Mahakama Kuu yasema hili kuhusu Lulu

Mahakama Kuu jijini Dar es salaam, imesema muigizaji Elizabeth Michael (Lulu) ana kesi ya kujibu dhidi ya tuhuma za kuuwawa kwa msanii Steven Kanumba , hivyo anatakiwa kujitetea.

Taarifa hiyo imetolewa leo na Mahakama kuu baada ya kufunga kusikiliza ushahidi upande wa mashtaka na kumtaka muigizaji huyo kuanza kujiandaa kwa ajili ya kutoa utetezi wake.

Wakili wa Elizabeth, Peter Kibatala ambaye ndiye anayemtetea muigizaji huyo, aliomba muda wa dakika 40 ili wajiandae kufanya hivyo, na kesi yake inasikilizwa tena saa 5 asubuhi hii.

Endelea kubaki nasi kwa taarifa zaidi

 

JICHOLAUSWAZI TUMETOA UPDATE YA APP YETU DOWNLOAD >BOFYA HAPA< KUIPATA MPYA SASA NA UFURAHIE HABARI MOTO MOTO

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.