkeo au mumeo ili akikuona kila siku anakuona ni kama kitu kipya.

Kwanini usijiulize ni kwanini nyumba ndogo zina dominate sana katika maswala ya unyumba? Ni kwasababu wanajipanga na kuonekana kila siku ni wapya kwa wapenzi wao, wanawasoma wapenzi wao na kujua wape madhaifu yalipo. Sasa basi wewe msichana weka mipaka katika mwili wako utaonekana wa thamani sana! Hata wewe kijana wa kiume muonyesha mpenzi wako kuwa unamalengo nae na mapenzi ni sehemu tu.

Tukutane katika makala nyingine za kusisimua kama, vitu vya kufanya na ukasahau mapenzi katika mahusiano kabla ya ndoa.

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.