MAGUFULI APANDA NDEGE KWENDA ETHIOPIA..!!!

0

RAIS John Magufuli ameondoka nchini na kuelekea Addis Ababa, Ethiopia ambako atahudhuria Mkutano Kilele wa 28 wa Wakuu wa Nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) unaoendelea nchini humo.
Ziara hiyo ni ya kwanza kwa Rais Magufuli kutoka nje ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) tangu aingie madarakani kuongoza Serikali ya Awamu ya Tano Novemba 5, mwaka jana.
Taarifa iliyotolewa na Ikulu Dar es Salaam jana ilisema katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wa jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli aliagwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Wengine waliojumuika kumuaga Rais Magufuli ni viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Paul Makonda.
Kwa mujibu wa Ikulu ya Dar es Salaam, pamoja na kuhudhuria mkutano huo, akiwa Addis Ababa, Rais Magufuli anatarajiwa kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa Bara la Afrika wanaohudhuria mkutano huo.
Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.